الكتاب المقدس (Van Dyke)

Swahili: New Testament

Matthew

22

1وجعل يسوع يكلمهم ايضا بامثال قائلا.
1Yesu alisema nao tena kwa kutumia mifano:
2يشبه ملكوت السموات انسانا ملكا صنع عرسا لابنه.
2"Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme aliyemwandalia mwanawe karamu ya arusi.
3وارسل عبيده ليدعوا المدعوين الى العرس فلم يريدوا ان يأتوا.
3Basi, akawatuma watumishi kuwaita walioalikwa waje arusini, lakini walioalikwa hawakutaka kufika.
4فارسل ايضا عبيدا آخرين قائلا قولوا للمدعوين هوذا غذائي اعددته. ثيراني ومسمناتي قد ذبحت وكل شيء معد. تعالوا الى العرس.
4Akawatuma tena watumishi wengine, akisema, Waambieni wale walioalikwa: karamu yangu iko tayari sasa; fahali wangu na ng'ombe wanono wamekwisha chinjwa; kila kitu ni tayari, njoni arusini.
5ولكنهم تهاونوا ومضوا واحد الى حقله وآخر الى تجارته.
5Lakini wao hawakujali, wakaenda zao; mmoja shambani kwake, mwingine kwenye shughuli zake,
6والباقون امسكوا عبيده وشتموهم وقتلوهم.
6na wengine wakawakamata wale watumishi wakawatukana, wakawaua.
7فلما سمع الملك غضب وارسل جنوده واهلك أولئك القاتلين واحرق مدينتهم.
7Yule mfalme akakasirika, akawatuma askari wake wakawaangamize wauaji hao na kuuteketeza mji wao.
8ثم قال لعبيده اما العرس فمستعد واما المدعوون فلم يكونوا مستحقين.
8Kisha akawaambia watumishi wake: Karamu ya arusi iko tayari kweli, lakini walioalikwa hawakustahili.
9فاذهبوا الى مفارق الطرق وكل من وجدتموه فادعوه الى العرس.
9Basi, nendeni kwenye barabara na wowote wale mtakaowakuta waiteni waje arusini.
10فخرج أولئك العبيد الى الطرق وجمعوا كل الذين وجدوهم اشرارا وصالحين. فامتلأ العرس من المتكئين.
10Wale watumishi wakatoka, wakaenda njiani, wakawaleta watu wote, wabaya na wema. Nyumba ya arusi ikajaa wageni.
11فلما دخل الملك لينظر المتكئين رأى هناك انسانا لم يكن لابسا لباس العرس.
11"Mfalme alipoingia kuwaona wageni, akamwona mtu mmoja ambaye hakuvaa mavazi ya arusi.
12فقال له يا صاحب كيف دخلت الى هنا وليس عليك لباس العرس. فسكت.
12Mfalme akamwuliza, Rafiki, umeingiaje hapa bila vazi la arusi? Lakini yeye akakaa kimya.
13حينئذ قال الملك للخدام اربطوا رجليه ويديه وخذوه واطرحوه في الظلمة الخارجية. هناك يكون البكاء وصرير الاسنان.
13Hapo mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni miguu na mikono mkamtupe nje gizani; huko atalia na kusaga meno."
14لان كثيرين يدعون وقليلين ينتخبون
14Yesu akamaliza kwa kusema, "Wengi wamealikwa, lakini wachache wameteuliwa."
15حينئذ ذهب الفريسيون وتشاوروا لكي يصطادوه بكلمة.
15Kisha, Mafarisayo wakaenda zao, wakashauriana jinsi ya kumnasa Yesu kwa maneno yake.
16فارسلوا اليه تلاميذهم مع الهيرودسيين قائلين يا معلّم نعلم انك صادق وتعلّم طريق الله بالحق ولا تبالي باحد لانك لا تنظر الى وجوه الناس.
16Basi, wakawatuma wafuasi wao pamoja na wafuasi wa kikundi cha Herode. Wakamwuliza, "Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwaminifu, na kwamba wafundisha njia ya Mungu kwa uaminifu; humwogopi mtu yeyote, maana cheo cha mtu si kitu kwako.
17فقل لنا ماذا تظن. أيجوز ان تعطى جزية لقيصر ام لا.
17Haya, twambie maoni yako. Je, ni halali au la, kulipa Kaisari?"
18فعلم يسوع خبثهم وقال لماذا تجربونني يا مراؤون.
18Lakini Yesu alitambua uovu wao, akawaambia, "Enyi
19أروني معاملة الجزية. فقدموا له دينارا.
19Nionyesheni fedha ya kulipia kodi." Nao wakamtolea sarafu ya fedha. sarafu ya fedha.
20فقال لهم لمن هذه الصورة والكتابة.
20Basi, Yesu akawauliza, "Sura na chapa hii ni ya nani?"
21قالوا له لقيصر. فقال لهم اعطوا اذا ما لقيصر لقيصر وما للّه للّه.
21Wakamjibu, "Ni vya Kaisari." Hapo Yesu akawaambia, "Basi, mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisari, na Mungu yaliyo yake Mungu."
22فلما سمعوا تعجبوا وتركوه ومضوا
22Waliposikia hivyo wakashangaa; wakamwacha, wakaenda zao.
23في ذلك اليوم جاء اليه صدوقيون الذين يقولون ليس قيامة فسألوه
23Siku hiyo, baadhi ya Masadukayo walimwendea Yesu. Hao ndio wale wasemao kwamba wafu hawafufuki.
24قائلين يا معلّم قال موسى ان مات احد وليس له اولاد يتزوج اخوه بامرأته ويقم نسلا لاخيه.
24Basi, wakamwambia, "Mwalimu, Mose alisema mtu aliyeoa akifa bila kuacha watoto, lazima ndugu yake amwoe huyo mama mjane, amzalie ndugu yake watoto.
25فكان عندنا سبعة اخوة وتزوج الاول ومات. واذ لم يكن له نسل ترك امرأته لاخيه.
25Sasa, hapa petu palikuwa na ndugu saba. Wa kwanza alioa kisha akafa bila kujaliwa watoto, akamwachia ndugu yake huyo mke wake mjane.
26وكذلك الثاني والثالث الى السبعة.
26Ikawa vivyo hivyo kwa ndugu wa pili, na wa tatu, mpaka wa saba.
27وآخر الكل ماتت المرأة ايضا.
27Baada ya ndugu hao wote kufa, akafa pia yule mama.
28ففي القيامة لمن من السبعة تكون زوجة. فانها كانت للجميع.
28Je, siku wafu watakapofufuka mama huyo atakuwa mke wa nani miongoni mwa wale ndugu saba? Maana Wote saba walimwoa."
29فاجاب يسوع وقال لهم تضلون اذ لا تعرفون الكتب ولا قوة الله.
29Yesu akawajibu, "Kweli mmekosea kwa sababu hamjui Maandiko Matakatifu wala nguvu ya Mungu!
30لانهم في القيامة لا يزوجون ولا يتزوجون بل يكونون كملائكة الله في السماء.
30Maana wafu watakapofufuliwa hawataoa wala kuolewa, watakuwa kama malaika mbinguni.
31واما من جهة قيامة الاموات أفما قرأتم ما قيل لكم من قبل الله القائل
31Lakini kuhusu suala la wafu kufufuka, hamjasoma yale aliyowaambieni Mungu?
32انا اله ابراهيم واله اسحق واله يعقوب. ليس الله اله اموات بل اله احياء.
32Aliwaambia, Mimi ni Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo! Basi, yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai."
33فلما سمع الجموع بهتوا من تعليمه
33Ule umati wa watu uliposikia hivyo ukayastaajabia mafundisho yake.
34اما الفريسيون فلما سمعوا انه ابكم الصدوقيين اجتمعوا معا.
34Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwa amewanyamazisha Masadukayo, wakakutana pamoja.
35وسأله واحد منهم وهو ناموسي ليجربه قائلا
35Mmoja wao, mwanasheria, akamwuliza Yesu kwa kumjaribu,
36يا معلّم اية وصية هي العظمى في الناموس.
36"Mwalimu, ni amri ipi iliyo kuu katika Sheria ya Mose?"
37فقال له يسوع تحب الرب الهك من كل قلبك ومن كل نفسك ومن كل فكرك.
37Yesu akamjibu, "Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote na kwa akili yako yote.
38هذه هي الوصية الاولى والعظمى.
38Hii ndiyo amri kuu ya kwanza.
39والثانية مثلها. تحب قريبك كنفسك.
39Ya pili inafanana na hiyo: Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe.
40بهاتين الوصيتين يتعلق الناموس كله والانبياء
40Sheria yote ya Mose na mafundisho ya manabii vinategemea amri hizi mbili."
41وفيما كان الفريسيون مجتمعين سألهم يسوع
41Mafarisayo walipokusanyika pamoja, Yesu aliwauliza,
42قائلا ماذا تظنون في المسيح. ابن من هو. قالوا له ابن داود.
42"Ninyi mwaonaje juu ya Kristo? Je, ni mwana wa nani?" Wakamjibu, "Wa Daudi."
43قال لهم فكيف يدعوه داود بالروح ربا قائلا
43Yesu akawaambia, "Basi, inawezekanaje kwamba kwa nguvu ya Roho Mtakatifu Daudi anamwita yeye Bwana? Maana alisema:
44قال الرب لربي اجلس عن يميني حتى اضع اعداءك موطئا لقدميك.
44Bwana alimwambia Bwana wangu: keti upande wangu wa kulia, mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako.
45فان كان داود يدعوه ربا فكيف يكون ابنه.
45Basi, ikiwa Daudi anamwita Kristo Bwana, anawezaje kuwa mwanawe?"
46فلم يستطع احد ان يجيبه بكلمة. ومن ذلك اليوم لم يجسر احد ان يسأله بتة
46Hakuna mtu yeyote aliyeweza kumjibu neno. Na tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu tena kumwuliza swali.