1الحق الحق اقول لكم ان الذي لا يدخل من الباب الى حظيرة الخراف بل يطلع من موضع آخر فذاك سارق ولص.
1Yesu alisema "Kweli nawaambieni, yeyote yule asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia mlangoni, bali hupenya na kuingia kwa njia nyingine, huyo ni mwizi na mnyang'anyi.
2واما الذي يدخل من الباب فهو راعي الخراف.
2Lakini anayeingia kwa kupitia mlangoni, huyo ndiye mchungaji wa kondoo.
3لهذا يفتح البواب والخراف تسمع صوته فيدعو خرافه الخاصة باسماء ويخرجها.
3Mngoja mlango wa zizi humfungulia, na kondoo husikia sauti yake, naye huwaita kondoo wake kila mmoja kwa jina lake na kuwaongoza nje.
4ومتى اخرج خرافه الخاصة يذهب امامها والخراف تتبعه لانها تعرف صوته.
4Akisha watoa nje huwatangulia mbele nao kondoo humfuata, kwani wanaijua sauti yake.
5واما الغريب فلا تتبعه بل تهرب منه لانها لا تعرف صوت الغرباء.
5Kondoo hao hawawezi kumfuata mgeni, bali watamkimbia kwa sababu hawaijui sauti yake."
6هذا المثل قاله لهم يسوع. واما هم فلم يفهموا ما هو الذي كان يكلمهم به
6Yesu aliwaambia mfano huo, lakini wao hawakuelewa alichotaka kuwaambia.
7فقال لهم يسوع ايضا الحق الحق اقول لكم اني انا باب الخراف.
7Basi, akasema tena, "Kweli nawaambieni, mimi ni mlango wa kondoo.
8جميع الذين أتوا قبلي هم سراق ولصوص. ولكن الخراف لم تسمع لهم.
8Wale wengine wote waliokuja kabla yangu ni wezi na wanyang'anyi, nao kondoo hawakuwasikiliza.
9انا هو الباب. ان دخل بي احد فيخلص ويدخل ويخرج ويجد مرعى.
9Mimi ni mlango. Anayeingia kwa kupitia kwangu ataokolewa; ataingia na kutoka, na kupata malisho.
10السارق لا يأتي الا ليسرق ويذبح ويهلك. واما انا فقد أتيت لتكون لهم حياة وليكون لهم افضل.
10Mwizi huja kwa shabaha ya kuiba, kuua na kuharibu. Mimi nimekuja mpate kuwa na uzima--uzima kamili.
11انا هو الراعي الصالح. والراعي الصالح يبذل نفسه عن الخراف.
11"Mimi ni mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo wake.
12واما الذي هو اجير وليس راعيا الذي ليست الخراف له فيرى الذئب مقبلا ويترك الخراف ويهرب. فيخطف الذئب الخراف ويبددها.
12Mtu wa kuajiriwa ambaye si mchungaji, na wala kondoo si mali yake, anapoona mbwa mwitu anakuja, huwaacha kondoo na kukimbia. Kisha mbwa mwitu huwakamata na kuwatawanya.
13والاجير يهرب لانه اجير ولا يبالي بالخراف.
13Yeye hajali kitu juu ya kondoo kwa sababu yeye ni mtu wa mshahara tu.
14اما انا فاني الراعي الصالح واعرف خاصتي وخاصتي تعرفني
14Mimi ni mchungaji mwema. Nawajua walio wangu, nao walio wangu wananijua mimi,
15كما ان الآب يعرفني وانا اعرف الآب. وانا اضع نفسي عن الخراف.
15kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Mimi nayatoa maisha yangu kwa ajili yao.
16ولي خراف أخر ليست من هذه الحظيرة ينبغي ان آتي بتلك ايضا فتسمع صوتي وتكون رعية واحدة وراع واحد.
16Tena ninao kondoo wengine ambao hawamo zizini humu. Inanibidi kuwaleta hao pia, nao wataisikia sauti yangu, na kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.
17لهذا يحبني الآب لاني اضع نفسي لآخذها ايضا.
17"Baba ananipenda kwani nautoa uhai wangu ili nipate kuupokea tena.
18ليس احد يأخذها مني بل اضعها انا من ذاتي. لي سلطان ان اضعها ولي سلطان ان آخذها ايضا. هذه الوصية قبلتها من ابي.
18Hakuna mtu anayeninyang'anya uhai wangu; mimi na nautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa na uwezo wa kuuchukua tena. Hivi ndivyo Baba alivyoniamuru nifanye."
19فحدث ايضا انشقاق بين اليهود بسبب هذا الكلام.
19Kukawa tena na mafarakano kati ya Wayahudi kwa sababu ya maneno haya.
20فقال كثيرون منهم به شيطان وهو يهذي. لماذا تستمعون له.
20Wengi wao wakasema, "Ana pepo; tena ni mwendawazimu! Ya nini kumsikiliza?"
21آخرون قالوا ليس هذا كلام من به شيطان. ألعل شيطانا يقدر ان يفتح اعين العميان
21Wengine wakasema, "Haya si maneno ya mwenye pepo. Je, pepo anaweza kuyafumbua macho ya vipofu?"
22وكان عيد التجديد في اورشليم وكان شتاء.
22Huko Yerusalemu kulikuwa na sikukuu ya Kutabaruku. Wakati huo ulikuwa wa baridi.
23وكان يسوع يتمشى في الهيكل في رواق سليمان.
23Naye Yesu akawa anatembea Hekaluni katika ukumbi wa Solomoni.
24فاحتاط به اليهود وقالوا له الى متى تعلّق انفسنا. ان كنت انت المسيح فقل لنا جهرا.
24Basi, Wayahudi wakamzunguka, wakamwuliza, "Utatuacha katika mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiye Kristo, basi, tuambie wazi."
25اجابهم يسوع اني قلت لكم ولستم تؤمنون. الاعمال التي انا اعملها باسم ابي هي تشهد لي.
25Yesu akawajibu, "Nimewaambieni, lakini hamsadiki. Kazi ninazozifanya mimi kwa jina la Baba yangu zinanishuhudia.
26ولكنكم لستم تؤمنون لانكم لستم من خرافي كما قلت لكم.
26Lakini ninyi hamsadiki kwa sababu ninyi si kondoo wangu.
27خرافي تسمع صوتي وانا اعرفها فتتبعني.
27Kondoo wangu huisikia sauti yangu; mimi nawajua, nao hunifuata.
28وانا اعطيها حياة ابدية ولن تهلك الى الابد ولا يخطفها احد من يدي.
28Mimi nawapa uzima wa milele; nao hawatapotea milele, wala hakuna mtu atakayeweza kuwatoa mkononi mwangu.
29ابي الذي اعطاني اياها هو اعظم من الكل ولا يقدر احد ان يخطف من يد ابي.
29Baba yangu ambaye ndiye aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote, wale hakuna awezaye kuwatoa mikononi mwake Baba.
30انا والآب واحد
30Mimi na Baba, tu mmoja."
31فتناول اليهود ايضا حجارة ليرجموه.
31Basi, Wayahudi wakachukua mawe ili wamtupie.
32اجابهم يسوع اعمالا كثيرة حسنة أريتكم من عند ابي. بسبب اي عمل منها ترجمونني.
32Yesu akawaambia, "Nimewaonyesheni kazi nyingi kutoka kwa Baba. Ni ipi kati ya hizo inayowafanya mnipige mawe?"
33اجابه اليهود قائلين لسنا نرجمك لاجل عمل حسن بل لاجل تجديف. فانك وانت انسان تجعل نفسك الها.
33Wayahudi wakamjibu, "Hatukupigi mawe kwa ajili ya tendo jema, ila kwa sababu ya kukufuru! Maana wajifanya kuwa Mungu hali wewe ni binadamu tu."
34اجابهم يسوع أليس مكتوبا في ناموسكم انا قلت انكم آلهة.
34Yesu akawajibu, "Je, haikuandikwa katika Sheria yenu: Mimi nimesema, ninyi ni miungu?
35ان قال آلهة لاولئك الذين صارت اليهم كلمة الله. ولا يمكن ان ينقض المكتوب.
35Mungu aliwaita miungu wale waliopewa neno lake; nasi twajua kwamba Maandiko Matakatifu yasema ukweli daima.
36فالذي قدسه الآب وارسله الى العالم أتقولون له انك تجدف لاني قلت اني ابن الله.
36Je, yeye ambaye Baba alimweka wakfu na kumtuma ulimwenguni, mnamwambia: Unakufuru, eti kwa sababu nilisema: Mimi ni Mwana wa Mungu?
37ان كنت لست اعمل اعمال ابي فلا تؤمنوا بي.
37Kama sifanyi kazi za Baba yangu msiniamini.
38ولكن ان كنت اعمل فان لم تؤمنوا بي فآمنوا بالاعمال لكي تعرفوا وتؤمنوا ان الآب فيّ وانا فيه
38Lakini ikiwa ninazifanya, hata kama hamniamini, walau ziaminini hizo kazi mpate kujua na kutambua kwamba Baba yuko ndani yangu, nami niko ndani yake."
39فطلبوا ايضا ان يمسكوه فخرج من ايديهم.
39Wakajaribu tena kumkamata lakini akachopoka mikononi mwao.
40ومضى ايضا الى عبر الاردن الى المكان الذي كان يوحنا يعمد فيه اولا ومكث هناك.
40Yesu akaenda tena ng'ambo ya mto Yordani, mahali Yohane alipokuwa akibatiza, akakaa huko.
41فأتى اليه كثيرون وقالوا ان يوحنا لم يفعل آية واحدة. ولكن كل ما قاله يوحنا عن هذا كان حقا.
41Watu wengi walimwendea wakasema, "Yohane hakufanya ishara yoyote. Lakini yale yote Yohane aliyosema juu ya mtu huyu ni kweli kabisa."
42فآمن كثيرون به هناك
42Watu wengi mahali hapo wakamwamini.