1Basi, ikiwa mmefufuka pamoja na Kristo, panieni mambo ya juu, kule Kristo aliko, ameketi upande wa kulia wa Mungu.
1If ye then be risen with Christ, seek those things which are above, where Christ sitteth on the right hand of God.
2Muwe na hamu ya mambo ya huko juu, na siyo mambo ya hapa duniani.
2Set your affection on things above, not on things on the earth.
3Maana ninyi mmekufa na uzima wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.
3For ye are dead, and your life is hid with Christ in God.
4Uzima wenu halisi ni Kristo, na wakati atakapotokea ndipo nanyi pia mtakapotokea pamoja naye katika utukufu.
4When Christ, who is our life, shall appear, then shall ye also appear with him in glory.
5Basi, komesheni kabisa kila kitu kilicho ndani yenu ambacho chahusika na mambo ya kidunia: uasherati, uchafu, shauku, tamaa mbaya na uchu (ambao ni sawa na kuabudu sanamu).
5Mortify therefore your members which are upon the earth; fornication, uncleanness, inordinate affection, evil concupiscence, and covetousness, which is idolatry:
6Kwa sababu ya mambo hayo hasira ya Mungu huwajia wote wanaomwasi.
6For which things' sake the wrath of God cometh on the children of disobedience:
7Wakati mmoja ninyi pia mliishi kufuatana na mambo hayo, mlipotawaliwa nayo.
7In the which ye also walked some time, when ye lived in them.
8Lakini sasa mnapaswa kuachana na mambo haya yote: hasira, tamaa, uovu; kufuru au maneno yasiyofaa yasitoke kamwe vinywani mwenu.
8But now ye also put off all these; anger, wrath, malice, blasphemy, filthy communication out of your mouth.
9Msiambiane uongo, kwani ninyi mmekwisha vua ule utu wa kale pamoja na matendo yake yote,
9Lie not one to another, seeing that ye have put off the old man with his deeds;
10mkavaa utu mpya. Huu unaendelea kurekebishwa na Mungu, Muumba wake, kadiri ya mfano wake, ili mpate kumjua Mungu kwa ukamilifu.
10And have put on the new man, which is renewed in knowledge after the image of him that created him:
11Katika hali hii, hakuna tena tofauti kati ya Mgiriki na Myahudi, aliyetahiriwa na asiyetahiriwa, msomi na asiye msomi, mtumwa na mtu aliye huru. Kristo ni kila kitu, na yumo katika yote.
11Where there is neither Greek nor Jew, circumcision nor uncircumcision, Barbarian, Scythian, bond nor free: but Christ is all, and in all.
12Ninyi ni watu wake Mungu; yeye aliwapenda na kuwateua. Kwa hiyo basi, vaeni moyo wa huruma, wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.
12Put on therefore, as the elect of God, holy and beloved, bowels of mercies, kindness, humbleness of mind, meekness, longsuffering;
13Vumilianeni na kusameheana iwapo mmoja wenu analo jambo lolote dhidi ya mwenzake. Mnapaswa kusameheana kama Bwana alivyowasamehe ninyi.
13Forbearing one another, and forgiving one another, if any man have a quarrel against any: even as Christ forgave you, so also do ye.
14Zaidi ya hayo yote, zingatieni upendo kwani upendo huunganisha kila kitu katika umoja ulio kamili.
14And above all these things put on charity, which is the bond of perfectness.
15Nayo amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu; maana kwa ajili hiyo ninyi mmeitwa katika mwili huo mmoja. Tena muwe na shukrani!
15And let the peace of God rule in your hearts, to the which also ye are called in one body; and be ye thankful.
16Ujumbe wa Kristo ukae ndani yenu pamoja na utajiri wake wote. Fundishaneni na kushauriana kwa hekima yote. Imbeni zaburi, nyimbo na tenzi za kiroho; mwimbieni Mungu mioyoni mwenu kwa shukrani.
16Let the word of Christ dwell in you richly in all wisdom; teaching and admonishing one another in psalms and hymns and spiritual songs, singing with grace in your hearts to the Lord.
17Na, kila mfanyacho kwa neno au tendo, fanyeni vyote kwa jina la Bwana Yesu na kumshukuru Mungu Baba kwa njia yake.
17And whatsoever ye do in word or deed, do all in the name of the Lord Jesus, giving thanks to God and the Father by him.
18Enyi akina mama, watiini waume zenu, kwani ndivyo apendavyo Bwana.
18Wives, submit yourselves unto your own husbands, as it is fit in the Lord.
19Nanyi waume, wapendeni wake zenu, na msiwe wakali kwao.
19Husbands, love your wives, and be not bitter against them.
20Enyi watoto, watiini wazazi wenu daima maana hiyo humpendeza Bwana.
20Children, obey your parents in all things: for this is well pleasing unto the Lord.
21Nanyi wazazi, msiwachukize watoto wenu, la sivyo watakata tamaa.
21Fathers, provoke not your children to anger, lest they be discouraged.
22Enyi watumwa, watiini wakuu wenu wa kidunia katika mambo yote, na si tu wakati wanapowatazama kwa kuwa mnataka kujipendekeza kwao; ila fanyeni hivyo kwa moyo wote, kwa sababu ya kumcha Bwana.
22Servants, obey in all things your masters according to the flesh; not with eyeservice, as menpleasers; but in singleness of heart, fearing God;
23Kila mfanyalo, fanyeni kwa moyo wote, kwa sababu ya Bwana na si kwa ajili ya mtu.
23And whatsoever ye do, do it heartily, as to the Lord, and not unto men;
24Kumbukeni kwamba atawapeni tuzo lile alilowawekea watu wake. Mtumikieni Kristo Bwana!
24Knowing that of the Lord ye shall receive the reward of the inheritance: for ye serve the Lord Christ.
25Atendaye mabaya atalipwa kufuatana na ubaya wake; Mungu hana ubaguzi.
25But he that doeth wrong shall receive for the wrong which he hath done: and there is no respect of persons.