1The elder to [the] elect lady and her children, whom *I* love in truth, and not *I* only but also all who have known the truth,
1Mimi Mzee nakuandikia wewe Bimkubwa mteule, pamoja na watoto wako ninaowapenda kweli. Wala si mimi tu ninayewapenda, bali pia wote wanaoujua ule ukweli wanawapenda ninyi,
2for the truth's sake which abides in us and shall be with us to eternity.
2kwa sababu ukweli unakaa nasi milele.
3Grace shall be with you, mercy, peace from God [the] Father, and from [the] Lord Jesus Christ, the Son of the Father, in truth and love.
3Neema na huruma na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Yesu Kristo, Mwana wa Baba, zitakuwa pamoja nasi katika ukweli na upendo.
4I rejoiced greatly that I have found of thy children walking in truth, as we have received commandment from the Father.
4Nilifurahi sana kuona kwamba baadhi ya watoto wako wanaishi katika ukweli kama Baba alivyotuamuru.
5And now I beseech thee, lady, not as writing to thee a new commandment, but that which we have had from [the] beginning, that we should love one another.
5Basi, Bimkubwa, ninalo ombi moja kwako: tupendane. Ombi hili si amri mpya, bali ni amri ileile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo.
6And this is love, that we should walk according to his commandments. This is the commandment, according as ye have heard from the beginning, that ye might walk in it.
6Upendo maana yake ni kuishi kwa kuzitii amri zake Mungu. Amri niliyoisikia tangu mwanzo ndiyo hii: mnapaswa nyote kuishi katika upendo.
7For many deceivers have gone out into the world, they who do not confess Jesus Christ coming in flesh -- this is the deceiver and the antichrist.
7Wadanganyifu wengi wamezuka duniani, watu ambao hawakiri kwamba Yesu Kristo amekuja kwetu akawa binadamu. Mtu asemaye hivyo ni mdanganyifu na ni Adui wa Kristo.
8See to yourselves, that we may not lose what we have wrought, but may receive full wages.
8Basi, jihadharini ninyi wenyewe ili msije mkapoteza kile mlichokishugulikia, bali mpate tuzo lenu kamili.
9Whosoever goes forward and abides not in the doctrine of the Christ has not God. He that abides in the doctrine, *he* has both the Father and the Son.
9Asiyezingatia na kudumu katika mafundisho ya Kristo, bali anayakiuka, hana Mungu. Lakini anayedumu katika mafundisho hayo anaye Baba na Mwana.
10If any one come to you and bring not this doctrine, do not receive him into [the] house, and greet him not;
10Basi, kama mtu akija kwenu bila kuwaleteeni mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani kwenu, wala msimsalimu.
11for he who greets him partakes in his wicked works.
11Maana anayemsalimu mtu huyo, anashirikiana naye katika matendo yake maovu.
12Having many things to write to you, I would not with paper and ink; but hope to come to you, and to speak mouth to mouth, that our joy may be full.
12Ninayo mengi ya kuwaambieni lakini sipendi kufanya hivyo kwa karatasi na wino; badala yake, natumaini kuwatembeleeni na kuzungumza nanyi ana kwa ana, ili furaha yetu ikamilike.
13The children of thine elect sister greet thee.
13Watoto wa dada yako mteule wanakusalimu.