聖經新譯本 (Simplified)

Swahili: New Testament

Revelation

22

1天使又指示我一道明亮如水晶的生命水的河流,从 神和羊羔的宝座那里流出来,
1Kisha malaika akanionyesha mto wa maji ya uzima maangavu kama kioo yakitoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu na Mwanakondoo.
2经过城里的街道。河的两边有生命树,结十二次果子,每月都结果子;树叶可以医治列国。
2Mto huo ulitiririka kupitia katikati ya barabara kuu ya mji. Kandokando ya mto huo kulikuwa na mti wa uzima unaozaa matunda mara kumi na mbili kwa mwaka, yaani kila mwezi; na majani yake ni dawa ya kuwaponya watu wa mataifa.
3所有咒诅都不再有了。城里有 神和羊羔的宝座,他的仆人都要事奉他,
3Hapana kitu chochote kilicholaaniwa kitakachokuwa katika mji huo. Kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwanakondoo kitakuwa katika mji huo, na watumishi wake watamwabudu.
4也要见他的面。他的名字必写在他们的额上。
4Watauona uso wake, na jina lake litaandikwa juu ya paji za nyuso zao.
5不再有黑夜了,他们也不需要灯光或日光了,因为主 神要光照他们。他们要作王,直到永永远远。
5Usiku hautakuwako tena, wala hawatahitaji mwanga wa taa au wa jua, maana Bwana Mungu atawaangazia, nao watatawala milele na milele.
6耶稣再来天使对我说:“这些话是可信的、真实的!主,就是众先知之灵的 神,差遣了他的天使,把那快要发生的事,指示他的仆人。”
6Kisha malaika akaniambia, "Maneno haya ni ya kweli na ya kuaminika. Bwana Mungu ambaye huwapa manabii Roho wake, alimtuma malaika wake awaonyeshe watumishi wake mambo ambayo lazima yatukie punde.
7“看哪!我必快来!那遵守这书上预言的人是有福的!”
7"Sikiliza! Naja upesi. Heri yake anayeyazingatia maneno ya unabii yaliyo katika kitabu hiki."
8听见又看见了这些事的,就是我约翰。我听见又看见了之后,就俯伏在指示我这些事的天使脚前要拜他。
8Mimi Yohane, niliyaona na kusikia mambo haya. Nilipokwisha sikia na kuona nikajitupa chini mbele ya miguu ya huyo malaika aliyenionyesha mambo hayo, nikataka kumwabudu.
9他对我说:“千万不可以这样!我和你,以及你的弟兄众先知,还有那些遵守这书上的话的人,都是同作仆人的。你应当敬拜 神。”
9Lakini yeye akaniambia, "Acha! Mimi ni mtumishi tu kama wewe na ndugu zako manabii na wote wanaoyatii maagizo yaliyomo katika kitabu hiki. Mwabudu Mungu!"
10他又对我说:“不要封住这书上的预言,因为时候近了。
10Tena akaniambia, "Usiyafiche kama siri maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, maana wakati wa kutimizwa kwake umekaribia.
11不义的,要他仍旧不义;污秽的,要他仍旧污秽;行义的,要他仍旧行义;圣洁的,要他仍旧圣洁。”
11Kwa sasa anayetenda mabaya na aendelee kutenda mabaya, na aliye mchafu aendelee kuwa mchafu. Mwenye kutenda mema na azidi kutenda mema, na aliye mtakatifu na azidi kuwa mtakatifu."
12“看哪,我必快来!赏赐在我,我要照着各人所行的报应他。
12"Sikiliza!" Asema Yesu, "Naja upesi, pamoja na tuzo nitakalompa kila mmoja kufuatana na matendo yake.
13我是阿拉法,是俄梅格;我是首先的,也是末后的;我是创始的,也是成终的。”
13Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho, wa kwanza na wa mwisho."
14那些洗净自己袍子的人是有福的!他们可以有权到生命树那里,也可以从门进到城里。
14Heri yao wale wanaoosha mavazi yao, kwani watakuwa na haki ya kula tunda la mti wa uzima, na haki ya kuingia mjini kwa kupitia milango yake.
15在城外,有那些狗,那些行邪术的、淫乱的、杀人的、拜偶像的,以及所有喜爱说谎的和实行说谎的人。
15Lakini mbwa, wachawi, wazinzi, wauaji, waabudu sanamu na wote wanaopenda kusema uongo, watakaa nje ya mji.
16“差遣了我的使者、为众教会向你们证明这些事的,就是我耶稣。我是大卫的根,又是他的后裔,我是明亮的晨星。”
16"Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu awathibitishieni mambo haya katika makanisa. Mimi ni mzawa wa ukoo wa Daudi. Mimi ni nyota angavu ya asubuhi!"
17圣灵和新娘都说:“来!”听见的人也要说:“来!”口渴的人也要来!愿意的人都要白白接受生命的水!
17Roho na Bibiarusi waseme, "Njoo!" Kila mtu asikiaye hili, na aseme, "Njoo!" Kisha, yeyote aliye na kiu na aje; anayetaka maji ya uzima na apokee bila malipo yoyote.
18我警告所有听见这书上预言的人:如果有人在这些预言上加添什么, 神必把写在这书上的灾难加在他身上。
18Mimi Yohane nawapa onyo wote wanaosikia maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki: mtu yeyote akiongeza chochote katika mambo haya, Mungu atamwongezea mabaa yaliyoandikwa katika kitabu hiki.
19如果有人从这书上的预言删减什么, 神必从这书上所记的生命树和圣城删去他的分。
19Na mtu yeyote akipunguza chochote katika maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, Mungu atamnyang'anya sehemu yake katika ule mti wa uzima, na sehemu yake katika mji mtakatifu, ambavyo vimeelezwa katika kitabu hiki.
20证明这些事的那一位说:“是的,我必快来!”阿们!主耶稣啊,请你来吧!
20Naye anayetoa ushahidi wake juu ya mambo haya asema: "Naam! Naja upesi." Amina. Na iwe hivyo! Njoo Bwana Yesu!
21愿主耶稣的恩惠与所有的圣徒同在!阿们!
21Nawatakieni nyote neema ya Bwana Yesu. Amen.