1Siku moja ya Sabato, Yesu alikwenda kula chakula nyumbani kwa mmoja wa viongozi wa Mafarisayo; watu waliokuwapo hapo wakawa wanamchunguza.
1And it came to pass, on his going into the house of a certain one of the chiefs of the Pharisees, on a sabbath, to eat bread, that they were watching him,
2Mbele yake Yesu palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa na ugonjwa wa kuvimba mwili.
2and lo, there was a certain dropsical man before him;
3Yesu akawauliza walimu wa Sheria na Mafarisayo, "Je, ni halali au la kumponya mtu siku ya sabato?"
3and Jesus answering spake to the lawyers and Pharisees, saying, `Is it lawful on the sabbath-day to heal?`
4Lakini wao wakakaa kimya. Yesu akamshika huyo mgonjwa, akamponya, akamwacha aende zake.
4and they were silent, and having taken hold of [him], he healed him, and let [him] go;
5Halafu akawaambia, "Ni nani kati yenu ambaye mtoto wake au ng'ombe wake akitumbukia shimoni, hangemtoa hata kama ni siku ya Sabato?"
5and answering them he said, `Of which of you shall an ass or ox fall into a pit, and he will not immediately draw it up on the sabbath-day?`
6Nao hawakuweza kumjibu swali hilo.
6and they were not able to answer him again unto these things.
7Yesu aliona jinsi wale walioalikwa walivyokuwa wanajichagulia nafasi za heshima, akawaambia mfano:
7And he spake a simile unto those called, marking how they were choosing out the first couches, saying unto them,
8"Kama mtu akikualika arusini, usiketi mahali pa heshima isije ikawa amealikwa mwingine mheshimiwa kuliko wewe;
8`When thou mayest be called by any one to marriage-feasts, thou mayest not recline on the first couch, lest a more honourable than thou may have been called by him,
9na mwenyeji wenu ninyi wawili atakuja na kukwambia: Mwachie huyu nafasi. Hapo utaaibika mbele ya wote na kulazimika kwenda kuchukua nafasi ya mwisho.
9and he who did call thee and him having come shall say to thee, Give to this one place, and then thou mayest begin with shame to occupy the last place.
10Bali ukialikwa kwenye karamu, keti mahali pa mwisho, ili mwenyeji wako atakapokuja akwambie: Rafiki, njoo hapa mbele, mahali pazuri zaidi. Hapo utakuwa umeheshimika mbele ya wote wanaoketi pamoja nawe.
10`But, when thou mayest be called, having gone on, recline in the last place, that when he who called thee may come, he may say to thee, Friend, come up higher; then thou shalt have glory before those reclining with thee;
11Kwa maana yeyote anayejikweza atashushwa, na anayejishusha, atakwezwa."
11because every one who is exalting himself shall be humbled, and he who is humbling himself shall be exalted.`
12Halafu akamwambia na yule aliyemwalika, "Kama ukiwaandalia watu karamu mchana au jioni, usiwaalike rafiki zako au jamaa zako au jirani zako walio matajiri, wasije nao wakakualika nawe ukawa umelipwa kile ulichowatendea.
12And he said also to him who did call him, `When thou mayest make a dinner or a supper, be not calling thy friends, nor thy brethren, nor thy kindred, nor rich neighbours, lest they may also call thee again, and a recompense may come to thee;
13Badala yake, unapofanya karamu, waalike maskini, vilema viwete na vipofu,
13but when thou mayest make a feast, be calling poor, maimed, lame, blind,
14nawe utakuwa umepata baraka, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa. Maana Mungu atakupa tuzo lako wakati watu wema watakapofufuka."
14and happy thou shalt be, because they have not to recompense thee, for it shall be recompensed to thee in the rising again of the righteous.`
15Mmoja wa wale waliokuwa wameketi pamoja na Yesu akasema, "Ana heri mtu yule atakayekula chakula katika Ufalme wa Mungu."
15And one of those reclining with him, having heard these things, said to him, `Happy [is] he who shall eat bread in the reign of God;`
16Yesu akamjibu, "Mtu mmoja alifanya karamu kubwa, akaalika watu wengi.
16and he said to him, `A certain man made a great supper, and called many,
17Wakati wa karamu ulipofika alimtuma mtumishi wake awaambie walioalikwa, Njoni, kila kitu ni tayari.
17and he sent his servant at the hour of the supper to say to those having been called, Be coming, because now are all things ready.
18Lakini wote, kwa namna moja, wakaanza kuomba radhi. Wa kwanza akamwambia mtumishi: Nimenunua shamba, kwa hiyo sina budi kwenda kuliangalia; nakuomba uniwie radhi.
18`And they began with one consent all to excuse themselves: The first said to him, A field I bought, and I have need to go forth and see it; I beg of thee, have me excused.
19Mwingine akasema: Nimenunua ng'ombe jozi tano wa kulima; sasa nimo njiani kwenda kuwajaribu; nakuomba uniwie radhi.
19`And another said, Five yoke of oxen I bought, and I go on to prove them; I beg of thee, have me excused:
20Na mwingine akasema: Nimeoa mke, kwa hiyo siwezi kuja.
20and another said, A wife I married, and because of this I am not able to come.
21Mtumishi huyo akarudi na kumwarifu bwana wake jambo hilo. Yule mwenye nyumba alikasirika, akamwambia mtumishi wake: Nenda upesi kwenye barabara na vichochoro vya mji, uwalete hapa ndani maskini, viwete, vipofu na waliolemaa.
21`And that servant having come, told to his lord these things, then the master of the house, having been angry, said to his servant, Go forth quickly to the broad places and lanes of the city, and the poor, and maimed, and lame, and blind, bring in hither.
22Baadaye, mtumishi huyo akasema: Bwana mambo yamefanyika kama ulivyoamuru, lakini bado iko nafasi.
22`And the servant said, Sir, it hath been done as thou didst command, and still there is room.
23Yule bwana akamwambia mtumishi: Nenda katika barabara na vichochoro vya mji uwashurutishe watu kuingia ili nyumba yangu ijae.
23`And the lord said unto the servant, Go forth to the ways and hedges, and constrain to come in, that my house may be filled;
24Kwa maana, nawaambieni, hakuna hata mmoja wa wale walioalikwa atakayeonja karamu yangu."
24for I say to you, that none of those men who have been called shall taste of my supper.`
25Hapo, makundi mengi yakawa yanaandamana pamoja na Yesu. Basi, akawageukia akawaambia,
25And there were going on with him great multitudes, and having turned, he said unto them,
26"Mtu yeyote akija kwangu, asipowachukia baba na mama yake, mke wake, watoto, ndugu na dada zake, naam, hata na nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
26`If any one doth come unto me, and doth not hate his own father, and mother, and wife, and children, and brothers, and sisters, and yet even his own life, he is not able to be my disciple;
27Mtu asipochukua msalaba wake na kunifuata hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
27and whoever doth not bear his cross, and come after me, is not able to be my disciple.
28Kwa maana, ni nani miongoni mwenu ambaye akitaka kujenga mnara hataketi kwanza akadirie gharama zake ili ajue kama ana kiasi cha kutosha cha kumalizia?
28`For who of you, willing to build a tower, doth not first, having sat down, count the expense, whether he have the things for completing?
29La sivyo, baada ya kuweka msingi na kushindwa kumaliza, watu watamcheka
29lest that he having laid a foundation, and not being able to finish, all who are beholding may begin to mock him,
30wakisema: Mtu huyu alianza kujenga, lakini hakumalizia.
30saying — This man began to build, and was not able to finish.
31"Au, ni mfalme gani ambaye, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, hataketi kwanza chini na kufikiri kama ataweza, kwa askari wake elfu ishirini?
31`Or what king going on to engage with another king in war, doth not, having sat down, first consult if he be able with ten thousand to meet him who with twenty thousand is coming against him?
32Kama anaona hataweza, atawatuma wajumbe kutaka masharti ya amani wakati mfalme huyo mwingine angali mbali.
32and if not so — he being yet a long way off — having sent an embassy, he doth ask the things for peace.
33Vivyo hivyo, basi, hakuna hata mmoja wenu atakayekuwa mwanafunzi wangu kama asipoachilia kila kitu alicho nacho.
33`So, then, every one of you who doth not take leave of all that he himself hath, is not able to be my disciple.
34"Chumvi ni nzuri; lakini ikipoteza ladha yake, itakolezwa na nini?
34`The salt [is] good, but if the salt doth become tasteless, with what shall it be seasoned?
35Haifai kitu wala kwa udongo wala kwa mbolea. Watu huitupilia mbali. Sikieni basi, kama mna masikio!"
35neither for land nor for manure is it fit — they cast it without. He who is having ears to hear — let him hear.`