1Now there were some present at that very season who told him of the Galilaeans, whose blood Pilate had mingled with their sacrifices.
1Wakati huo watu fulani walikuja, wakamweleza Yesu juu ya watu wa Galilaya ambao Pilato alikuwa amewaua wakati walipokuwa wanachinja wanyama wao wa tambiko.
2And he answered and said unto them, Think ye that these Galilaeans were sinners above all the Galilaeans, because they have suffered these things?
2Naye Yesu akawaambia, "Mnadhani Wagalilaya hao walikuwa wahalifu zaidi kuliko Wagalilaya wengine, ati kwa sababu wameteseka hivyo?
3I tell you, Nay: but, except ye repent, ye shall all in like manner perish.
3Nawaambieni hakika sivyo; lakini nanyi, hali kadhalika, msipotubu, mtaangamia kama wao.
4Or those eighteen, upon whom the tower in Siloam fell, and killed them, think ye that they were offenders above all the men that dwell in Jerusalem?
4Au wale kumi na wanane walioangukiwa na mnara kule Siloamu wakafa; mnadhani wao walikuwa wakosefu zaidi kuliko wengine wote walioishi Yerusalemu?
5I tell you, Nay: but, except ye repent, ye shall all likewise perish.
5Nawaambieni sivyo; lakini nanyi msipotubu, mtaangamia kama wao."
6And he spake this parable; A certain man had a fig tree planted in his vineyard; and he came seeking fruit thereon, and found none.
6Kisha, Yesu akawaambia mfano huu: "Mtu mmoja alikuwa na mtini katika shamba lake. Mtu huyu akaenda akitaka kuchuma matunda yake, lakini akaukuta haujazaa hata tunda moja.
7And he said unto the vinedresser, Behold, these three years I come seeking fruit on this fig tree, and find none: cut it down; why doth it also cumber the ground?
7Basi, akamwambia mfanyakazi wake: Angalia! Kwa miaka mitatu nimekuwa nikija kuchuma matunda ya mtini huu, nami nisiambulie kitu. Ukate! Kwa nini uitumie ardhi bure?
8And he answering saith unto him, Lord, let it alone this year also, till I shall dig about it, and dung it:
8Lakini naye akamjibu: Bwana, tuuache tena mwaka huu; nitauzungushia mtaro na kuutilia mbolea.
9and if it bear fruit thenceforth, [well]; but if not, thou shalt cut it down.
9Kama ukizaa matunda mwaka ujao, vema; la sivyo, basi utaweza kuukata."
10And he was teaching in one of the synagogues on the sabbath day.
10Yesu alikuwa akifundisha katika sunagogi moja siku ya Sabato.
11And behold, a woman that had a spirit of infirmity eighteen years; and she was bowed together, and could in no wise lift herself up.
11Na hapo palikuwa na mwanamke mmoja aliyekuwa mgonjwa kwa miaka kumi na minane kutokana na pepo aliyekuwa amempagaa. Kwa sababu hiyo, mwili wake ulikuwa umepindika vibaya hata asiweze kusimama wima.
12And when Jesus saw her, he called her, and said to her, Woman, thou art loosed from thine infirmity.
12Yesu alipomwona, alimwita, akamwambia, "Mama, umeponywa ugonjwa wako."
13And he laid his hands upon her: and immediately she was made straight, and glorified God.
13Akamwekea mikono, na mara mwili wake ukawa wima tena, akawa anamtukuza Mungu.
14And the ruler of the synagogue, being moved with indignation because Jesus had healed on the sabbath, answered and said to the multitude, There are six days in which men ought to work: in them therefore come and be healed, and not on the day of the sabbath.
14Lakini mkuu wa sunagogi alikasirika kwa sababu Yesu alikuwa amemponya siku ya Sabato. Hivyo akawaambia wale watu walikusanyika pale, "Mnazo siku sita za kufanya kazi. Basi, fikeni siku hizo mkaponywe magonjwa yenu; lakini msije siku ya Sabato."
15But the Lord answered him, and said, Ye hypocrites, doth not each one of you on the sabbath loose his ox or his ass from the stall, and lead him away to watering?
15Hapo Bwana akamjibu, "Enyi wanafiki! Nani kati yenu hangemfungua ng'ombe au punda wake kutoka zizini ampeleke kunywa maji, hata kama siku hiyo ni ya Sabato?
16And ought not this woman, being a daughter of Abraham, whom Satan had bound, lo, [these] eighteen years, to have been loosed from this bond on the day of the sabbath?
16Sasa, hapa yupo binti wa Abrahamu ambaye Shetani alimfanya kilema kwa muda wa miaka kumi na minane. Je, haikuwa vizuri kumfungulia vifungo vyake siku ya Sabato?"
17And as he said these things, all his adversaries were put to shame: and all the multitude rejoiced for all the glorious things that were done by him.
17Alipokwisha sema hayo, wapinzani wake waliona aibu lakini watu wengine wote wakajaa furaha kwa sababu ya mambo yote aliyotenda.
18He said therefore, Unto what is the kingdom of God like? and whereunto shall I liken it?
18Yesu akauliza: "Ufalme wa Mungu unafanana na nini? Nitaulinganisha na nini?
19It is like unto a grain of mustard seed, which a man took, and cast into his own garden; and it grew, and became a tree; and the birds of the heaven lodged in the branches thereof.
19NI kama mbegu ya haradali aliyotwaa mtu mmoja na kuipanda shambani mwake; ikaota hata ikawa mti. Ndege wa angani wakajenga viota vyao katika matawi yake."
20And again he said, Whereunto shall I liken the kingdom of God?
20Tena akauliza: "Nitaulinganisha Ufalme wa Mungu na nini?
21It is like unto leaven, which a woman took and hid in three measures of meal, till it was all leavened.
21Ni kama chachu aliyoitwaa mama mmoja na kuichanganya pamoja na unga debe moja kisha unga wote ukaumuka wote."
22And he went on his way through cities and villages, teaching, and journeying on unto Jerusalem.
22Yesu alindelea na safari yake kwenda Yerusalemu huku akipitia mijini na vijijini, akihubiri.
23And one said unto him, Lord, are they few that are saved? And he said unto them,
23Mtu mmoja akamwuliza, "Je, Mwalimu, watu watakaookoka ni wachache?"
24Strive to enter in by the narrow door: for many, I say unto you, shall seek to enter in, and shall not be able.
24Yesu akawaambia, "Jitahidini kuingia kwa kupitia mlango mwembamba; maana nawaambieni, wengi watajaribu kuingia lakini hawataweza.
25When once the master of the house is risen up, and hath shut to the door, and ye begin to stand without, and to knock at the door, saying, Lord, open to us; and he shall answer and say to you, I know you not whence ye are;
25"Wakati utakuja ambapo mwenye nyumba atainuka na kufunga mlango. Ninyi mtasimama nje na kuanza kupiga hodi mkisema: Bwana, tufungulie mlango. Lakini yeye atawajibu: Sijui mmetoka wapi.
26then shall ye begin to say, We did eat and drink in thy presence, and thou didst teach in our streets;
26Nanyi mtaanza kumwambia: Sisi ndio wale tuliokula na kunywa pamoja nawe; na wewe ulifundisha katika vijiji vyetu.
27and he shall say, I tell you, I know not whence ye are; depart from me, all ye workers of iniquity.
27Lakini yeye atasema: Sijui ninyi mmetoka wapi; ondokeni mbele yangu, enyi nyote watenda maovu.
28There shall be the weeping and the gnashing of teeth, when ye shall see Abraham, and Isaac, and Jacob, and all the prophets, in the kingdom of God, and yourselves cast forth without.
28Ndipo mtakuwa na kulia na kusaga meno, wakati mtakapowaona Abrahamu, Isaka na Yakobo, na manabii wote wapo katika Ufalme wa Mungu, lakini ninyi wenyewe mmetupwa nje!
29And they shall come from the east and west, and from the north and south, and shall sit down in the kingdom of God.
29Watu watakuja kutoka mashariki na magharibi, kutoka kaskazini na kusini, watakuja na kukaa kwenye karamu katika Ufalme wa Mungu.
30And behold, there are last who shall be first, and there are first who shall be last.
30Naam, wale walio wa mwisho watakuwa wa kwanza; na wale walio wa kwanza watakuwa wa mwisho."
31In that very hour there came certain Pharisees, saying to him, Get thee out, and go hence: for Herod would fain kill thee.
31Wakati huohuo, Mafarisayo na watu wengine walimwendea Yesu wakamwambia, "Ondoka hapa uende mahali pengine, kwa maana Herode anataka kukuua."
32And he said unto them, Go and say to that fox, Behold, I cast out demons and perform cures to-day and to-morrow, and the third [day] I am perfected.
32Yesu akawajibu, "Nendeni mkamwambie huyo mbweha hivi: Leo na kesho ninafukuza pepo na kuponya wagonjwa, na siku ya tatu nitakamilisha kazi yangu.
33Nevertheless I must go on my way to-day and to-morrow and the [day] following: for it cannot be that a prophet perish out of Jerusalem.
33Hata hivyo, kwa leo, kesho na kesho kutwa, ni lazima niendelee na safari yangu, kwa sababu si sawa nabii auawe nje ya Yerusalemu.
34O Jerusalem, Jerusalem, that killeth the prophets, and stoneth them that are sent unto her! how often would I have gathered thy children together, even as a hen [gathereth] her own brood under her wings, and ye would not!
34"Yerusalemu! We Yerusalemu! Unawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako pamoja kama kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake, Lakini wewe umekataa.
35Behold, your house is left unto you [desolate]: and I say unto you, Ye shall not see me, until ye shall say, Blessed is he that cometh in the name of the Lord.
35Haya, utaachiwa mwenyewe nyumba yako. Naam, hakika nawaambieni, hamtaniona mpaka wakati utakapofika mseme: Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana."