1Ndugu zangu, mkiwa mnamwamini Bwana Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwabague watu kamwe.
1My brethren, have not the faith of our Lord Jesus Christ, the Lord of glory, with respect of persons.
2Tuseme mtu mmoja ambaye amevaa pete ya dhahabu na mavazi nadhifu anaingia katika mkutano wenu, na papo hapo akaingia mtu maskini aliyevaa mavazi machafu.
2For if there come unto your assembly a man with a gold ring, in goodly apparel, and there come in also a poor man in vile raiment;
3Ikiwa mtamstahi zaidi yule aliyevaa mavazi ya kuvutia na kumwambia: "Keti hapa mahali pazuri," na kumwambia yule maskini: "Wewe, simama huko," au "Keti hapa sakafuni miguuni pangu,"
3And ye have respect to him that weareth the gay clothing, and say unto him, Sit thou here in a good place; and say to the poor, Stand thou there, or sit here under my footstool:
4je, huo si ubaguzi kati yenu? Je, na huo uamuzi wenu haujatokana na fikira mbaya?
4Are ye not then partial in yourselves, and are become judges of evil thoughts?
5Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni! Mungu amechagua watu ambao ni maskini katika ulimwengu huu ili wapate kuwa matajiri katika imani na kupokea Utawala aliowaahidia wale wanaompenda.
5Hearken, my beloved brethren, Hath not God chosen the poor of this world rich in faith, and heirs of the kingdom which he hath promised to them that love him?
6Lakini ninyi mnawadharau watu maskini! Je, matajiri si ndio wanaowakandamizeni na kuwapeleka mahakamani?
6But ye have despised the poor. Do not rich men oppress you, and draw you before the judgment seats?
7Je, si haohao wanaolitukana hilo jina lenu zuri mlilopewa?
7Do not they blaspheme that worthy name by the which ye are called?
8Kama mnaitimiza ile sheria ya Utawala kama ilivyoandikwa katika Maandiko Matakatifu: "Mpende binadamu mwenzako kama unavyojipenda wewe mwenyewe", mtakuwa mnafanya vema kabisa.
8If ye fulfil the royal law according to the scripture, Thou shalt love thy neighbour as thyself, ye do well:
9Lakini mkiwabagua watu, basi, mwatenda dhambi, nayo Sheria inawahukumu ninyi kuwa mna hatia.
9But if ye have respect to persons, ye commit sin, and are convinced of the law as transgressors.
10Anayevunja amri mojawapo ya Sheria, atakuwa na hatia ya kuivunja Sheria yote.
10For whosoever shall keep the whole law, and yet offend in one point, he is guilty of all.
11Maana yuleyule aliyesema: "Usizini," alisema pia "Usiue". Kwa hiyo, hata ikiwa hukuzini lakini umeua, wewe umeivunja Sheria.
11For he that said, Do not commit adultery, said also, Do not kill. Now if thou commit no adultery, yet if thou kill, thou art become a transgressor of the law.
12Basi, semeni na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria iletayo uhuru.
12So speak ye, and so do, as they that shall be judged by the law of liberty.
13Maana, Mungu hatakuwa na huruma atakapomhukumu mtu asiyekuwa na huruma. Lakini huruma hushinda hukumu.
13For he shall have judgment without mercy, that hath shewed no mercy; and mercy rejoiceth against judgment.
14Ndugu zangu, kuna faida gani mtu kusema ana imani, lakini haonyeshi kwa vitendo? Je, hiyo imani yawezaje kumwokoa?
14What doth it profit, my brethren, though a man say he hath faith, and have not works? can faith save him?
15Tuseme kaka au dada hana nguo au chakula.
15If a brother or sister be naked, and destitute of daily food,
16Yafaa kitu gani ninyi kuwaambia hao: "Nendeni salama mkaote moto na kushiba," bila kuwapatia mahitaji yao ya maisha?
16And one of you say unto them, Depart in peace, be ye warmed and filled; notwithstanding ye give them not those things which are needful to the body; what doth it profit?
17Vivyo hivyo, imani peke yake bila matendo imekufa.
17Even so faith, if it hath not works, is dead, being alone.
18Lakini mtu anaweza kusema: "Wewe unayo imani, mimi ninayo matendo!" Haya! Nionyeshe jinsi mtu anavyoweza kuwa na imani bila matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa matendo yangu.
18Yea, a man may say, Thou hast faith, and I have works: shew me thy faith without thy works, and I will shew thee my faith by my works.
19Je, wewe unaamini kwamba yuko Mungu mmoja? Sawa! Lakini hata pepo huamini hilo, na hutetemeka kwa hofu.
19Thou believest that there is one God; thou doest well: the devils also believe, and tremble.
20Mpumbavu wee! Je, wataka kuonyeshwa kwamba imani bila matendo imekufa?
20But wilt thou know, O vain man, that faith without works is dead?
21Je, Abrahamu baba yetu alipataje kukubalika mbele yake Mungu? Kwa matendo yake, wakati alipomtoa mwanae Isaka sadaka juu ya madhabahu.
21Was not Abraham our father justified by works, when he had offered Isaac his son upon the altar?
22Waona basi, kwamba imani yake iliandamana na matendo yake; imani yake ilikamilishwa kwa matendo yake.
22Seest thou how faith wrought with his works, and by works was faith made perfect?
23Hivyo yakatimia yale Maandiko Matakatifu yasemayo: "Abrahamu alimwamini Mungu na kwa imani yake akakubaliwa kuwa mtu mwadilifu; na hivyo Abrahamu akaitwa rafiki wa Mungu."
23And the scripture was fulfilled which saith, Abraham believed God, and it was imputed unto him for righteousness: and he was called the Friend of God.
24Mnaona basi, kwamba mtu hukubaliwa kuwa mwadilifu kwa matendo yake na si kwa imani peke yake.
24Ye see then how that by works a man is justified, and not by faith only.
25Ilikuwa vivyo hivyo kuhusu yule malaya Rahabu; yeye alikubaliwa kuwa mwadilifu kwa sababu aliwapokea wale wapelelezi na kuwasaidia waende zao kwa kupitia njia nyingine.
25Likewise also was not Rahab the harlot justified by works, when she had received the messengers, and had sent them out another way?
26Basi, kama vile mwili bila roho umekufa, vivyo hivyo imani bila matendo imekufa.
26For as the body without the spirit is dead, so faith without works is dead also.