1Jesus went unto the mount of Olives.
1lakini Yesu akaenda kwenye mlima wa Mizeituni.
2And early in the morning he came again into the temple, and all the people came unto him; and he sat down, and taught them.
2Kesho yake asubuhi na mapema alikwenda tena Hekaluni. Watu wote wakamwendea, naye akaketi akawa anawafundisha.
3And the scribes and Pharisees brought unto him a woman taken in adultery; and when they had set her in the midst,
3Basi, walimu wa Sheria na Mafarisayo wakamletea mwanamke mmoja aliyefumaniwa katika uzinzi. Wakamsimamisha katikati yao.
4They say unto him, Master, this woman was taken in adultery, in the very act.
4Kisha wakamwuliza Yesu, "Mwalimu! Mwanamke huyu alifumaniwa katika uzinzi.
5Now Moses in the law commanded us, that such should be stoned: but what sayest thou?
5Katika Sheria yetu Mose alituamuru mwanamke kama huyu apigwe mawe. Basi, wewe wasemaje?"
6This they said, tempting him, that they might have to accuse him. But Jesus stooped down, and with his finger wrote on the ground, as though he heard them not.
6Walisema hivyo kumjaribu, wapate kisa cha kumshtaki. Lakini Yesu akainama chini, akaandika ardhini kwa kidole.
7So when they continued asking him, he lifted up himself, and said unto them, He that is without sin among you, let him first cast a stone at her.
7Walipozidi kumwuliza, Yesu akainuka, akawaambia, "Mtu asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza kumpiga jiwe."
8And again he stooped down, and wrote on the ground.
8Kisha akainama tena, akawa anaandika ardhini.
9And they which heard it, being convicted by their own conscience, went out one by one, beginning at the eldest, even unto the last: and Jesus was left alone, and the woman standing in the midst.
9Waliposikia hivyo, wakaanza kutoweka mmojammoja, wakitanguliwa na wazee. Yesu akabaki peke yake, na yule mwanamke amesimama palepale.
10When Jesus had lifted up himself, and saw none but the woman, he said unto her, Woman, where are those thine accusers? hath no man condemned thee?
10Yesu alipoinuka akamwuliza huyo mwanamke, "Wako wapi wale watu? Je, hakuna hata mmoja aliyekuhukumu?"
11She said, No man, Lord. And Jesus said unto her, Neither do I condemn thee: go, and sin no more.
11Huyo mwanamke akamjibu, "Mheshimiwa, hakuna hata mmoja!" Naye Yesu akamwambia, "Wala mimi sikuhukumu. Nenda zako; na tangu sasa usitende dhambi tena."
12Then spake Jesus again unto them, saying, I am the light of the world: he that followeth me shall not walk in darkness, but shall have the light of life.
12Yesu alipozungumza nao tena, aliwaambia, "Mimi ndimi mwanga wa ulimwengu. Anayenifuata mimi hatembei kamwe gizani, bali atakuwa na mwanga wa uzima."
13The Pharisees therefore said unto him, Thou bearest record of thyself; thy record is not true.
13Basi, Mafarisayo wakamwambia, "Wewe unajishuhudia mwenyewe; kwa hiyo ushahidi wako si halali."
14Jesus answered and said unto them, Though I bear record of myself, yet my record is true: for I know whence I came, and whither I go; but ye cannot tell whence I come, and whither I go.
14Yesu akawajibu, "Hata kama ninajishuhudia mwenyewe, ushahidi wangu ni wa kweli kwa sababu mimi najua nilikotoka na ninakokwenda. Lakini ninyi hamjui nilikotoka wala ninakokwenda.
15Ye judge after the flesh; I judge no man.
15Ninyi mnahukumu kwa fikira za kibinadamu, lakini mimi simhukumu mtu.
16And yet if I judge, my judgment is true: for I am not alone, but I and the Father that sent me.
16Hata nikihukumu, hukumu yangu ni ya haki kwa sababu mimi siko peke yangu; Baba aliyenituma yuko pamoja nami.
17It is also written in your law, that the testimony of two men is true.
17Imeandikwa katika Sheria yenu ya kwamba ushahidi wa watu wawili ni halali.
18I am one that bear witness of myself, and the Father that sent me beareth witness of me.
18Mimi najishuhudia mwenyewe, naye Baba aliyenituma, ananishuhudia pia."
19Then said they unto him, Where is thy Father? Jesus answered, Ye neither know me, nor my Father: if ye had known me, ye should have known my Father also.
19Hapo wakamwuliza, "Baba yako yuko wapi?" Yesu akawajibu "Ninyi hamnijui mimi wala hamumjui Baba. Kama mngenijua mimi, mngemjua na Baba yangu pia."
20These words spake Jesus in the treasury, as he taught in the temple: and no man laid hands on him; for his hour was not yet come.
20Yesu alisema maneno hayo kwenye chumba cha hazina alipokuwa anafundisha Hekaluni. Wala hakuna mtu aliyemtia nguvuni, kwa sababu saa yake ilikuwa haijafika bado.
21Then said Jesus again unto them, I go my way, and ye shall seek me, and shall die in your sins: whither I go, ye cannot come.
21Yesu akawaambia tena, "Naenda zangu nanyi mtanitafuta, lakini mtakufa katika dhambi zenu. Niendako mimi, ninyi hamwezi kufika."
22Then said the Jews, Will he kill himself? because he saith, Whither I go, ye cannot come.
22Basi, viongozi wa Wayahudi wakasema, "Je, atajiua? Mbona anasema: Niendako ninyi hamwezi kufika?"
23And he said unto them, Ye are from beneath; I am from above: ye are of this world; I am not of this world.
23Yesu akawaambia, "Ninyi mmetoka papa hapa chini, mimi nimetoka juu; ninyi ni wa ulimwengu huu, mimi si wa ulimwengu huu.
24I said therefore unto you, that ye shall die in your sins: for if ye believe not that I am he, ye shall die in your sins.
24Ndiyo maana niliwaambieni mtakufa katika dhambi zenu. Kama msipoamini kwamba Mimi ndimi, mtakufa katika dhambi zenu."
25Then said they unto him, Who art thou? And Jesus saith unto them, Even the same that I said unto you from the beginning.
25Nao wakamwuliza, "Wewe ni nani?" Yesu akawajibu, "Nimewaambieni tangu mwanzo!
26I have many things to say and to judge of you: but he that sent me is true; and I speak to the world those things which I have heard of him.
26Ninayo mengi ya kusema na kuhukumu juu yenu. Lakini yule aliyenituma ni kweli; nami nauambia ulimwengu mambo yale tu niliyoyasikia kutoka kwake."
27They understood not that he spake to them of the Father.
27Hawakuelewa kwamba Yesu alikuwa akisema nao juu ya Baba.
28Then said Jesus unto them, When ye have lifted up the Son of man, then shall ye know that I am he, and that I do nothing of myself; but as my Father hath taught me, I speak these things.
28Basi, Yesu akawaambia, "Mtakapokwisha mwinua Mwana wa Mtu hapo ndipo mtakapojua kwamba Mimi ndimi, na kwamba sifanyi chochote mimi mwenyewe, ila nasema tu yale Baba aliyonifundisha.
29And he that sent me is with me: the Father hath not left me alone; for I do always those things that please him.
29Yule aliyenituma yuko pamoja nami; yeye hakuniacha peke yangu kwani nafanya daima yale yanayompendeza."
30As he spake these words, many believed on him.
30Baada ya kusema hayo watu wengi walimwamini.
31Then said Jesus to those Jews which believed on him, If ye continue in my word, then are ye my disciples indeed;
31Basi, Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, "Kama mkiyazingatia mafundisho yangu mtakuwa kweli wanafunzi wangu.
32And ye shall know the truth, and the truth shall make you free.
32Mtaujua ukweli, nao ukweli utawapeni uhuru."
33They answered him, We be Abraham's seed, and were never in bondage to any man: how sayest thou, Ye shall be made free?
33Nao wakamjibu, "Sisi ni wazawa wa Abrahamu, na hatujapata kamwe kuwa watumwa wa mtu yeyote yule. Una maana gani unaposema: mtakuwa huru?"
34Jesus answered them, Verily, verily, I say unto you, Whosoever committeth sin is the servant of sin.
34Yesu akawajibu, "Kweli nawaambieni, kila mtu anayetenda dhambi ni mtumwa wa dhambi.
35And the servant abideth not in the house for ever: but the Son abideth ever.
35Mtumwa hana makao ya kudumu nyumbani, lakini mwana anayo makao ya kudumu.
36If the Son therefore shall make you free, ye shall be free indeed.
36Kama mwana akiwapeni uhuru mtakuwa huru kweli.
37I know that ye are Abraham's seed; but ye seek to kill me, because my word hath no place in you.
37Najua kwamba ninyi ni wazawa wa Abrahamu. Hata hivyo, mnataka kuniua kwa sababu hamuyakubali mafundisho yangu.
38I speak that which I have seen with my Father: and ye do that which ye have seen with your father.
38Mimi nasema yale aliyonionyesha Baba, lakini ninyi mwafanya yale aliyowaambieni baba yenu."
39They answered and said unto him, Abraham is our father. Jesus saith unto them, If ye were Abraham's children, ye would do the works of Abraham.
39Wao wakamjibu, "Baba yetu ni Abrahamu!" Yesu akawaambia, "Kama ninyi mngekuwa watoto wa Abrahamu, mngefanya kama alivyofanya Abrahamu,
40But now ye seek to kill me, a man that hath told you the truth, which I have heard of God: this did not Abraham.
40Mimi nimewaambieni ukweli niliousikia kwa Mungu; hata hivyo, ninyi mwataka kuniua. Abrahamu hakufanya hivyo!
41Ye do the deeds of your father. Then said they to him, We be not born of fornication; we have one Father, even God.
41Ninyi mnafanya mambo yaleyale aliyofanya babu yenu." Wao wakamwambia, "Sisi si watoto haramu! Tunaye baba mmoja tu, yaani Mungu."
42Jesus said unto them, If God were your Father, ye would love me: for I proceeded forth and came from God; neither came I of myself, but he sent me.
42Yesu akawaambia, "Kama Mungu angekuwa Baba yenu, mngenipenda mimi, maana mimi nilitoka kwa Mungu na sasa niko hapa. Sikuja kwa mamlaka yangu mwenyewe, ila yeye alinituma.
43Why do ye not understand my speech? even because ye cannot hear my word.
43Kwa nini hamwelewi hayo ninayosema? Ni kwa kuwa hamwezi kuusikiliza ujumbe wangu.
44Ye are of your father the devil, and the lusts of your father ye will do. He was a murderer from the beginning, and abode not in the truth, because there is no truth in him. When he speaketh a lie, he speaketh of his own: for he is a liar, and the father of it.
44Ninyi ni watoto wa baba yenu Ibilisi na mnataka tu kutekeleza tamaa za baba yenu. Yeye alikuwa muuaji tangu mwanzo; hana msimamo katika ukweli, kwani ukweli haumo ndani yake. Kila asemapo uongo, husema kutokana na hali yake ya maumbile, maana yeye ni mwongo na baba wa uongo.
45And because I tell you the truth, ye believe me not.
45Mimi nasema ukweli, na ndiyo maana ninyi hamniamini.
46Which of you convinceth me of sin? And if I say the truth, why do ye not believe me?
46Nani kati yenu awezaye kuthibitisha kuwa mimi nina dhambi? Ikiwa basi nasema ukweli, kwa nini hamniamini?
47He that is of God heareth God's words: ye therefore hear them not, because ye are not of God.
47Aliye wa Mungu husikiliza maneno ya Mungu. Lakini ninyi hamsikilizi kwa sababu ninyi si (watu wa) Mungu."
48Then answered the Jews, and said unto him, Say we not well that thou art a Samaritan, and hast a devil?
48Wayahudi wakamwambia, "Je, hatukusema kweli kwamba wewe ni Msamaria, na tena una pepo?"
49Jesus answered, I have not a devil; but I honour my Father, and ye do dishonour me.
49Yesu akajibu, "Mimi sina pepo; mimi namheshimu Baba yangu, lakini ninyi hamniheshimu.
50And I seek not mine own glory: there is one that seeketh and judgeth.
50Mimi sijitafutii utukufu wangu mwenyewe; yuko mmoja mwenye kuutafuta utukufu huo, naye ni hakimu.
51Verily, verily, I say unto you, If a man keep my saying, he shall never see death.
51Kweli nawaambieni, anayeuzingatia ujumbe wangu hatakufa milele."
52Then said the Jews unto him, Now we know that thou hast a devil. Abraham is dead, and the prophets; and thou sayest, If a man keep my saying, he shall never taste of death.
52Basi, Wayahudi wakasema, "Sasa tunajua kweli kwamba wewe ni mwendawazimu! Abrahamu alikufa, na manabii pia walikufa, nawe wasema ati, Anayeuzingatia ujumbe wangu hatakufa milele!
53Art thou greater than our father Abraham, which is dead? and the prophets are dead: whom makest thou thyself?
53Je, unajifanya mkuu zaidi kuliko baba yetu Abrahamu ambaye alikufa? Hata na manabii walikufa. Wewe unajifanya kuwa nani?"
54Jesus answered, If I honour myself, my honour is nothing: it is my Father that honoureth me; of whom ye say, that he is your God:
54Yesu akawajibu, "Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu. Baba yangu ambaye ninyi mwasema ni Baba yenu, ndiye anayenitukuza.
55Yet ye have not known him; but I know him: and if I should say, I know him not, I shall be a liar like unto you: but I know him, and keep his saying.
55Ninyi hamjapata kumjua, lakini mimi namjua. Na, nikisema simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi. Mimi namjua na ninashika neno lake.
56Your father Abraham rejoiced to see my day: and he saw it, and was glad.
56Abrahamu, baba yenu, alishangilia aione siku yangu; naye aliiona, akafurahi."
57Then said the Jews unto him, Thou art not yet fifty years old, and hast thou seen Abraham?
57Basi, Wayahudi wakamwambia, "Wewe hujatimiza miaka hamsini bado, nawe umemwona Abrahamu?"
58Jesus said unto them, Verily, verily, I say unto you, Before Abraham was, I am.
58Yesu akawaambia, "Kweli nawaambieni, kabla Abrahamu hajazaliwa, mimi niko."
59Then took they up stones to cast at him: but Jesus hid himself, and went out of the temple, going through the midst of them, and so passed by.
59Hapo wakaokota mawe ili wamtupie, lakini Yesu akajificha, akatoka Hekaluni.