American Standard Version

Swahili: New Testament

Mark

1

1The beginning of the gospel of Jesus Christ, the Son of God.
1Habari Njema ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.
2Even as it is written in Isaiah the prophet, Behold, I send my messenger before thy face, Who shall prepare thy way.
2Ilianza kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: "Tazama, namtuma mjumbe wangu akutangulie; yeye atakutayarishia njia yako.
3The voice of one crying in the wilderness, Make ye ready the way of the Lord, Make his paths straight;
3Sauti ya mtu imesikika jangwani: Mtayarishieni Bwana njia yake, nyoosheni mapito yake."
4John came, who baptized in the wilderness and preached the baptism of repentance unto remission of sins.
4Yohane Mbatizaji alitokea jangwani, akahubiri kwamba ni lazima watu watubu na kubatizwa ili Mungu awasamehe dhambi zao.
5And there went out unto him all the country of Judaea, and all they of Jerusalem; And they were baptized of him in the river Jordan, confessing their sins.
5Watu kutoka sehemu zote za Yudea na wenyeji wote wa Yerusalemu walimwendea, wakaziungama dhambi zao, naye akawabatiza katika mto Yordani.
6And John was clothed with camel's hair, and [had] a leathern girdle about his loins, and did eat locusts and wild honey.
6Yohane alikuwa amevaa vazi lililofumwa kwa manyoya ya ngamia, na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.
7And he preached, saying, There cometh after me he that is mightier than I, the latchet of whose shoes I am not worthy to stoop down and unloose.
7Naye alihubiri akisema, "Baada yangu anakuja mwenye uwezo zaidi kuliko mimi, ambaye mimi sistahili hata kuinama na kufungua kamba za viatu vyake.
8I baptized you in water; But he shall baptize you in the Holy Spirit.
8Mimi ninawabatiza kwa maji, lakini yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu."
9And it came to pass in those days, that Jesus came from Nazareth of Galilee, and was baptized of John in the Jordan.
9Siku hizo, Yesu alifika kutoka Nazareti, mji wa Galilaya, akabatizwa na Yohane katika mto Yordani.
10And straightway coming up out of the water, he saw the heavens rent asunder, and the Spirit as a dove descending upon him:
10Mara tu alipotoka majini, aliona mbingu zimefunguliwa, na Roho akishuka juu yake kama njiwa.
11And a voice came out of the heavens, Thou art my beloved Son, in thee I am well pleased.
11Sauti ikasikika kutoka mbinguni: "Wewe ni Mwanangu mpendwa, nimependezwa nawe."
12And straightway the Spirit driveth him forth into the wilderness.
12Mara akaongozwa na Roho kwenda jangwani,
13And he was in the wilderness forty days tempted of Satan; And he was with the wild beasts; And the angels ministered unto him.
13akakaa huko siku arubaini akijaribiwa na Shetani. Alikuwa huko pamoja na wanyama wa porini, nao malaika wakawa wanamtumikia.
14Now after John was delivered up, Jesus came into Galilee, preaching the gospel of God,
14Yohane alipokwisha fungwa gerezani, Yesu alikwenda Galilaya, akahubiri Habari Njema ya Mungu, akisema,
15and saying, The time is fulfilled, and the kingdom of God is at hand: repent ye, and believe in the gospel.
15"Wakati umetimia, na Ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini Habari Njema!"
16And passing along by the sea of Galilee, he saw Simon and Andrew the brother of Simon casting a net in the sea; for they were fishers.
16Alipokuwa anapita kando ya ziwa Galilaya, aliwaona wavuvi wawili: Simoni na Andrea ndugu yake wakivua samaki kwa wavu.
17And Jesus said unto them, Come ye after me, and I will make you to become fishers of men.
17Yesu akawaambia, "Nifuateni nami nitawafanya ninyi wavuvi wa watu."
18And straightway they left the nets, and followed him.
18Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.
19And going on a little further, he saw James the [son] of Zebedee, and John his brother, who also were in the boat mending the nets.
19Alipokwenda mbele kidogo, aliwaona Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo. Nao pia walikuwa ndani ya mashua yao wakizitengeneza nyavu zao.
20And straightway he called them: and they left their father Zebedee in the boat with the hired servants, and went after him.
20Yesu akawaita mara, nao wakamwacha baba yao Zebedayo katika mashua pamoja na wafanyakazi, wakamfuata.
21And they go into Capernaum; and straightway on the sabbath day he entered into the synagogue and taught.
21Wakafika mjini Kafarnaumu, na mara ilipofika Sabato, Yesu akaingia katika Sunagogi, akaanza kufundisha.
22And they were astonished at his teaching: For he taught them as having authority, and not as the scribes.
22Watu wote waliomsikia walishangazwa na mafundisho yake, maana hakuwa anafundisha kama walimu wao wa Sheria, bali kama mtu mwenye mamlaka.
23And straightway there was in their synagogue a man with an unclean spirit; and he cried out,
23Mara akatokea mle ndani ya sunagogi mtu mmoja mwenye pepo mchafu,
24saying, What have we to do with thee, Jesus thou Nazarene? art thou come to destroy us? I know thee who thou art, the Holy One of God.
24akapaaza sauti, "Una nini nasi, wewe Yesu wa Nazareti? Je, umekuja kutuangamiza? Najua wewe ni nani: wewe ni Mtakatifu wa Mungu!"
25And Jesus rebuked him, saying, Hold thy peace, and come out of him.
25Yesu akamkemea, "Nyamaza! Mtoke mtu huyu."
26And the unclean spirit, tearing him and crying with a loud voice, came out of him.
26Basi, huyo pepo mchafu akamtikisatikisa mtu huyo, kisha akalia kwa sauti kubwa, akamtoka.
27And they were all amazed, insomuch that they questioned among themselves, saying, What is this? a new teaching! with authority he commandeth even the unclean spirits, and they obey him.
27Watu wote wakashangaa, wakaulizana, "Ni mambo gani haya? Je, ni mafundisho mapya? Mtu huyu anayo mamlaka ya kuamuru hata pepo wachafu, nao wanamtii!"
28And the report of him went out straightway everywhere into all the region of Galilee round about.
28Habari za Yesu zikaenea upesi kila mahali katika wilaya ya Galilaya.
29And straightway, when they were come out of the synagogue, they came into the house of Simon and Andrew, with James and John.
29Wakatoka katika sunagogi, wakaenda moja kwa moja hadi nyumbani kwa Simoni na Andrea; Yakobo na Yohane walikwenda pamoja nao.
30Now Simon's wife's mother lay sick of a fever; and straightway they tell him of her:
30Basi, mama mmoja, mkwewe Simoni, alikuwa kitandani ana homa kali. Wakamwarifu Yesu mara alipowasili.
31and he came and took her by the hand, and raised her up; and the fever left her, and she ministered unto them.
31Yesu akamwendea huyo mama, akamshika mkono, akamwinua. Na ile homa ikamwacha, akaanza kuwatumikia.
32And at even, when the sun did set, they brought unto him all that were sick, and them that were possessed with demons.
32Jioni, jua lilipokwisha tua, wakamletea Yesu wagonjwa wote na watu waliopagawa na pepo.
33And all the city was gathered together at the door.
33Watu wote wa mji ule wakakusanyika nje ya mlango.
34And he healed many that were sick with divers diseases, and cast out many demons; and he suffered not the demons to speak, because they knew him.
34Naye Yesu akawaponya watu wengi waliokuwa na magonjwa mbalimbali; aliwafukuza pepo wengi, lakini hakuwaruhusu kusema kitu maana walikuwa wanamjua yeye ni nani.
35And in the morning, a great while before day, he rose up and went out, and departed into a desert place, and there prayed.
35Kesho yake, kabla ya mapambazuko, Yesu alitoka, akaenda mahali pa faragha kusali.
36And Simon and they that were with him followed after him;
36Simoni na wenzake wakaenda kumtafuta.
37and they found him, and say unto him, All are seeking thee.
37Walipomwona wakamwambia, "Kila mtu anakutafuta."
38And he saith unto them, Let us go elsewhere into the next towns, that I may preach there also; for to this end came I forth.
38Yesu akawaambia, "Twendeni katika miji mingine ya jirani nikahubiri huko pia, maana nimekuja kwa sababu hiyo."
39And he went into their synagogues throughout all Galilee, preaching and casting out demons.
39Basi, akaenda kila mahali Galilaya akihubiri katika masunagogi na kufukuza pepo.
40And there cometh to him a leper, beseeching him, and kneeling down to him, and saying unto him, If thou wilt, thou canst make me clean.
40Mtu mmoja mwenye ukoma alimwendea Yesu, akapiga magoti, akamwomba, "Ukitaka, waweza kunitakasa!"
41And being moved with compassion, he stretched forth his hand, and touched him, and saith unto him, I will; be thou made clean.
41Yesu akamwonea huruma, akanyosha mkono wake, akamgusa na kumwambia, "Nataka, takasika!"
42And straightway the leprosy departed from him, and he was made clean.
42Mara ukoma ukamwacha mtu huyo, akatakasika.
43And he strictly charged him, and straightway sent him out,
43Kisha Yesu akamwambia aende zake upesi na kumwonya vikali,
44and saith unto him, See thou say nothing to any man: but go show thyself to the priest, and offer for thy cleansing the things which Moses commanded, for a testimony unto them.
44"Usimwambie mtu yeyote jambo hili, ila nenda ukajionyeshe kwa kuhani; kisha utoe sadaka kwa ajili ya kutakasika kwako kama alivyoamuru Mose, iwe uthibitisho kwao kwamba umepona."
45But he went out, and began to publish it much, and to spread abroad the matter, insomuch that Jesus could no more openly enter into a city, but was without in desert places: and they came to him from every quarter.
45Lakini huyo mtu akaenda, akaanza kueneza habari hiyo kila mahali na kusema mambo mengi hata Yesu hakuweza tena kuingia katika mji wowote waziwazi; ikamlazimu kukaa nje, mahali pa faragha. Hata hivyo, watu wakamwendea kutoka kila upande.