Swahili: New Testament

King James Version

Galatians

1

1Mimi Paulo mtume,
1Paul, an apostle, (not of men, neither by man, but by Jesus Christ, and God the Father, who raised him from the dead;)
2na ndugu wote walio pamoja nami, tunayaandikia makanisa yaliyoko Galatia. Mimi nimepata kuwa mtume si kutokana na mamlaka ya binadamu, wala si kwa nguvu ya mtu, bali kwa uwezo wa Yesu Kristo na wa Mungu Baba aliyemfufua Yesu kutoka wafu.
2And all the brethren which are with me, unto the churches of Galatia:
3Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kutoka kwa Bwana Yesu Kristo.
3Grace be to you and peace from God the Father, and from our Lord Jesus Christ,
4Kristo alijitoa mwenyewe kwa ajili ya dhambi zetu kufuatana na mapenzi ya Mungu wetu na Baba, ili apate kutuokoa katika ulimwengu huu mbaya wa sasa.
4Who gave himself for our sins, that he might deliver us from this present evil world, according to the will of God and our Father:
5Kwake yeye uwe utukufu milele! Amina.
5To whom be glory for ever and ever. Amen.
6Nashangaa kwamba muda mfupi tu umepita, nanyi mnamwasi yule aliyewaita kwa neema ya Kristo, mkafuata Habari Njema ya namna nyingine.
6I marvel that ye are so soon removed from him that called you into the grace of Christ unto another gospel:
7Lakini hakuna "Habari Njema" nyingine. Ukweli ni kwamba wako watu wanaowavurugeni, watu wanaotaka kuipotosha Habari Njema ya Kristo.
7Which is not another; but there be some that trouble you, and would pervert the gospel of Christ.
8Lakini, hata kama mmoja wetu au malaika kutoka mbinguni, atawahubirieni Habari Njema tofauti na ile tuliyowahubirieni sisi, basi huyo na alaaniwe!
8But though we, or an angel from heaven, preach any other gospel unto you than that which we have preached unto you, let him be accursed.
9Tulikwisha sema, na sasa nasema tena: kama mtu yeyote anawahubirieni Habari Njema ya aina nyingine, tofauti na ile mliyokwisha pokea, huyo na alaaniwe!
9As we said before, so say I now again, if any man preach any other gospel unto you than that ye have received, let him be accursed.
10Sasa nataka kibali cha nani: cha binadamu, ama cha Mungu? Au je, nataka kuwapendeza watu? Kama ningefanya hivyo, mimi singekuwa kamwe mtumishi wa Kristo.
10For do I now persuade men, or God? or do I seek to please men? for if I yet pleased men, I should not be the servant of Christ.
11Ndugu, napenda mfahamu kwamba ile Habari Njema niliyoihubiri si ujumbe wa kibinadamu.
11But I certify you, brethren, that the gospel which was preached of me is not after man.
12Wala mimi sikuipokea kutoka kwa binadamu, wala sikufundishwa na mtu. Yesu Kristo mwenyewe ndiye aliyenifunulia.
12For I neither received it of man, neither was I taught it, but by the revelation of Jesus Christ.
13Bila shaka mlikwisha sikia jinsi nilivyokuwa ninaishi zamani kwa kuzingatia dini ya Kiyahudi, na jinsi nilivyolitesa kanisa la Mungu kupita kiasi na kutaka kuliharibu kabisa.
13For ye have heard of my conversation in time past in the Jews' religion, how that beyond measure I persecuted the church of God, and wasted it:
14Naam, mimi niliwashinda wengi wa wananchi wenzangu wa rika langu katika kuizingatia dini ya Kiyahudi, nikajitahidi sana kuyashika mapokeo ya wazee wetu.
14And profited in the Jews' religion above many my equals in mine own nation, being more exceedingly zealous of the traditions of my fathers.
15Lakini Mungu, kwa neema yake, alikuwa ameniteua hata kabla sijazaliwa, akaniita nimtumikie.
15But when it pleased God, who separated me from my mother's womb, and called me by his grace,
16Mara tu alipoamua kunifunulia Mwanae kusudi niihubiri Habari Njema yake kwa watu wa mataifa mengine, bila kutafuta maoni ya binadamu,
16To reveal his Son in me, that I might preach him among the heathen; immediately I conferred not with flesh and blood:
17na bila kwenda kwanza Yerusalemu kwa wale waliopata kuwa mitume kabla yangu, nilikwenda kwanza Arabia, kisha nikarudi tena Damasko.
17Neither went I up to Jerusalem to them which were apostles before me; but I went into Arabia, and returned again unto Damascus.
18Ilikuwa tu baada ya miaka mitatu, ndipo nilipokwenda Yerusalemu kuonana na Kefa; nilikaa kwake siku kumi na tano.
18Then after three years I went up to Jerusalem to see Peter, and abode with him fifteen days.
19Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana.
19But other of the apostles saw I none, save James the Lord's brother.
20Haya ninayowaandikieni, Mungu anajua; sisemi uongo.
20Now the things which I write unto you, behold, before God, I lie not.
21Baadaye nilikwenda katika tarafa za Siria na Kilikia.
21Afterwards I came into the regions of Syria and Cilicia;
22Wakati huo, mimi binafsi sikujulikana kwa jumuiya za Wakristo kule Yudea.
22And was unknown by face unto the churches of Judaea which were in Christ:
23Walichokuwa wanajua ni kile tu walichosikia: "Mtu yule aliyekuwa akitutesa hapo awali, sasa anaihubiri imani ileile aliyokuwa anajaribu kuiangamiza."
23But they had heard only, That he which persecuted us in times past now preacheth the faith which once he destroyed.
24Basi, wakamtukuza Mungu kwa sababu yangu.
24And they glorified God in me.