1Siku moja, Yesu alipokuwa akiwafundisha watu Hekaluni na kuwahubiria juu ya Habari Njema, makuhani wakuu na walimu wa Sheria pamoja na wazee walifika,
1وفي احدى تلك الايام اذ كان يعلّم الشعب في الهيكل ويبشر وقف رؤساء الكهنة والكتبة مع الشيوخ
2wakasema, "Tuambie! Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani?"
2وكلموه قائلين قل لنا باي سلطان تفعل هذا. او من هو الذي اعطاك هذا السلطان.
3Yesu akawaambia, "Na mimi nitawaulizeni swali:
3فاجاب وقال لهم وانا ايضا اسألكم كلمة واحدة فقولوا لي.
4mamlaka ya Yohane ya kubatiza yalitoka kwa Mungu au kwa watu?"
4معمودية يوحنا من السماء كانت ام من الناس.
5Lakini wao wakajadiliana hivi: "Tukisema yalitoka mbinguni, yeye atatuuliza: Mbona hamkumsadiki?
5فتآمروا فيما بينهم قائلين ان قلنا من السماء يقول فلماذا لم تؤمنوا به.
6Na tukisema yalitoka kwa binadamu, watu wote hapa watatupiga mawe, maana wote wanaamini kwamba Yohane alikuwa nabii."
6وان قلنا من الناس فجميع الشعب يرجموننا لانهم واثقون بان يوحنا نبي.
7Basi, wakamwambia, "Hatujui mamlaka hayo yalitoka wapi."
7فاجابوا انهم لا يعلمون من اين.
8Yesu akawaambia, "Hata mimi sitawaambia ninafanya mambo haya kwa mamlaka gani."
8فقال لهم يسوع ولا انا اقول لكم باي سلطان افعل هذا
9Yesu akaendelea kuwaambia watu mfano huu: "Mtu mmoja alilima shamba la mizabibu, akalikodisha kwa wakulima; kisha akasafiri hadi nchi ya mbali, akakaa huko kwa muda mrefu.
9وابتدأ يقول للشعب هذا المثل. انسان غرس كرما وسلمه الى كرامين وسافر زمانا طويلا.
10Wakati wa mavuno, mtu huyo alimtuma mtumishi wake kwa wale wakulima, akachukue sehemu ya matunda ya shamba la mizabibu. Lakini wale wakulima wakampiga mtumishi huyo wakamrudisha mikono mitupu.
10وفي الوقت ارسل الى الكرامين عبدا لكي يعطوه من ثمر الكرم. فجلده الكرامون وارسلوه فارغا.
11Yule bwana akamtuma tena mtumishi mwingine; lakini wao wakampiga huyo vilevile na kumtendea vibaya, wakamrudisha mikono mitupu.
11فعاد وارسل عبدا آخر. فجلدوا ذلك ايضا واهانوه وارسلوه فارغا.
12Akamtuma tena wa tatu; huyu naye, baada ya kumwumiza, wakamfukuza.
12ثم عاد فارسل ثالثا. فجرحوا هذا ايضا واخرجوه.
13Yule mwenye shamba akafikiri: Nitafanya nini? Nitamtuma mwanangu mpenzi; labda watamjali yeye.
13فقال صاحب الكرم ماذا افعل. أرسل ابني الحبيب. لعلهم اذا رأوه يهابون.
14Wale wakulima walipomwona tu, wakasemezana: Huyu ndiye mrithi. Basi, tumwue ili urithi wake uwe wetu.
14فلما رآه الكرامون تآمروا فيما بينهم قائلين هذا هو الوارث. هلموا نقتله لكي يصير لنا الميراث.
15Basi, wakamtoa nje ya lile shamba la mizabibu, wakamwua." Yesu akauliza, "Yule mwenye shamba atawafanya nini hao wakulima?
15فاخرجوه خارج الكرم وقتلوه. فماذا يفعل بهم صاحب الكرم.
16Atakuja kuwaangamiza wakulima hao, na atawapa wakulima wengine hilo shamba la mizabibu." Watu waliposikia maneno hayo, walisema: "Hasha! Yasitukie hata kidogo!"
16يأتي ويهلك هؤلاء الكرامين ويعطي الكرم لآخرين. فلما سمعوا قالوا حاشا.
17Lakini Yesu akawatazama, akawaambia, "Maandiko haya Matakatifu yana maana gani basi? Jiwe walilokataa waashi, sasa limekuwa jiwe kuu la msingi!
17فنظر اليهم وقال اذا ما هو هذا المكتوب الحجر الذي رفضه البناؤون هو قد صار راس الزاوية.
18Mtu yeyote akianguka juu ya jiwe hilo, atavunjika vipandevipande; na likimwangukia mtu yeyote, litamsaga kabisa."
18كل من يسقط على ذلك الحجر يترضض. ومن سقط هو عليه يسحقه.
19Walimu wa Sheria na makuhani wakuu walifahamu kwamba mfano huo ulikuwa unawahusu, na hivyo walitaka kumkamata palepale, ila tu waliogopa watu.
19فطلب رؤساء الكهنة والكتبة ان يلقوا الايادي عليه في تلك الساعة ولكنهم خافوا الشعب. لانهم عرفوا انه قال هذا المثل عليهم
20Basi, wakawa wanatafuta wakati wa kufaa. Wakawahonga watu fulani wajisingizie kuwa wema, wakawatuma wamnase Yesu kwa maswali, na hivyo waweze kumtia nguvuni na kumpeleka kwa wakuu wa serikali.
20فراقبوه وارسلوا جواسيس يتراءون انهم ابرار لكي يمسكوه بكلمة حتى يسلموه الى حكم الوالي وسلطانه.
21Hao wapelelezi wakamwambia, "Mwalimu, tunajua kwamba unasema na kufundisha mambo ya kweli; tunajua kwamba wewe huna ubaguzi; wewe wafundisha ukweli juu ya njia ya Mungu.
21فسألوه قائلين يا معلّم نعلم انك بالاستقامة تتكلم وتعلّم ولا تقبل الوجوه بل بالحق تعلّم طريق الله.
22Basi, twambie kama ni halali, au la, kulipa kodi kwa Kaisari!"
22أيجوز لنا ان نعطي جزية لقيصر ام لا.
23Yesu alitambua mtego wao, akawaambia,
23فشعر بمكرهم وقال لهم لماذا تجربونني.
24"Nionyesheni sarafu. Je, sura na chapa ni vya nani?"
24أروني دينارا. لمن الصورة والكتابة. فاجابوا وقالوا لقيصر.
25Nao wakamjibu, "Ni vya Kaisari." Yesu akawaambia, "Basi, mpeni Kaisari vilivyo vyake Kaisari, na Mungu vilivyo vyake Mungu."
25فقال لهم اعطوا اذا ما لقيصر لقيصر وما للّه للّه.
26Hawakufaulu kumnasa kwa neno lolote pale mbele ya watu na hivyo wakakaa kimya wakilistaajabia jibu lake.
26فلم يقدروا ان يمسكوه بكلمة قدام الشعب. وتعجبوا من جوابه وسكتوا
27Kisha Masadukayo, ambao husema kwamba wafu hawafufuki, wakamjia Yesu, wakasema:
27وحضر قوم من الصدوقيين الذين يقاومون امر القيامة وسألوه
28"Mwalimu, Mose alituandikia kwamba kama ndugu ya mtu fulani akifa na kumwacha mjane wake bila watoto, ni lazima ndugu yake amchukue huyo mama mjane, amzalie watoto ndugu yake marehemu.
28قائلين يا معلّم كتب لنا موسى ان مات لاحد اخ وله امرأة ومات بغير ولد يأخذ اخوه المرأة ويقيم نسلا لاخيه.
29Sasa, wakati mmoja kulikuwa na ndugu saba. Yule wa kwanza alioa na baadaye akafa bila kuacha mtoto.
29فكان سبعة اخوة. واخذ الاول امرأة ومات بغير ولد.
30Yule ndugu wa pili akamwoa yule mjane, naye pia, akafa;
30فأخذ الثاني المرأة ومات بغير ولد.
31na ndugu wa tatu vilevile. Mambo yakawa yaleyale kwa wote saba--wote walikufa bila kuacha watoto.
31ثم اخذها الثالث وهكذا السبعة. ولم يتركوا ولدا وماتوا.
32Mwishowe akafa pia yule mwanamke.
32وآخر الكل ماتت المرأة ايضا.
33Je, siku wafu watakapofufuliwa, mwanamke huyo atakuwa mke wa nani? Alikuwa ameolewa na wote saba."
33ففي القيامة لمن منهم تكون زوجة. لانها كانت زوجة للسبعة.
34Yesu akawaambia, "Watu wa nyakati hizi huoa na kuolewa;
34فاجاب وقال لهم يسوع ابناء هذا الدهر يزوجون ويزوجون.
35lakini wale ambao Mungu atawawezesha kushiriki ule wakati wa ufufuo, hawataoa wala kuolewa.
35ولكن الذين حسبوا اهلا للحصول على ذلك الدهر والقيامة من الاموات لا يزوجون ولا يزوجون.
36Ama hakika, hawawezi kufa tena, kwa sababu watakuwa kama malaika, na ni watoto wa Mungu kwa vile wamefufuliwa katika wafu.
36اذ لا يستطيعون ان يموتوا ايضا لانهم مثل الملائكة وهم ابناء الله اذ هم ابناء القيامة.
37Lakini, kwamba kuna kufufuka kutoka wafu, hata Mose alithibitisha jambo hilo katika Maandiko Matakatifu. Katika sehemu ya Maandiko Matakatifu juu ya kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto, anamtaja Bwana kama Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo.
37واما ان الموتى يقومون فقد دل عليه موسى ايضا في امر العليقة كما يقول. الرب اله ابراهيم واله اسحق واله يعقوب.
38Basi, yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa wale walio hai; maana wale aliowaita kwake, wanaishi naye."
38وليس هو اله اموات بل اله احياء لان الجميع عنده احياء.
39Baadhi ya wale walimu wa Sheria wakasema, "Mwalimu, umejibu vema kabisa."
39فاجاب قوما من الكتبة وقالوا يا معلّم حسنا قلت.
40Walisema hivyo kwa sababu hawakuthubutu kumwuliza tena maswali mengine.
40ولم يتجاسروا ايضا ان يسألوه عن شيء
41Yesu akawauliza, "Yasemekanaje kwamba Kristo ni mwana wa Daudi?
41وقال لهم كيف يقولون ان المسيح ابن داود.
42Maana Daudi mwenyewe anasema katika Zaburi: Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti upande wangu wa kulia
42وداود نفسه يقول في كتاب المزامير قال الرب لربي اجلس عن يميني
43mpaka niwafanye adui zako kama kiti cha kuwekea miguu yako.
43حتى اضع اعداءك موطئا لقدميك.
44Ikiwa Daudi anamwita yeye, Bwana, basi atakuwaje mwanawe?"
44فاذا داود يدعوه ربا فكيف يكون ابنه
45Yesu aliwaambia wanafunzi wake mbele ya watu wote,
45وفيما كان جميع الشعب يسمعون قال لتلاميذه
46"Jihadharini na walimu wa Sheria ambao hupenda kupitapita wamevalia kanzu. Hupenda kusalimiwa na watu kwa heshima masokoni, huketi mahali pa heshima katika masunagogi na kuchukua nafasi za heshima katika karamu.
46احذروا من الكتبة الذين يرغبون المشي بالطيالسة ويحبون التحيات في الاسواق والمجالس الاولى في المجامع والمتكآت الأولى في الولائم.
47Huwadhulumu wajane huku wakisingizia kuwa wema kwa kusali sala ndefu. Hao watapata hukumu kali zaidi!"
47الذين يأكلون بيوت الارامل ولعلة يطيلون الصلوات. هؤلاء يأخذون دينونة اعظم