1Yesu aliingia tena katika sunagogi na mle ndani mlikuwa na mtu aliyekuwa na mkono uliopooza.
1And he entered again into the synagogue, and there was there a man having the hand withered,
2Humo baadhi ya watu walimngojea amponye mtu huyo siku ya sabato ili wapate kumshtaki.
2and they were watching him, whether on the sabbaths he will heal him, that they might accuse him.
3Yesu akamwambia huyo mtu aliyekuwa na mkono uliopooza, "Njoo hapa katikati."
3And he saith to the man having the hand withered, `Rise up in the midst.`
4Kisha, akawauliza, "Je, ni halali siku ya Sabato kutenda jambo jema au kutenda jambo baya; kuokoa maisha au kuua?" Lakini wao hawakusema neno.
4And he saith to them, `Is it lawful on the sabbaths to do good, or to do evil? life to save, or to kill?` but they were silent.
5Hapo akawatazama wote kwa hasira, akaona huzuni kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. Kisha akamwambia huyo mtu, "Nyosha mkono wako!" Naye akaunyosha mkono wake, ukawa mzima tena.
5And having looked round upon them with anger, being grieved for the hardness of their heart, he saith to the man, `Stretch forth thy hand;` and he stretched forth, and his hand was restored whole as the other;
6Mara Mafarisayo wakatoka nje, wakafanya shauri pamoja na watu wa kikundi cha Herode jinsi ya kumwangamiza Yesu.
6and the Pharisees having gone forth, immediately, with the Herodians, were taking counsel against him how they might destroy him.
7Yesu aliondoka hapo pamoja na wanafunzi wake, akaenda kando ya ziwa, na umati wa watu ukamfuata. Watu hao walikuwa wametoka Yerusalemu, Yudea,
7And Jesus withdrew with his disciples unto the sea, and a great multitude from Galilee followed him, and from Judea,
8Idumea, ng'ambo ya mto Yordani, Tiro na Sidoni. Watu hao wengi walimwendea Yesu kwa sababu ya kusikia mambo mengi aliyokuwa ameyatenda.
8and from Jerusalem, and from Idumea and beyond the Jordan; and they about Tyre and Sidon — a great multitude — having heard how great things he was doing, came unto him.
9Yesu akawaambia wanafunzi wake wamtayarishie mashua moja, ili umati wa watu usije ukamsonga.
9And he said to his disciples that a little boat may wait on him, because of the multitude, that they may not press upon him,
10Alikuwa amewaponya watu wengi, na wagonjwa wote wakawa wanamsonga ili wapate kumgusa.
10for he did heal many, so that they threw themselves on him, in order to touch him — as many as had plagues;
11Na watu waliokuwa wamepagawa na pepo wachafu walipomwona, walijitupa chini mbele yake na kupaaza sauti, "Wewe ni Mwana wa Mungu!"
11and the unclean spirits, when they were seeing him, were falling down before him, and were crying, saying — `Thou art the Son of God;`
12Lakini Yesu akawaamuru kwa ukali wasimjulishe kwa watu.
12and many times he was charging them that they might not make him manifest.
13Yesu alipanda kilimani, akawaita wale aliowataka. Basi, wakamwendea,
13And he goeth up to the mountain, and doth call near whom he willed, and they went away to him;
14naye akawateua watu kumi na wawili ambao aliwaita mitume, wakae naye, awatume kuhubiri
14and he appointed twelve, that they may be with him, and that he may send them forth to preach,
15na wawe na mamlaka ya kuwafukuza pepo.
15and to have power to heal the sicknesses, and to cast out the demons.
16Basi, hao kumi na wawili walioteuliwa ndio hawa: Simoni (ambaye Yesu alimpa jina, Petro),
16And he put on Simon the name Peter;
17Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo (Yesu aliwapa hawa ndugu wawili jina Boanerge, maana yake "wanangurumo"),
17and James of Zebedee, and John the brother of James, and he put on them names — Boanerges, that is, `Sons of thunder;`
18Andrea na Filipo, Batholomayo, Mathayo, Thoma, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkanani na
18and Andrew, and Philip, and Bartholomew, and Matthew, and Thomas, and James of Alpheus, and Thaddeus, and Simon the Cananite,
19Yuda Iskarioti ambaye alimsaliti Yesu.
19and Judas Iscariot, who did also deliver him up; and they come into a house.
20Kisha Yesu alikwenda nyumbani. Umati wa watu ukakusanyika tena, hata Yesu na wafuasi wake wasiweze kupata nafasi ya kula chakula.
20And come together again doth a multitude, so that they are not able even to eat bread;
21Basi, watu wa jamaa yake walipopata habari hiyo wakatoka kwenda kumchukua maana walikuwa wanasema kwamba amepatwa na wazimu.
21and his friends having heard, went forth to lay hold on him, for they said that he was beside himself,
22Nao walimu wa Sheria waliokuwa wametoka Yerusalemu, wakasema, "Ana Beelzebuli! Tena, anawafukuza pepo kwa nguvu ya mkuu wa pepo."
22and the scribes who [are] from Jerusalem having come down, said — `He hath Beelzeboul,` and — `By the ruler of the demons he doth cast out the demons.`
23Hapo Yesu akawaita, akawaambia kwa mifano, "Shetani anawezaje kumfukuza Shetani?
23And, having called them near, in similes he said to them, `How is the Adversary able to cast out the Adversary?
24Ikiwa utawala mmoja umegawanyika makundimakundi yanayopigana, utawala huo hauwezi kudumu.
24and if a kingdom against itself be divided, that kingdom cannot be made to stand;
25Tena, ikiwa jamaa moja imegawanyika makundimakundi yanayopingana, jamaa hiyo itaangamia.
25and if a house against itself be divided, that house cannot be made to stand;
26Ikiwa basi, utawala wa Shetani umegawanyika vikundivikundi hauwezi kudumu, bali utaangamia kabisa.
26and if the Adversary did rise against himself, and hath been divided, he cannot be made to stand, but hath an end.
27"Hakuna mtu awezaye kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kumnyang'anya mali yake, isipokuwa kwanza amemfunga huyo mtu mwenye nguvu; hapo ndipo atakapoweza kumnyang'anya mali yake.
27`No one is able the vessels of the strong man — having entered into his house — to spoil, if first he may not bind the strong man, and then his house he will spoil.
28"Kweli nawaambieni, watu watasamehewa dhambi zao zote na kufuru zao zote;
28`Verily I say to you, that all the sins shall be forgiven to the sons of men, and evil speakings with which they might speak evil,
29lakini anayesema mabaya dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa kamwe; ana hatia ya dhambi ya milele."
29but whoever may speak evil in regard to the Holy Spirit hath not forgiveness — to the age, but is in danger of age-during judgment;`
30(Yesu alisema hivyo kwa sababu walikuwa wanasema, "Ana pepo mchafu.")
30because they said, `He hath an unclean spirit.`
31Mama yake Yesu na ndugu zake walifika hapo, wakasimama nje, wakampelekea ujumbe kutaka kumwona.
31Then come do his brethren and mother, and standing without, they sent unto him, calling him,
32Umati wa watu ulikuwa umekaa hapo kumzunguka. Basi, wakamwambia, "Mama yako na ndugu zako wako nje, wanataka kukuona."
32and a multitude was sitting about him, and they said to him, `Lo, thy mother and thy brethren without do seek thee.`
33Yesu akawaambia, "Mama yangu na ndugu zangu ni kina nani?"
33And he answered them, saying, `Who is my mother, or my brethren?`
34Hapo akawatazama watu waliokuwa wamemzunguka, akasema, "Tazameni! Hawa ndio mama yangu na ndugu zangu.
34And having looked round in a circle to those sitting about him, he saith, `Lo, my mother and my brethren!
35Mtu yeyote anayefanya anayotaka Mungu, huyo ndiye kaka yangu, dada yangu na mama yangu."
35for whoever may do the will of God, he is my brother, and my sister, and mother.`