American Standard Version

Swahili: New Testament

Matthew

13

1On that day went Jesus out of the house, and sat by the sea side.
1Siku hiyohiyo, Yesu alitoka katika ile nyumba, akaenda na kuketi kando ya ziwa.
2And there were gathered unto him great multitudes, so that he entered into a boat, and sat; and all the multitude stood on the beach.
2Makundi makubwa ya watu yalimzunguka hata Yesu akapanda mashua, akaketi. Hao watu walisimama kwenye ukingo wa ziwa,
3And he spake to them many things in parables, saying, Behold, the sower went forth to sow;
3naye Yesu akawaambia mambo mengi kwa mifano. "Sikilizeni! Mpanzi alikwenda kupanda mbegu.
4and as he sowed, some [seeds] fell by the way side, and the birds came and devoured them:
4Alipokuwa akipanda, nyingine zilianguka njiani, ndege wakaja wakazila.
5and others fell upon the rocky places, where they had not much earth: and straightway they sprang up, because they had no deepness of earth:
5Nyingine zilianguka penye mawe pasipokuwa na udongo mwingi. Zikaota mara kwa kuwa udongo haukuwa na kina.
6and when the sun was risen, they were scorched; and because they had no root, they withered away.
6Jua lilipochomoza, zilichomeka; na kwa kuwa mizizi yake haikuwa na nguvu, zikanyauka.
7And others fell upon the thorns; and the thorns grew up and choked them:
7Nyingine zilianguka kwenye miti ya miiba, nayo ikakua na kuzisonga.
8and others fell upon the good ground, and yielded fruit, some a hundredfold, some sixty, some thirty.
8Lakini nyingine zilianguka penye udongo mzuri, zikaota, zikazaa: nyingine punje mia moja, nyingine sitini na nyingine thelathini.
9He that hath ears, let him hear.
9Mwenye masikio na asikie!"
10And the disciples came, and said unto him, Why speakest thou unto them in parables?
10Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwuliza, "Kwa nini unasema na watu kwa mifano?"
11And he answered and said unto them, Unto you it is given to know the mysteries of the kingdom of heaven, but to them it is not given.
11Yesu akawajibu, "Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za Ufalme wa mbinguni, lakini wao hawakujaliwa.
12For whosoever hath, to him shall be given, and he shall have abundance: but whosoever hath not, from him shall be taken away even that which he hath.
12Maana, aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa; lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
13Therefore speak I to them in parables; because seeing they see not, and hearing they hear not, neither do they understand.
13Ndiyo maana ninasema nao kwa mifano, kwa sababu wanatazama lakini hawaoni, wanasikiliza lakini hawasikii, wala hawaelewi.
14And unto them is fulfilled the prophecy of Isaiah, which saith, By hearing ye shall hear, and shall in no wise understand; And seeing ye shall see, and shall in no wise perceive:
14Kwao yametimia yale aliyosema nabii Isaya: Kusikia mtasikia, lakini hamtaelewa; Kutazama mtatazama, lakini hamtaona.
15For this people's heart is waxed gross, And their ears are dull of hearing, And their eyes they have closed; Lest haply they should perceive with their eyes, And hear with their ears, And understand with their heart, And should turn again, And I should heal them.
15Maana akili za watu hawa zimepumbaa, wameyaziba masikio yao, wameyafumba macho yao. La sivyo, wangeona kwa macho yao. wangesikia kwa masikio yao, wangeelewa kwa akili zao, na kunigeukia, asema Bwana, nami ningewaponya.
16But blessed are your eyes, for they see; and your ears, for they hear.
16"Lakini heri yenu ninyi, maana macho yenu yanaona na masikio yenu yanasikia.
17For verily I say unto you, that many prophets and righteous men desired to see the things which ye see, and saw them not; and to hear the things which ye hear, and heard them not.
17Kweli nawaambieni, manabii na watu wengi wema walitamani kuyaona yale mnayoyaona, wasiyaone, na kuyasikia yale mnayoyasikia, wasiyasikie.
18Hear then ye the parable of the sower.
18"Basi, ninyi sikilizeni maana ya mfano huo wa mpanzi.
19When any one heareth the word of the kingdom, and understandeth it not, [then] cometh the evil [one], and snatcheth away that which hath been sown in his heart. This is he that was sown by the way side.
19Yeyote asikiaye ujumbe wa ufalme bila kuuelewa, ni kama zile mbegu zilizoanguka njiani; yule Mwovu huja na kunyakua kile kilichopandwa moyoni mwake.
20And he that was sown upon the rocky places, this is he that heareth the word, and straightway with joy receiveth it;
20Ile mbegu iliyopandwa penye mawe ni mfano wa mtu asikiaye ujumbe huo na mara akaupokea kwa furaha.
21yet hath he not root in himself, but endureth for a while; and when tribulation or persecution ariseth because of the word, straightway he stumbleth.
21Lakini haumwingii na kuwa na mizizi ndani yake; huendelea kuuzingatia ujumbe huo kwa kitambo tu, na wakati taabu au udhalimu vinapotokea kwa sababu ya ujumbe huo, anakata tamaa mara.
22And he that was sown among the thorns, this is he that heareth the word; and the care of the world, and the deceitfulness of riches, choke the word, and he becometh unfruitful.
22Ile mbegu iliyoanguka kati ya miti ya miiba, ni mfano wa mtu asikiaye huo ujumbe, lakini wasiwasi wa ulimwengu huu na anasa za mali huusonga ujumbe huo, naye hazai matunda.
23And he that was sown upon the good ground, this is he that heareth the word, and understandeth it; who verily beareth fruit, and bringeth forth, some a hundredfold, some sixty, some thirty.
23Ile mbegu iliyopandwa katika udongo mzuri ni mfano wa mtu ausikiaye ujumbe huo na kuuelewa, naye huzaa matunda; mmoja mia, mwingine sitini na mwingine thelathini."
24Another parable set he before them, saying, The kingdom of heaven is likened unto a man that sowed good seed in his field:
24Yesu akawaambia watu mfano mwingine: "Ufalme wa mbinguni unafanana na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake.
25but while men slept, his enemy came and sowed tares also among the wheat, and went away.
25Lakini watu wakiwa wamelala, adui yake akaja akapanda magugu kati ya ngano, akaenda zake.
26But when the blade sprang up and brought forth fruit, then appeared the tares also.
26Basi, mimea ilipoota na kuanza kuchanua, magugu pia yakaanza kuonekana.
27And the servants of the householder came and said unto him, Sir, didst thou not sow good seed in thy field? whence then hath it tares?
27Watumishi wa yule mwenye shamba wakamwendea, wakamwambia, Mheshimiwa, bila shaka ulipanda mbegu nzuri katika shamba lako. Sasa magugu yametoka wapi?
28And he said unto them, An enemy hath done this. And the servants say unto him, Wilt thou then that we go and gather them up?
28Yeye akawajibu, Adui ndiye aliyefanya hivyo. Basi, watumishi wake wakamwuliza, Je, unataka twende tukayang'oe
29But he saith, Nay; lest haply while ye gather up the tares, ye root up the wheat with them.
29Naye akawajibu, La, msije labda mnapokusanya magugu, mkang'oa na ngano pia.
30Let both grow together until the harvest: and in the time of the harvest I will say to the reapers, Gather up first the tares, and bind them in bundles to burn them; but gather the wheat into my barn.
30Acheni vikue pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati huo nitawaambia wavunaji: kusanyeni kwanza magugu mkayafunge mafungumafungu ya kuchomwa. Lakini ngano ikusanyeni mkaiweke ghalani mwangu."
31Another parable set he before them, saying, The kingdom of heaven is like unto a grain of mustard seed, which a man took, and sowed in his field:
31Yesu akawaambia watu mfano mwingine: "Ufalme wa mbinguni unafanana na mbegu ya haradali aliyotwaa mtu mmoja, akaipanda katika shamba lake.
32which indeed is less than all seeds; but when it is grown, it is greater than the herbs, and becometh a tree, so that the birds of the heaven come and lodge in the branches thereof.
32Yenyewe ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini ikishaota huwa kubwa kuliko mimea yote. Hukua ikawa mti, na ndege wa angani huja na kujenga viota katika matawi yake."
33Another parable spake he unto them; The kingdom of heaven is like unto leaven, which a woman took, and hid in three measures of meal, till it was all leavened.
33Yesu akawaambia mfano mwingine: "Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyotwaa mama mmoja, akaichanganya na unga pishi tatu, hata unga wote ukaumuka."
34All these things spake Jesus in parables unto the multitudes; and without a parable spake he nothing unto them:
34Yesu aliwaambia watu hayo yote kwa mifano. Hakuwaambia chochote bila kutumia mifano,
35that it might be fulfilled which was spoken through the prophet, saying, I will open my mouth in parables; I will utter things hidden from the foundation of the world.
35ili jambo lililonenwa na nabii litimie: "Nitasema kwa mifano; nitawaambia mambo yaliyofichika tangu kuumbwa ulimwengu."
36Then he left the multitudes, and went into the house: and his disciples came unto him, saying, Explain unto us the parable of the tares of the field.
36Kisha Yesu aliwaaga wale watu, akaingia nyumbani. Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwambia, "Tufafanulie ule mfano wa magugu shambani."
37And he answered and said, He that soweth the good seed is the Son of man;
37Yesu akawaambia, "Mpanzi wa zile mbegu nzuri ni Mwana wa Mtu.
38and the field is the world; and the good seed, these are the sons of the kingdom; and the tares are the sons of the evil [one];
38Lile shamba ni ulimwengu. Zile mbegu nzuri ni watu wale ambao Ufalme ni wao. Lakini yale magugu ni wale watu wa yule Mwovu.
39and the enemy that sowed them is the devil: and the harvest is the end of the world; and the reapers are angels.
39Adui aliyepanda yale magugu ni Ibilisi. Mavuno ni mwisho wa nyakati na wavunaji ni malaika.
40As therefore the tares are gathered up and burned with fire; so shall it be in the end of the world.
40Kama vile magugu yanavyokusanywa kuchomwa moto, ndivyo itakavyokuwa mwishoni mwa nyakati;
41The Son of man shall send forth his angels, and they shall gather out of his kingdom all things that cause stumbling, and them that do iniquity,
41Mwana wa Mtu atawatuma malaika wake wawakusanye kutoka katika Ufalme wake wale wote wenye kusababisha dhambi, na wote wenye kutenda maovu,
42and shall cast them into the furnace of fire: there shall be the weeping and the gnashing of teeth.
42na kuwatupa katika tanuru ya moto, na huko watalia na kusaga meno.
43Then shall the righteous shine forth as the sun in the kingdom of their Father. He that hath ears, let him hear.
43Kisha, wale wema watang'ara kama jua katika Ufalme wa Baba yao. Sikieni basi, kama mna masikio!
44The kingdom of heaven is like unto a treasure hidden in the field; which a man found, and hid; and in his joy he goeth and selleth all that he hath, and buyeth that field.
44"Ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyofichika shambani. Mtu mmoja aliigundua, akaificha tena. Alifurahi sana hata akaenda kuuza yote aliyokuwa nayo, akalinunua shamba lile.
45Again, the kingdom of heaven is like unto a man that is a merchant seeking goodly pearls:
45"Tena, Ufalme wa mbinguni umefanana na mfanyabiashara mmoja mwenye kutafuta lulu nzuri.
46and having found one pearl of great price, he went and sold all that he had, and bought it.
46Alipopata lulu moja ya thamani kubwa, alienda akauza yote aliyokuwa nayo, akainunua lulu ile.
47Again, the kingdom of heaven is like unto a net, that was cast into the sea, and gathered of every kind:
47"Tena, Ufalme wa mbinguni unafanana na wavu uliotupwa baharini, ukanasa samaki wa kila aina.
48which, when it was filled, they drew up on the beach; and they sat down, and gathered the good into vessels, but the bad they cast away.
48Ulipojaa, watu waliuvuta pwani, wakaketi, wakachagua samaki wazuri wakawaweka ndani ya vikapu vyao, na wabaya wakawatupa.
49So shall it be in the end of the world: the angels shall come forth, and sever the wicked from among the righteous,
49Ndivyo itakavyokuwa mwishoni mwa nyakati: malaika watatokea, watawatenganisha watu wabaya na watu wema,
50and shall cast them into the furnace of fire: there shall be the weeping and the gnashing of teeth.
50na kuwatupa hao wabaya katika tanuru ya moto. Huko watalia na kusaga meno."
51Have ye understood all these things? They say unto him, Yea.
51Yesu akawauliza, "Je, mmeelewa mambo haya yote?" Wakamjibu, "Naam."
52And he said unto them, Therefore every scribe who hath been made a disciple to the kingdom of heaven is like unto a man that is a householder, who bringeth forth out of his treasure things new and old.
52Naye akawaambia, "Hivyo basi, kila mwalimu wa Sheria aliye mwanafunzi wa Ufalme wa mbinguni anafanana na mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale."
53And it came to pass, when Jesus had finished these parables, he departed thence.
53Yesu alipomaliza kusema mifano hiyo alitoka mahali hapo,
54And coming into his own country he taught them in their synagogue, insomuch that they were astonished, and said, Whence hath this man this wisdom, and these mighty works?
54akaenda kijijini kwake. Huko akawa anawafundisha watu katika sunagogi hata wakashangaa, wakasema, "Huyu amepata wapi hekima hii na maajabu?
55Is not this the carpenter's son? is not his mother called Mary? and his brethren, James, and Joseph, and Simon, and Judas?
55Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda?
56And his sisters, are they not all with us? Whence then hath this man all these things?
56Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?"
57And they were offended in him. But Jesus said unto them, A prophet is not without honor, save in his own country, and in his own house.
57Basi, wakawa na mashaka naye. Lakini Yesu akawaambia, "Nabii hakosi kuheshimiwa, isipokuwa katika nchi yake na nyumbani mwake!"
58And he did not many mighty works there because of their unbelief.
58Kwa hiyo, hakutenda miujiza mingi pale kwa sababu ya kutoamini kwao.