1But concerning the times and the seasons, brethren, ye have no need that aught be written unto you.
1Ndugu, hakuna haja ya kuwaandikieni juu ya nyakati na majira yatakapotukia mambo haya.
2For yourselves know perfectly that the day of the Lord so cometh as a thief in the night.
2Maana ninyi wenyewe mwajua kwamba Siku ya Bwana itakuja kama mwizi ajavyo usiku.
3When they are saying, Peace and safety, then sudden destruction cometh upon them, as travail upon a woman with child; and they shall in no wise escape.
3Watu watakapokuwa wanasema: "Kila kitu ni shwari na salama" ndipo uharibifu utakapowaangukia ghafla! Mambo hayo yatatukia ghafla kama uchungu wa uzazi unavyomjia mama anayejifungua, wala watu hawataweza kuepukana nayo.
4But ye, brethren, are not in darkness, that that day should overtake you as a thief:
4Lakini ninyi ndugu, hamko gizani, na siku hiyo haipaswi kuwajieni ghafla kama vile mwizi.
5for ye are all sons of light, and sons of the day: we are not of the night, nor of darkness;
5Ninyi nyote ni watu mnaoishi katika mwanga, watu wa mchana. Sisi si watu wa usiku, wala wa giza.
6so then let us not sleep, as do the rest, but let us watch and be sober.
6Basi, tusilale usingizi kama wengine; tunapaswa kukesha na kuwa na kiasi.
7For they that sleep sleep in the night: and they that are drunken are drunken in the night.
7Wanaolala hulala usiku, na walevi hulewa usiku.
8But let us, since we are of the day, be sober, putting on the breastplate of faith and love; and for a helmet, the hope of salvation.
8Lakini sisi ni watu wa mchana na tunapaswa kuwa na kiasi. Tunapaswa kuvaa imani na upendo kama vazi la kujikinga kifuani, na tumaini letu la wokovu kama kofia ya chuma.
9For God appointed us not into wrath, but unto the obtaining of salvation through our Lord Jesus Christ,
9Maana Mungu hakututeua ili tuangamizwe na ghadhabu yake, bali tuupate wokovu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,
10who died for us, that, whether we wake or sleep, we should live together with him.
10ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, iwe tu hai au tumekufa.
11Wherefore exhort one another, and build each other up, even as also ye do.
11Kwa hiyo farijianeni na kusaidiana ninyi kwa ninyi kama mnavyofanya sasa.
12But we beseech you, brethren, to know them that labor among you, and are over you in the Lord, and admonish you;
12Ndugu, tunawaombeni muwastahi wale wanaofanya kazi kati yenu, wale wanaowaongoza na kuwafundisheni kuhusu maisha ya Kikristo.
13and to esteem them exceeding highly in love for their work's sake. Be at peace among yourselves.
13Wapeni heshima kubwa na kuwapenda kwa sababu ya kazi wanayofanya. Muwe na amani kati yenu.
14And we exhort you, brethren, admonish the disorderly, encourage the fainthearted, support the weak, be longsuffering toward all.
14Ndugu, tunawahimizeni muwaonye watu walio wavivu, muwatie moyo watu wanyonge, muwasaidie watu dhaifu, muwe na subira kwa wote.
15See that none render unto any one evil for evil; but always follow after that which is good, one toward another, and toward all.
15Angalieni mtu yeyote asimlipe mwingine maovu kwa maovu, ila nia yenu iwe kutendeana mema daima na kuwatendea mema watu wote.
16Rejoice always;
16Furahini daima,
17pray without ceasing;
17salini kila wakati
18in everything give thanks: for this is the will of God in Christ Jesus to you-ward.
18na muwe na shukrani katika kila hali. Hayo ndiyo anayotaka Mungu kwenu katika kuungana kwenu na Kristo Yesu.
19Quench not the Spirit;
19Msimpinge Roho Mtakatifu;
20despise not prophesyings;
20msidharau unabii.
21prove all things; hold fast that which is good;
21Pimeni kila kitu: zingatieni kilicho chema,
22abstain from every form of evil.
22na epukeni kila aina ya uovu.
23And the God of peace himself sanctify you wholly; and may your spirit and soul and body be preserved entire, without blame at the coming of our Lord Jesus Christ.
23Mungu anayetupatia amani awafanye ninyi watakatifu kwa kila namna na kuzilinda nafsi zenu--roho, mioyo na miili yenu--mbali na hatia yoyote wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
24Faithful is he that calleth you, who will also do it.
24Yeye anayewaita ninyi atafanya hivyo kwani ni mwaminifu.
25Brethren, pray for us.
25Ndugu, tuombeeni na sisi pia.
26Salute all the brethren with a holy kiss.
26Wasalimuni ndugu wote kwa ishara ya upendo.
27I adjure you by the Lord that this epistle be read unto all the brethren.
27Nawahimizeni kwa jina la Bwana muwasomee ndugu zetu wote barua hii.
28The grace of our Lord Jesus Christ be with you.
28Tunawatakieni neema ya Bwana wetu Yesu Kristo.