King James Version

Swahili: New Testament

1 Corinthians

12

1Now concerning spiritual gifts, brethren, I would not have you ignorant.
1Ndugu, kuhusu vipaji vya kiroho, napenda mfahamu vizuri mambo haya:
2Ye know that ye were Gentiles, carried away unto these dumb idols, even as ye were led.
2Mnajua kwamba, kabla ya kuongoka kwenu, mlitawaliwa na kupotoshwa na sanamu tupu.
3Wherefore I give you to understand, that no man speaking by the Spirit of God calleth Jesus accursed: and that no man can say that Jesus is the Lord, but by the Holy Ghost.
3Basi, jueni kwamba mtu yeyote anayeongozwa na Roho wa Mungu hawezi kusema: "Yesu alaaniwe!" Hali kadhalika, mtu yeyote hawezi kusema: "Yesu ni Bwana," asipoongozwa na Roho Mtakatifu.
4Now there are diversities of gifts, but the same Spirit.
4Vipaji vya kiroho ni vya namna nyingi, lakini Roho avitoaye ni mmoja.
5And there are differences of administrations, but the same Lord.
5Kuna namna nyingi za kutumikia, lakini Bwana anayetumikiwa ni mmoja.
6And there are diversities of operations, but it is the same God which worketh all in all.
6Kuna namna mbalimbali za kufanya kazi ya huduma, lakini Mungu ni mmoja, anayewezesha kazi zote katika wote.
7But the manifestation of the Spirit is given to every man to profit withal.
7Kila mtu hupewa mwangaza wa Roho kwa faida ya wote.
8For to one is given by the Spirit the word of wisdom; to another the word of knowledge by the same Spirit;
8Roho humpa mmoja ujumbe wa hekima, na mwingine ujumbe wa elimu apendavyo Roho huyohuyo.
9To another faith by the same Spirit; to another the gifts of healing by the same Spirit;
9Roho huyohuyo humpa mmoja imani, na humpa mwingine kipaji cha kuponya;
10To another the working of miracles; to another prophecy; to another discerning of spirits; to another divers kinds of tongues; to another the interpretation of tongues:
10humpa mmoja kipaji cha kufanya miujiza, mwingine kipaji cha kusema ujumbe wa Mungu, mwingine kipaji cha kubainisha vipaji vitokavyo kwa Roho na visivyo vya Roho; humpa mmoja kipaji cha kusema lugha ngeni, na mwingine kipaji cha kuzifafanua.
11But all these worketh that one and the selfsame Spirit, dividing to every man severally as he will.
11Hizo zote ni kazi za Roho huyohuyo mmoja, ambaye humpa kila mtu kipaji tofauti, kama apendavyo mwenyewe.
12For as the body is one, and hath many members, and all the members of that one body, being many, are one body: so also is Christ.
12Kama vile mwili ulivyo mmoja wenye viungo vingi, na viungo hivyo vyote--ingawaje ni vingi--hufanya mwili mmoja, ndivyo ilivyo pia kwa Kristo.
13For by one Spirit are we all baptized into one body, whether we be Jews or Gentiles, whether we be bond or free; and have been all made to drink into one Spirit.
13Maana sisi, tukiwa Wayahudi au watu wa mataifa mengine, watumwa au watu huru, sote tumebatizwa kwa Roho mmoja katika mwili huo mmoja; na sote tukanyweshwa Roho huyo mmoja.
14For the body is not one member, but many.
14Mwili hauna kiungo kimoja tu, bali una viungo vingi.
15If the foot shall say, Because I am not the hand, I am not of the body; is it therefore not of the body?
15Kama mguu ungejisemea: "Kwa kuwa mimi si mkono, basi mimi si mali ya mwili", je, ungekoma kuwa sehemu ya mwili? La hasha!
16And if the ear shall say, Because I am not the eye, I am not of the body; is it therefore not of the body?
16Kama sikio lingejisemea: "Kwa vile mimi si jicho, basi mimi si mali ya mwili", je, kwa hoja hiyo lingekoma kuwa sehemu ya mwili? La!
17If the whole body were an eye, where were the hearing? If the whole were hearing, where were the smelling?
17Kama mwili wote ungekuwa jicho, sikio lingekuwa wapi? Na kama mwili wote ungekuwa sikio, mtu angewezaje kunusa?
18But now hath God set the members every one of them in the body, as it hath pleased him.
18Lakini kama ilivyo, Mungu alizipanga sehemu hizo tofauti katika mwili kama alivyopenda.
19And if they were all one member, where were the body?
19Kama sehemu zote zingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?
20But now are they many members, yet but one body.
20Ukweli ni kwamba, sehemu za mwili ni nyingi, lakini mwili ni mmoja.
21And the eye cannot say unto the hand, I have no need of thee: nor again the head to the feet, I have no need of you.
21Basi, jicho haliwezi kuuambia mkono: "Sikuhitaji wewe", wala kichwa hakiwezi kuiambia miguu: "Siwahitaji ninyi."
22Nay, much more those members of the body, which seem to be more feeble, are necessary:
22Zaidi ya hayo, inaonekana kwamba sehemu zile za mwili zinazoonekana kuwa ni dhaifu ndizo zilizo muhimu zaidi.
23And those members of the body, which we think to be less honourable, upon these we bestow more abundant honour; and our uncomely parts have more abundant comeliness.
23Tena, viungo vile tunavyovifikiria kuwa havistahili heshima kubwa, ndivyo tunavyovitunza kwa uangalifu zaidi; viungo vya mwili ambavyo havionekani kuwa vizuri sana, huhifadhiwa zaidi,
24For our comely parts have no need: but God hath tempered the body together, having given more abundant honour to that part which lacked.
24ambapo viungo vingine havihitaji kushughulikiwa. Mungu mwenyewe ameuweka mwili katika mpango, akakipa heshima zaidi kiungo kile kilichopungukiwa heshima,
25That there should be no schism in the body; but that the members should have the same care one for another.
25ili kusiweko na utengano katika mwili bali viungo vyote vishughulikiane.
26And whether one member suffer, all the members suffer with it; or one member be honoured, all the members rejoice with it.
26Kama kiungo kimoja kinaumia viungo vyote huumia pamoja nacho. Kiungo kimoja kikisifiwa viungo vingine vyote hufurahi pamoja nacho.
27Now ye are the body of Christ, and members in particular.
27Basi, ninyi nyote ni mwili wa Kristo; kila mmoja wenu ni kiungo cha mwili huo.
28And God hath set some in the church, first apostles, secondarily prophets, thirdly teachers, after that miracles, then gifts of healings, helps, governments, diversities of tongues.
28Mungu ameweka katika kanisa: kwanza mitume, pili manabii, tatu walimu; kisha ameweka wale wenye kipaji cha kufanya miujiza, kuponya, kusaidia; viongozi na wenye kusema lugha ngeni.
29Are all apostles? are all prophets? are all teachers? are all workers of miracles?
29Je, wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni walimu? Wote ni wenye kipaji cha kufanya miujiza?
30Have all the gifts of healing? do all speak with tongues? do all interpret?
30Je, wote ni wenye kipaji cha kuponya? Wote ni wenye kipaji cha kusema lugha ngeni? Je, wote hufafanua lugha?
31But covet earnestly the best gifts: and yet shew I unto you a more excellent way.
31Muwe basi, na tamaa ya kupata vipaji muhimu zaidi. Nami sasa nitawaonyesheni njia bora zaidi kuliko hizi zote.