الكتاب المقدس (Van Dyke)

Swahili: New Testament

Mark

15

1وللوقت في الصباح تشاور رؤساء الكهنة والشيوخ والكتبة والمجمع كله فأوثقوا يسوع ومضوا به واسلموه الى بيلاطس
1Kulipopambazuka, makuhani wakuu walifanya shauri pamoja na wazee, walimu wa Sheria na Baraza lote, wakamfunga Yesu pingu, wakampeleka na kumkabidhi kwa Pilato.
2فسأله بيلاطس انت ملك اليهود. فاجاب وقال له انت تقول.
2Pilato akamwuliza Yesu, "Je, wewe ni mfalme wa Wayahudi?" Yesu akajibu, "Wewe umesema."
3وكان رؤساء الكهنة يشتكون عليه كثيرا.
3Makuhani wakuu wakamshtaki Yesu mambo mengi.
4فسأله بيلاطس ايضا قائلا أما تجيب بشيء. انظر كم يشهدون عليك.
4Pilato akamwuliza tena Yesu, "Je, hujibu neno? Tazama wanavyotoa mashtaka mengi juu yako."
5فلم يجب يسوع ايضا بشيء حتى تعجب بيلاطس.
5Lakini Yesu hakujibu neno, hata pilato akashangaa.
6وكان يطلق لهم في كل عيد اسيرا واحدا من طلبوه.
6Kila wakati wa sikukuu ya Pasaka, Pilato alikuwa na desturi ya kuwafungulia mfungwa mmoja waliyemtaka.
7وكان المسمى باراباس موثقا مع رفقائه في الفتنة الذين في الفتنة فعلوا قتلا.
7Basi, kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Baraba, ambaye alikuwa amefungwa pamoja na waasi wengine kwa kusababisha uasi na mauaji.
8فصرخ الجمع وابتدأوا يطلبون ان يفعل كما كان دائما يفعل لهم.
8Watu wengi wakamwendea Pilato wakamwomba awafanyie kama kawaida yake.
9فاجابهم بيلاطس قائلا أتريدون ان اطلق لكم ملك اليهود.
9Pilato akawauliza, "Je, mwataka niwafungulieni Mfalme wa Wayahudi?"
10لانه عرف ان رؤساء الكهنة كانوا قد اسلموه حسدا.
10Alisema hivyo kwa sababu alijua wazi kwamba makuhani wakuu walimkabidhi Yesu kwake kwa sababu ya wivu.
11فهيج رؤساء الكهنة الجمع لكي يطلق لهم بالحري باراباس.
11Lakini makuhani wakuu wakawachochea watu wamwombe Pilato awafungulie Baraba.
12فاجاب بيلاطس ايضا وقال لهم فماذا تريدون ان افعل بالذي تدعونه ملك اليهود.
12Pilato akawauliza tena, "Basi, sasa mwataka nifanye nini na mtu huyu mnayemwita Mfalme wa Wayahudi?"
13فصرخوا ايضا اصلبه.
13Watu wote wakapaaza sauti tena: "Msulubishe!"
14فقال لهم بيلاطس واي شر عمل. فازدادوا جدا صراخا اصلبه.
14Lakini Pilato akawauliza, "Kwa nini! Amefanya kosa gani?" Lakini wao wakazidi kupaaza sauti, "Msulubishe!"
15فبيلاطس اذ كان يريد ان يعمل للجمع ما يرضيهم اطلق لهم باراباس واسلم يسوع بعدما جلده ليصلب
15Pilato alitaka kuuridhisha huo umati wa watu; basi, akamwachilia Baraba kutoka gerezani. Akaamuru Yesu apigwe viboko, kisha akamtoa asulubiwe.
16فمضى به العسكر الى داخل الدار التي هي دار الولاية وجمعوا كل الكتيبة.
16Kisha askari walimpeleka Yesu ndani ukumbini, katika ikulu, wakakusanya kikosi kizima cha askari.
17وألبسوه ارجوانا وضفروا اكليلا من شوك ووضعوه عليه.
17Wakamvika vazi la rangi ya zambarau, wakasokota taji ya miiba, wakamwekea kichwani.
18وابتدأوا يسلمون عليه قائلين السلام يا ملك اليهود.
18Wakaanza kumsalimu, "Shikamoo Mfalme wa Wayahudi!"
19وكانوا يضربونه على راسه بقصبة ويبصقون عليه ثم يسجدون له جاثين على ركبهم.
19Wakampiga kichwani kwa mwanzi, wakamtemea mate; wakampigia magoti na kumsujudia.
20وبعدما استهزأوا به نزعوا عنه الارجوان والبسوه ثيابه ثم خرجوا به ليصلبوه.
20Baada ya kumdhihaki, walimvua lile joho, wakamvika nguo zake, kisha wakampeleka kumsulubisha.
21فسخّروا رجلا مجتازا كان آتيا من الحقل وهو سمعان القيرواني ابو ألكسندرس وروفس ليحمل صليبه.
21Walipokuwa njiani, walikutana na mtu mmoja aitwaye Simoni, mwenyeji wa Kurene. Yeye alikuwa baba wa Aleksanda na Rufo, na wakati huo alikuwa akitoka shambani. Basi, wakamlazimisha auchukue msalaba wa Yesu.
22وجاءوا به الى موضع جلجثة الذي تفسيره موضع جمجمة.
22Kisha wakampeleka Yesu mpaka mahali palipoitwa Golgotha, maana yake, "Mahali pa Fuvu la Kichwa."
23واعطوه خمرا ممزوجة بمرّ ليشرب فلم يقبل.
23Wakampa divai iliyochanganywa na manemane, lakini yeye akaikataa.
24ولما صلبوه اقتسموا ثيابه مقترعين عليها ماذا يأخذ كل واحد.
24Basi, wakamsulubisha, wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura waamue nani angepata nini.
25وكانت الساعة الثالثة فصلبوه.
25Ilikuwa saa tatu asubuhi walipomsulubisha.
26وكان عنوان علّته مكتوبا ملك اليهود.
26Na mshtaka wake ulikuwa umeandikwa: "Mfalme wa Wayahudi."
27وصلبوا معه لصين واحدا عن يمينه وآخر عن يساره.
27Pamoja naye waliwasulubisha wanyang'anyi wawili, mmoja upande wake wa kulia na mwingine upande wake wa kushoto.
28فتم الكتاب القائل واحصي مع اثمة.
28Hapo yakatimia Maandiko Matakatifu yanayosema, "Aliwekwa kundi moja na waovu."
29وكان المجتازون يجدفون عليه وهم يهزون رؤوسهم قائلين آه يا ناقض الهيكل وبانيه في ثلاثة ايام.
29Watu waliokuwa wanapita mahali hapo walimtukana, wakitikisa vichwa vyao na kusema, "Aha! Wewe mwenye kuvunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu!
30خلّص نفسك وانزل عن الصليب.
30Sasa, shuka msalabani ujiokoe mwenyewe!"
31وكذلك رؤساء الكهنة وهم مستهزئون فيما بينهم مع الكتبة قالوا خلّص آخرين واما نفسه فما يقدر ان يخلّصها.
31Nao makuhani wakuu pamoja na walimu wa Sheria walimdhihaki wakisema, "Aliwaokoa wengine, lakini kujiokoa mwenyewe hawezi!
32لينزل الآن المسيح ملك اسرائيل عن الصليب لنرى ونؤمن. واللذان صلبا معه كانا يعيّرانه
32Eti yeye ni Kristo, Mfalme wa Israeli! Basi, na ashuke msalabani ili tuone na kuamini." Hata watu wale waliosulubiwa pamoja naye walimtukana.
33ولما كانت الساعة السادسة كانت ظلمة على الارض كلها الى الساعة التاسعة.
33Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa kulikuwa giza nchini kote.
34وفي الساعة التاسعة صرخ يسوع بصوت عظيم قائلا ألوي ألوي لما شبقتني. الذي تفسيره الهي الهي لماذا تركتني.
34Saa tisa alasiri Yesu akalia kwa sauti kubwa, "Eloi, Eloi, lema sabakthani?" Maana yake, "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?"
35فقال قوم من الحاضرين لما سمعوا هوذا ينادي ايليا.
35Baadhi ya watu waliosimama pale waliposikia hivyo, walisema, "Sikiliza! Anamwita Eliya!"
36فركض واحد وملأ اسفنجة خلا وجعلها على قصبة وسقاه قائلا اتركوا. لنر هل يأتي ايليا لينزله
36Mtu mmoja akakimbia, akachovya sifongo katika siki, akaiweka juu ya mwanzi, akampa anywe akisema, "Hebu tuone kama Eliya atakuja kumteremsha msalabani!"
37فصرخ يسوع بصوت عظيم واسلم الروح.
37Yesu akapaaza sauti kubwa, akakata roho.
38وانشق حجاب الهيكل الى اثنين من فوق الى اسفل.
38Basi, pazia la Hekalu likapasuka vipande viwili toka juu mpaka chini.
39ولما رأى قائد المئة الواقف مقابله انه صرخ هكذا واسلم الروح قال حقا كان هذا الانسان ابن الله.
39Jemadari mmoja aliyekuwa amesimama mbele yake aliona jinsi Yesu alivyolia kwa sauti na kukata roho, akasema, "Kweli mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu!"
40وكانت ايضا نساء ينظرن من بعيد بينهنّ مريم المجدلية ومريم ام يعقوب الصغير ويوسي وسالومة.
40Walikuwako pia wanawake waliotazama kwa mbali, miongoni mwao akiwa Maria toka mji wa Magdala, Salome, na Maria mama wa kina Yakobo mdogo na Yose.
41اللواتي ايضا تبعنه وخدمنه حين كان في الجليل. وأخر كثيرات اللواتي صعدن معه الى اورشليم
41Hawa walimfuata Yesu alipokuwa Galilaya na kumtumikia. Kulikuwa na wanawake wengine wengi waliokuja Yerusalemu pamoja naye.
42ولما كان المساء اذ كان الاستعداد. اي ما قبل السبت.
42Wakati wa jioni ulikuwa umekwisha fika. Hiyo ilikuwa siku ya Maandalio, yaani siku inayotangulia Sabato.
43جاء يوسف الذي من الرامة مشير شريف وكان هو ايضا منتظرا ملكوت الله فتجاسر ودخل الى بيلاطس وطلب جسد يسوع.
43Hapo akaja Yosefu mwenyeji wa Armathaya, mjumbe wa Baraza Kuu, aliyeheshimika sana. Yeye pia alikuwa anatazamia kuja kwa Ufalme wa Mungu. Basi, alimwendea Pilato bila uoga, akaomba apewe mwili wa Yesu.
44فتعجب بيلاطس انه مات كذا سريعا فدعا قائد المئة وسأله هل له زمان قد مات.
44Pilato alishangaa kusikia kwamba Yesu alikuwa amekwisha kufa. Basi, akamwita jemadari, akamwuliza kama Yesu alikuwa amekufa kitambo.
45ولما عرف من قائد المئة وهب الجسد ليوسف.
45Pilato alipoarifiwa na huyo jemadari kwamba Yesu alikuwa amekwisha kufa, akamruhusu Yosefu auchukue mwili wake.
46فاشترى كتانا فانزله وكفنه بالكتان ووضعه في قبر كان منحوتا في صخرة ودحرج حجرا على باب القبر.
46Hapo Yosefu akanunua sanda ya kitani, akauteremsha chini huo mwili, akauzungushia sanda. Akauweka katika kaburi lililokuwa limechongwa mwambani, kisha akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango.
47وكانت مريم المجدلية ومريم ام يوسي تنظران اين وضع
47Nao Maria Magdalene na Maria mama yake Yose walipaona hapo alipolazwa.