1When therefore the LORD knew how the Pharisees had heard that Jesus made and baptized more disciples than John,
1Mafarisayo walisikia kwamba Yesu alikuwa anabatiza na kuwapata wanafunzi wengi kuliko Yohane.
2(Though Jesus himself baptized not, but his disciples,)
2(Lakini ukweli ni kwamba Yesu hakuwa anabatiza ila wanafunzi wake.)
3He left Judaea, and departed again into Galilee.
3Basi, Yesu aliposikia hayo, alitoka Yudea akarudi Galilaya;
4And he must needs go through Samaria.
4na katika safari hiyo ilimbidi apitie Samaria.
5Then cometh he to a city of Samaria, which is called Sychar, near to the parcel of ground that Jacob gave to his son Joseph.
5Basi, akafika Sukari, mji mmoja wa Samaria, karibu na shamba ambalo Yakobo alikuwa amempa mwanawe, Yosefu.
6Now Jacob's well was there. Jesus therefore, being wearied with his journey, sat thus on the well: and it was about the sixth hour.
6Mahali hapo palikuwa na kisima cha Yakobo, naye Yesu, kutokana na uchovu wa safari, akaketi kando ya kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.
7There cometh a woman of Samaria to draw water: Jesus saith unto her, Give me to drink.
7Basi, mwanamke mmoja Msamaria akafika kuteka maji. Yesu akamwambia, "Nipatie maji ninywe."
8(For his disciples were gone away unto the city to buy meat.)
8(Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wamekwenda mjini kununua chakula.)
9Then saith the woman of Samaria unto him, How is it that thou, being a Jew, askest drink of me, which am a woman of Samaria? for the Jews have no dealings with the Samaritans.
9Lakini huyo mwanamke akamwambia, "Wewe ni Myahudi; mimi ni mwanamke Msamaria! Unawezaje kuniomba maji?" (Wayahudi hawakuwa na ushirikiano na Wasamaria katika matumizi ya vitu.)
10Jesus answered and said unto her, If thou knewest the gift of God, and who it is that saith to thee, Give me to drink; thou wouldest have asked of him, and he would have given thee living water.
10Yesu akamjibu, "Kama tu ungalijua zawadi ya Mungu na ni nani anayekwambia: Nipatie maji ninywe, ungalikwisha mwomba, naye angekupa maji yaliyo hai."
11The woman saith unto him, Sir, thou hast nothing to draw with, and the well is deep: from whence then hast thou that living water?
11Huyo mama akasema, "Mheshimiwa, wewe huna chombo cha kutekea maji, nacho kisima ni kirefu; utapata wapi maji yaliyo hai?
12Art thou greater than our father Jacob, which gave us the well, and drank thereof himself, and his children, and his cattle?
12Au, labda wewe wajifanya mkuu kuliko babu yetu Yakobo? Yeye alitupa sisi kisima hiki; na yeye mwenyewe, watoto wake na mifugo yake walikunywa maji ya kisima hiki."
13Jesus answered and said unto her, Whosoever drinketh of this water shall thirst again:
13Yesu akamjibu, "Kila anayekunywa maji haya ataona kiu tena.
14But whosoever drinketh of the water that I shall give him shall never thirst; but the water that I shall give him shall be in him a well of water springing up into everlasting life.
14Lakini atakayekunywa maji nitakayompa mimi, hataona kiu milele. Maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji ya uzima na kumpatia uzima wa milele."
15The woman saith unto him, Sir, give me this water, that I thirst not, neither come hither to draw.
15Huyo mwanamke akamwambia, "Mheshimiwa, nipe maji hayo ili nisione kiu tena; nisije tena mpaka hapa kuteka maji."
16Jesus saith unto her, Go, call thy husband, and come hither.
16Yesu akamwambia, "Nenda ukamwite mumeo uje naye hapa."
17The woman answered and said, I have no husband. Jesus said unto her, Thou hast well said, I have no husband:
17Huyo mwanamke akamwambia, "Mimi sina mume." Yesu akamwambia, "Umesema kweli, kwamba huna mume.
18For thou hast had five husbands; and he whom thou now hast is not thy husband: in that saidst thou truly.
18Maana umekuwa na waume watano, na huyo unayeishi naye sasa si mume wako. Hapo umesema kweli."
19The woman saith unto him, Sir, I perceive that thou art a prophet.
19Huyo Mwanamke akamwambia, "Mheshimiwa, naona ya kuwa wewe u nabii.
20Our fathers worshipped in this mountain; and ye say, that in Jerusalem is the place where men ought to worship.
20Babu zetu waliabudu juu ya mlima huu, lakini ninyi mwasema kwamba mahali pa kumwabudu Mungu ni kule Yerusalemu."
21Jesus saith unto her, Woman, believe me, the hour cometh, when ye shall neither in this mountain, nor yet at Jerusalem, worship the Father.
21Yesu akamwambia, "Niamini; wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba juu ya mlima huu, wala kule Yerusalemu.
22Ye worship ye know not what: we know what we worship: for salvation is of the Jews.
22Ninyi Wasamaria mnamwabudu yule msiyemjua, lakini sisi tunamjua huyo tunayemwabudu, kwa maana wokovu unatoka kwa Wayahudi.
23But the hour cometh, and now is, when the true worshippers shall worship the Father in spirit and in truth: for the Father seeketh such to worship him.
23Lakini wakati unakuja, tena umekwisha fika, ambapo wanaoabudu kweli, watamwabudu Baba kwa nguvu ya Roho; watu wanaomwabudu hivyo ndio Baba anaotaka.
24God is a Spirit: and they that worship him must worship him in spirit and in truth.
24Mungu ni Roho, na watu wataweza tu kumwabudu kweli kwa nguvu ya Roho wake."
25The woman saith unto him, I know that Messias cometh, which is called Christ: when he is come, he will tell us all things.
25Huyo mama akamwambia, "Najua kwamba Masiha, aitwaye Kristo, anakuja. Atakapokuja atatujulisha kila kitu."
26Jesus saith unto her, I that speak unto thee am he.
26Yesu akamwambia, "Mimi ninayesema nawe, ndiye."
27And upon this came his disciples, and marvelled that he talked with the woman: yet no man said, What seekest thou? or, Why talkest thou with her?
27Hapo wanafunzi wake wakarudi, wakastaajabu sana kuona anaongea na mwanamke. Lakini hakuna mtu aliyesema: "Unataka nini?" au, "Kwa nini unaongea na mwanamke?"
28The woman then left her waterpot, and went her way into the city, and saith to the men,
28Huyo mama akauacha mtungi wake pale, akaenda mjini na kuwaambia watu,
29Come, see a man, which told me all things that ever I did: is not this the Christ?
29"Njoni mkamwone mtu aliyeniambia mambo yote niliyotenda! Je, yawezekana kuwa yeye ndiye Kristo?"
30Then they went out of the city, and came unto him.
30Watu wakatoka mjini, wakamwendea Yesu.
31In the mean while his disciples prayed him, saying, Master, eat.
31Wakati huohuo wanafunzi wake walikuwa wanamsihi Yesu: "Mwalimu, ule chakula."
32But he said unto them, I have meat to eat that ye know not of.
32Lakini Yesu akawaambia, "Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi."
33Therefore said the disciples one to another, Hath any man brought him ought to eat?
33Wanafunzi wake wakaulizana, "Je, kuna mtu aliyemletea chakula?"
34Jesus saith unto them, My meat is to do the will of him that sent me, and to finish his work.
34Yesu akawaambia, "Chakula changu ni kufanya anachotaka yule aliyenituma na kuitimiza kazi yake.
35Say not ye, There are yet four months, and then cometh harvest? behold, I say unto you, Lift up your eyes, and look on the fields; for they are white already to harvest.
35Ninyi mwasema: Bado miezi minne tu, na wakati wa mavuno utafika! Lakini mimi nawaambieni, yatazameni mashamba; mazao yako tayari kuvunwa.
36And he that reapeth receiveth wages, and gathereth fruit unto life eternal: that both he that soweth and he that reapeth may rejoice together.
36Mvunaji anapata mshahara wake, na anakusanya mavuno kwa ajili ya uzima wa milele; hivyo mpandaji na mvunaji watafurahi pamoja.
37And herein is that saying true, One soweth, and another reapeth.
37Kwa sababu hiyo msemo huu ni kweli: Mmoja hupanda na mwingine huvuna.
38I sent you to reap that whereon ye bestowed no labour: other men laboured, and ye are entered into their labours.
38Mimi nimewatuma mkavune mavuno ambayo hamkuyatolea jasho, wengine walifanya kazi, lakini ninyi mnafaidika kutokana na jasho lao."
39And many of the Samaritans of that city believed on him for the saying of the woman, which testified, He told me all that ever I did.
39Wasamaria wengi wa kijiji kile waliamini kwa sababu ya maneno aliyosema huyo mama: "Ameniambia mambo yote niliyofanya."
40So when the Samaritans were come unto him, they besought him that he would tarry with them: and he abode there two days.
40Wasamaria walimwendea Yesu wakamwomba akae nao; naye akakaa hapo siku mbili.
41And many more believed because of his own word;
41Watu wengi zaidi walimwamini kwa sababu ya ujumbe wake.
42And said unto the woman, Now we believe, not because of thy saying: for we have heard him ourselves, and know that this is indeed the Christ, the Saviour of the world.
42Wakamwambia yule mama, "Sisi hatuamini tu kwa sababu ya maneno yako; sisi wenyewe tumesikia, na tunajua kwamba huyu ndiye kweli Mwokozi wa ulimwengu."
43Now after two days he departed thence, and went into Galilee.
43Baada ya siku mbili Yesu aliondoka hapo, akaenda Galilaya.
44For Jesus himself testified, that a prophet hath no honour in his own country.
44Maana Yesu mwenyewe alisema waziwazi kwamba, "Nabii hapati heshima katika nchi yake."
45Then when he was come into Galilee, the Galilaeans received him, having seen all the things that he did at Jerusalem at the feast: for they also went unto the feast.
45Basi, alipofika Galilaya, Wagalilaya wengi walimkaribisha. Maana nao pia walikuwa kwenye sikukuu ya Pasaka, wakayaona mambo yote Yesu aliyotenda huko Yerusalemu wakati wa sikukuu hiyo.
46So Jesus came again into Cana of Galilee, where he made the water wine. And there was a certain nobleman, whose son was sick at Capernaum.
46Yesu alifika tena huko mjini Kana, mkoani Galilaya, mahali alipogeuza maji kuwa divai. Kulikuwa na ofisa mmoja aliyekuwa na mtoto mgonjwa huko Kafarnaumu.
47When he heard that Jesus was come out of Judaea into Galilee, he went unto him, and besought him that he would come down, and heal his son: for he was at the point of death.
47Basi, huyo ofisa aliposikia kuwa Yesu alikuwa ametoka Yudea na kufika Galilaya, alimwendea akamwomba aende kumponya mtoto wake aliyekuwa mgonjwa mahututi.
48Then said Jesus unto him, Except ye see signs and wonders, ye will not believe.
48Yesu akamwambia, "Msipoona ishara na maajabu hamtaamini!"
49The nobleman saith unto him, Sir, come down ere my child die.
49Huyo ofisa akamwambia, "Mheshimiwa, tafadhali twende kabla mwanangu hajafa."
50Jesus saith unto him, Go thy way; thy son liveth. And the man believed the word that Jesus had spoken unto him, and he went his way.
50Yesu akamwambia, "Nenda tu, mwanao yu mzima." Huyo mtu akaamini maneno ya Yesu, akaenda zake.
51And as he was now going down, his servants met him, and told him, saying, Thy son liveth.
51Alipokuwa bado njiani, watumishi wake walikutana naye, wakamwambia kwamba mwanawe alikuwa mzima.
52Then enquired he of them the hour when he began to amend. And they said unto him, Yesterday at the seventh hour the fever left him.
52Naye akawauliza saa mtoto alipopata nafuu; nao wakamwambia, "Jana saa saba mchana, homa ilimwacha."
53So the father knew that it was at the same hour, in the which Jesus said unto him, Thy son liveth: and himself believed, and his whole house.
53Huyo baba akakumbuka kwamba ilikuwa ni saa ileile ambapo Yesu alimwambia: "Mwanao yu mzima." Basi, yeye akaamini pamoja na jamaa yake yote.
54This is again the second miracle that Jesus did, when he was come out of Judaea into Galilee.
54Hii ilikuwa ishara ya pili aliyoifanya Yesu alipokuwa anatoka Yudea kwenda Galilaya.