1And he spake a parable unto them to this end, that men ought always to pray, and not to faint;
1Basi, Yesu aliwasimulia mfano kuonyesha kwamba ni lazima kusali daima bila kukata tamaa.
2Saying, There was in a city a judge, which feared not God, neither regarded man:
2Alisema: "Katika mji mmoja kulikuwa na hakimu ambaye hakuwa anamcha Mungu wala kumjali binadamu.
3And there was a widow in that city; and she came unto him, saying, Avenge me of mine adversary.
3Katika mji huohuo, kulikuwa pia na mama mmoja mjane, ambaye alimwendea huyo hakimu mara nyingi akimwomba amtetee apate haki yake kutoka kwa adui yake.
4And he would not for a while: but afterward he said within himself, Though I fear not God, nor regard man;
4Kwa muda mrefu huyo hakimu hakupenda kumtetea huyo mjane; lakini, mwishowe akajisemea: Ingawa mimi simchi Mungu wala simjali binadamu,
5Yet because this widow troubleth me, I will avenge her, lest by her continual coming she weary me.
5lakini kwa vile huyu mjane ananisumbua, nitamtetea; la sivyo ataendelea kufika hapa, na mwisho atanichosha kabisa!"
6And the Lord said, Hear what the unjust judge saith.
6Basi, Bwana akaendelea kusema, "Sikieni jinsi alivyosema huyo hakimu mbaya.
7And shall not God avenge his own elect, which cry day and night unto him, though he bear long with them?
7Je, ndio kusema Mungu hatawatetea wale aliowachagua, ambao wanamlilia mchana na usiku? Je, atakawia kuwasikiliza?
8I tell you that he will avenge them speedily. Nevertheless when the Son of man cometh, shall he find faith on the earth?
8Nawaambieni atawatetea upesi. Hata hivyo, je, kutakuwako na imani duniani wakati Mwana wa Mtu atakapokuja?"
9And he spake this parable unto certain which trusted in themselves that they were righteous, and despised others:
9Halafu Yesu aliwaambia pia mfano wa wale ambao walijiona kuwa wema na kuwadharau wengine.
10Two men went up into the temple to pray; the one a Pharisee, and the other a publican.
10"Watu wawili walipanda kwenda Hekaluni kusali: mmoja Mfarisayo, na mwingine mtoza ushuru.
11The Pharisee stood and prayed thus with himself, God, I thank thee, that I am not as other men are, extortioners, unjust, adulterers, or even as this publican.
11Huyo Mfarisayo akasimama, akasali kimoyomoyo: Ee Mungu, nakushukuru kwa vile mimi si kama watu wengine: walafi, wadanganyifu au wazinzi. Nakushukuru kwamba mimi si kama huyu mtoza ushuru.
12I fast twice in the week, I give tithes of all that I possess.
12Nafunga mara mbili kwa juma, natoa zaka sehemu ya kumi ya pato langu.
13And the publican, standing afar off, would not lift up so much as his eyes unto heaven, but smote upon his breast, saying, God be merciful to me a sinner.
13Lakini yule mtoza ushuru, akiwa amesimama kwa mbali bila hata kuinua macho yake mbinguni, ila tu akijipiga kifua kwa huzuni, alisema: Ee Mungu, unionee huruma mimi mwenye dhambi.
14I tell you, this man went down to his house justified rather than the other: for every one that exalteth himself shall be abased; and he that humbleth himself shall be exalted.
14Nawaambieni, huyu mtoza ushuru alirudi nyumbani akiwa amesamehewa. Lakini yule mwingine, sivyo. Kwa maana kila anayejikweza atashushwa, na kila anayejishusha atakwezwa."
15And they brought unto him also infants, that he would touch them: but when his disciples saw it, they rebuked them.
15Watu walimletea Yesu watoto wadogo ili awawekee mikono yake. Wanafunzi walipowaona, wakawazuia kwa maneno makali.
16But Jesus called them unto him, and said, Suffer little children to come unto me, and forbid them not: for of such is the kingdom of God.
16Lakini Yesu akawaita kwake akisema: "Waacheni hao watoto waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni kwa ajili ya watu kama hawa.
17Verily I say unto you, Whosoever shall not receive the kingdom of God as a little child shall in no wise enter therein.
17Nawaambieni kweli, mtu yeyote asiyeupokea Ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hataingia katika Ufalme huo."
18And a certain ruler asked him, saying, Good Master, what shall I do to inherit eternal life?
18Kiongozi mmoja, Myahudi, alimwuliza Yesu, "Mwalimu mwema, nifanye nini ili niweze kuupata uzima wa milele?"
19And Jesus said unto him, Why callest thou me good? none is good, save one, that is, God.
19Yesu akamwambia, "Mbona waniita mwema? Hakuna aliye mwema ila Mungu peke yake.
20Thou knowest the commandments, Do not commit adultery, Do not kill, Do not steal, Do not bear false witness, Honour thy father and thy mother.
20Unazijua amri: Usizini; usiue; usiibe; usitoe ushahidi wa uongo; waheshimu baba yako na mama yako."
21And he said, All these have I kept from my youth up.
21Yeye akasema, "Hayo yote nimeyazingatia tangu ujana wangu."
22Now when Jesus heard these things, he said unto him, Yet lackest thou one thing: sell all that thou hast, and distribute unto the poor, and thou shalt have treasure in heaven: and come, follow me.
22Yesu aliposikia hayo akamwambia, "Unatakiwa bado kufanya kitu kimoja: uza kila ulicho nacho, wagawie maskini, na hivyo utakuwa na hazina yako mbinguni; halafu njoo unifuate."
23And when he heard this, he was very sorrowful: for he was very rich.
23Lakini huyo mtu aliposikia hayo, alihuzunika sana kwa sababu alikuwa tajiri sana.
24And when Jesus saw that he was very sorrowful, he said, How hardly shall they that have riches enter into the kingdom of God!
24Yesu alipoona akihuzunika hivyo, akasema, "Jinsi gani ilivyo vigumu kwa matajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu!
25For it is easier for a camel to go through a needle's eye, than for a rich man to enter into the kingdom of God.
25Naam, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu."
26And they that heard it said, Who then can be saved?
26Wale watu waliposikia hayo, wakasema, "Nani basi, atakayeokolewa?"
27And he said, The things which are impossible with men are possible with God.
27Yesu akajibu, "Yasiyowezekana kwa binadamu, yanawezekana kwa Mungu."
28Then Peter said, Lo, we have left all, and followed thee.
28Naye Petro akamwuliza, "Na sisi je? Tumeacha vitu vyote tukakufuata!"
29And he said unto them, Verily I say unto you, There is no man that hath left house, or parents, or brethren, or wife, or children, for the kingdom of God's sake,
29Yesu akawaambia, "Kweli nawaambieni, mtu yeyote aliyeacha nyumba au mke au kaka au wazazi au watoto kwa ajili ya Ufalme wa Mungu,
30Who shall not receive manifold more in this present time, and in the world to come life everlasting.
30atapokea mengi zaidi wakati huu wa sasa, na kupokea uzima wa milele wakati ujao."
31Then he took unto him the twelve, and said unto them, Behold, we go up to Jerusalem, and all things that are written by the prophets concerning the Son of man shall be accomplished.
31Yesu aliwachukua kando wale kumi na wawili, akawaambia, "Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu na huko kila kitu kilichoandikwa na manabii kuhusu Mwana wa Mtu kitakamilishwa.
32For he shall be delivered unto the Gentiles, and shall be mocked, and spitefully entreated, and spitted on:
32Kwa maana atakabidhiwa kwa watu wa mataifa nao watamtendea vibaya na kumtemea mate.
33And they shall scourge him, and put him to death: and the third day he shall rise again.
33Watampiga mijeledi, watamuua; lakini siku ya tatu atafufuka."
34And they understood none of these things: and this saying was hid from them, neither knew they the things which were spoken.
34Lakini wao hawakuelewa hata kidogo jambo hilo; walikuwa wamefichwa maana ya maneno hayo, na hawakutambua yaliyosemwa.
35And it came to pass, that as he was come nigh unto Jericho, a certain blind man sat by the way side begging:
35Wakati Yesu alipokaribia Yeriko, kulikuwa na mtu mmoja kipofu ameketi njiani akiomba.
36And hearing the multitude pass by, he asked what it meant.
36Aliposikia umati wa watu ukipita aliuliza, "Kuna nini?"
37And they told him, that Jesus of Nazareth passeth by.
37Wakamwambia, "Yesu wa Nazareti anapita."
38And he cried, saying, Jesus, thou son of David, have mercy on me.
38Naye akapaza sauti akisema, "Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!"
39And they which went before rebuked him, that he should hold his peace: but he cried so much the more, Thou son of David, have mercy on me.
39Wale watu waliotangulia wakamkemea wakimwambia anyamaze; lakini yeye akazidi kupaza sauti: "Mwana wa Daudi, nihurumie;"
40And Jesus stood, and commanded him to be brought unto him: and when he was come near, he asked him,
40Yesu alisimama, akaamuru wamlete mbele yake. Yule kipofu alipofika karibu, Yesu akamwuliza,
41Saying, What wilt thou that I shall do unto thee? And he said, Lord, that I may receive my sight.
41"Unataka nikufanyie nini?" Naye akamjibu, "Bwana, naomba nipate kuona tena."
42And Jesus said unto him, Receive thy sight: thy faith hath saved thee.
42Yesu akamwambia, "Ona! Imani yako imekuponya."
43And immediately he received his sight, and followed him, glorifying God: and all the people, when they saw it, gave praise unto God.
43Na mara yule aliyekuwa kipofu akapata kuona, akamfuata Yesu akimtukuza Mungu. Watu wote walipoona hayo, wakamsifu Mungu.