1Usimkemee mtu mzee, bali msihi kama vile angekuwa baba yako. Watendee vijana kama ndugu zako,
1Rebuke not an elder, but exhort him as a father; the younger men as brethren:
2wanawake wazee kama mama yako, na wasichana kama dada zako, kwa usafi wote.
2the elder women as mothers; the younger as sisters, in all purity.
3Waheshimu wanawake wajane walio wajane kweli.
3Honor widows that are widows indeed.
4Lakini mjane aliye na watoto au wajukuu, hao wanapaswa kujifunza kutimiza wajibu wao wa kidini kwa jamaa zao wenyewe na hivyo kuwalipa wazazi wao na wazee wao, kwani hilo ni jambo la kupendeza mbele ya Mungu.
4But if any widow hath children or grandchildren, let them learn first to show piety towards their own family, and to requite their parents: for this is acceptable in the sight of God.
5Mwanamke mjane kweli, asiye na mtu wa kumsaidia, amemwekea Mungu tumaini lake na huendelea kusali na kumwomba msaada usiku na mchana.
5Now she that is a widow indeed, and desolate, hath her hope set on God, and continueth in supplications and prayers night and day.
6Lakini mwanamke ambaye huishi maisha ya anasa, huyo amekufa, ingawa yu hai.
6But she that giveth herself to pleasure is dead while she liveth.
7Wape maagizo haya, wasije wakawa na lawama.
7These things also command, that they may be without reproach.
8Lakini kama mtu hawatunzi watu wa jamaa yake, hasa wale wa nyumbani kwake, basi, mtu huyo ameikana imani, na ni mbaya zaidi kuliko mtu asiyeamini.
8But if any provideth not for his own, and specially his own household, he hath denied the faith, and is worse than an unbeliever.
9Usimtie katika orodha ya wajane, mjane yeyote ambaye hajatimiza miaka sitini. Tena awe amepata kuolewa mara moja tu,
9Let none be enrolled as a widow under threescore years old, [having been] the wife of one man,
10na awe mwenye sifa nzuri: aliyewalea watoto wake vizuri, aliyewakaribisha wageni nyumbani kwake, aliyewaosha miguu watu wa Mungu, aliyewasaidia watu wenye taabu, na aliyejitolea kufanya mambo mema.
10well reported of for good works; if she hath brought up children, if she hath used hospitality to strangers, if she hath washed the saints' feet, if she hath relieved the afflicted, if she hath diligently followed every good work.
11Usiwaandikishe wajane vijana, kwani kama tamaa zao za maumbile zikizidi kuwa na nguvu zaidi kuliko kujitolea kwao kwa Kristo watataka kuolewa tena,
11But younger widows refuse: for when they have waxed wanton against Christ, they desire to marry;
12na wataonekana kukosa uaminifu kuhusu ahadi yao ya pale awali.
12having condemnation, because they have rejected their first pledge.
13Wajane kama hao huanza kupoteza wakati wao wakizurura nyumba hata nyumba; tena ubaya zaidi ni kwamba huanza kuwasengenya watu, na kujitia katika mambo ya watu wengine, huku wakisema mambo ambayo hawangepaswa kusema.
13And withal they learn also [to be] idle, going about from house to house; and not only idle, but tattlers also and busybodies, speaking things which they ought not.
14Kwa hiyo ningependelea wajane vijana waolewe, wapate watoto na kutunza nyumba zao ili adui zetu wasipewe nafasi ya kusema mambo maovu juu yetu.
14I desire therefore that the younger [widows] marry, bear children, rule the household, give no occasion to the adversary for reviling:
15Kwa maana wajane wengine wamekwisha potoka na kumfuata Shetani.
15for already some are turned aside after Satan.
16Lakini kama mama Mkristo anao wajane katika jamaa yake, yeye anapaswa kuwatunza na si kuliachilia kanisa mzigo huo, ili kanisa liweze kuwatunza wajane wale waliobaki peke yao kabisa.
16If any woman that believeth hath widows, let her relieve them, and let not the church be burdened; that it mat relieve them that are widows indeed.
17Wazee wanaowaongoza watu vizuri wanastahili kupata riziki maradufu, hasa wale wanaofanya bidii katika kuhubiri na kufundisha.
17Let the elders that rule well be counted worthy of double honor, especially those who labor in the word and in teaching.
18Maana Maandiko Matakatifu yasema: "Usimfunge ng'ombe kinywa anapopura nafaka." na tena "Mfanyakazi astahili malipo yake."
18For the scripture saith, Thou shalt not muzzle the ox when he treadeth out the corn. And, The laborer is worthy of his hire.
19Usikubali kupokea mashtaka dhidi ya mzee yasipowakilishwa na mashahidi wawili au watatu.
19Against an elder receive not an accusation, except at [the mouth of] two or three witnesses.
20Wale wanaotenda dhambi waonye hadharani, ili wengine wapate kuogopa.
20Them that sin reprove in the sight of all, that the rest also may be in fear.
21Nakuamuru mbele ya Mungu, mbele ya Kristo Yesu, na mbele ya malaika watakatifu uyazingatie maagizo haya bila kuacha hata moja, wala kumpendelea mtu yeyote katika kila unachotenda.
21I charge [thee] in the sight of God, and Christ Jesus, and the elect angels, that thou observe these things without prejudice, doing nothing by partiality.
22Usiharakishe kumwekea mtu yeyote mikono kwa ajili ya kumtumikia Bwana. Usishiriki dhambi za wengine; jiweke katika hali safi.
22Lay hands hastily on no man, neither be partaker of other men's sins: keep thyself pure.
23Usinywe maji tu, bali unywe divai kidogo kwa ajili ya tumbo lako, kwani unaugua mara kwa mara.
23Be no longer a drinker of water, but use a little wine for thy stomach's sake and thine often infirmities.
24Dhambi za watu wengine huonekana waziwazi, nazo zawatangulia kwenye hukumu; lakini dhambi za wengine huonekana tu baadaye.
24Some men's sins are evident, going before unto judgment; and some men also they follow after.
25Vivyo hivyo, matendo mema huonekana waziwazi, na hata yale ambayo si dhahiri hayawezi kufichika.
25In like manner also there are good works that are evident; and such as are otherwise cannot be hid.