1Sheria ya Wayahudi si picha kamili ya mambo yale halisi: ni kivuli tu cha mema yanayokuja. Dhabihu zilezile hutolewa daima, mwaka baada ya mwaka. Sheria yawezaje, basi, kwa njia ya dhabihu hizo, kuwafanya wale wanaoabudu wawe wakamilifu?
1For the law having a shadow of the good [things] to come, not the very image of the things, can never with the same sacrifices year by year, which they offer continually, make perfect them that draw nigh.
2Kama hao watu wanaomwabudu Mungu wangekuwa wametakaswa dhambi zao kweli, hawangejisikia tena kuwa na dhambi, na dhabihu hizo zote zingekoma.
2Else would they not have ceased to be offered? because the worshippers, having been once cleansed, would have had no more consciousness of sins.
3Lakini dhabihu hizo hufanyika kila mwaka kuwakumbusha watu dhambi zao.
3But in those [sacrifices] there is a remembrance made of sins year by year.
4Maana damu ya fahali na mbuzi haiwezi kamwe kuondoa dhambi.
4For it is impossible that the blood of bulls and goats should take away sins.
5Ndiyo maana Kristo alipokuwa anakuja ulimwenguni, alimwambia Mungu: "Hukutaka dhabihu wala sadaka, lakini umenitayarishia mwili.
5Wherefore when he cometh into the world, he saith, Sacrifice and offering thou wouldest not, But a body didst thou prepare for me;
6Sadaka za kuteketezwa au za kuondoa dhambi hazikupendezi.
6In whole burnt offerings and [sacrifices] for sin thou hadst no pleasure:
7Hapo nikasema: Niko hapa ee Mungu, tayari kufanya mapenzi yako kama ilivyoandikwa juu yangu katika kitabu cha Sheria."
7Then said I, Lo, I am come (In the roll of the book it is written of me) To do thy will, O God.
8Kwanza alisema: "Hutaki, wala hupendezwi na dhabihu na sadaka, sadaka za kuteketezwa na za kuondoa dhambi." Alisema hivyo ingawa sadaka hizi zote hutolewa kufuatana na Sheria.
8Saying above, Sacrifices and offerings and whole burnt offerings and [sacrifices] for sin thou wouldest not, neither hadst pleasure therein (the which are offered according to the law),
9Kisha akasema: "Niko hapa, ee Mungu, tayari kufanya mapenzi yako." Hivyo Mungu alibatilisha dhabihu za zamani na mahali pake akaweka dhabihu nyingine moja.
9then hath he said, Lo, I am come to do thy will. He taketh away the first, that he may establish the second.
10Kwa kuwa Yesu Kristo alitimiza mapenzi ya Mungu, sisi tunatakaswa dhambi zetu kwa ile dhabihu ya mwili wake aliyotoa mara moja tu, ikatosha.
10By which will we have been sanctified through the offering of the body of Jesus Christ once for all.
11Kila kuhani Myahudi humhudumia Mungu kila siku, akitoa dhabibu zilezile mara nyingi, dhabibu ambazo haziwezi kuondoa dhambi.
11And every priest indeed standeth day by day ministering and offering oftentimes the same sacrifices, the which can never take away sins:
12Lakini Kristo alitoa dhabihu moja tu kwa ajili ya dhambi, dhabihu ifaayo milele, kisha akaketi upande wa kulia wa Mungu.
12but he, when he had offered one sacrifice for sins for ever, sat down on the right hand of God;
13Huko anangoja mpaka adui zake watakapowekwa kama kibao chini ya miguu yake.
13henceforth expecting till his enemies be made the footstool of his feet.
14Basi, kwa dhabihu yake moja tu, amewafanya kuwa wakamilifu milele wale wanaotakaswa dhambi zao.
14For by one offering he hath perfected for ever them that are sanctified.
15Naye Roho Mtakatifu anatupa ushahidi wake. Kwanza anasema:
15And the Holy Spirit also beareth witness to us; for after he hath said,
16"Hili ndilo agano nitakalofanya nao, katika siku zijazo, asema Bwana: Nitaweka sheria zangu mioyoni mwao, na kuziandika akilini mwao."
16This is the covenant that I will make with them After those days, saith the Lord: I will put my laws on their heart, And upon their mind also will I write them; [then saith he,]
17Kisha akaongeza kusema: "Sitakumbuka tena dhambi zao, wala vitendo vyao vya uhalifu."
17And their sins and their iniquities will I remember no more.
18Basi, dhambi zikisha ondolewa, hakutakuwa na haja tena ya kutoa dhabihu za kuondoa dhambi.
18Now where remission of these is, there is no more offering for sin.
19Basi, ndugu, kwa damu ya Yesu tunapewa moyo thabiti wa kuingia Mahali Patakatifu.
19Having therefore, brethren, boldness to enter into the holy place by the blood of Jesus,
20Yeye ametufungulia njia mpya na yenye uzima kupitia lile pazia, yaani kwa njia ya mwili wake mwenyewe.
20by the way which he dedicated for us, a new and living way, through the veil, that is to say, his flesh;
21Basi, tunaye kuhani maarufu aliye na mamlaka juu ya nyumba ya Mungu.
21and [having] a great priest over the house of God;
22Kwa hiyo tumkaribie Mungu kwa moyo mnyofu na imani timilifu, kwa mioyo iliyotakaswa dhamiri mbaya, na kwa miili iliyosafishwa kwa maji safi.
22let us draw near with a true heart in fulness of faith, having our hearts sprinkled from an evil conscience: and having our body washed with pure water,
23Tushikilie imara tumaini lile tunalokiri, maana Mungu aliyefanya ahadi zake ni mwaminifu.
23let us hold fast the confession of our hope that it waver not; for he is faithful that promised:
24Tujitahidi kushughulikiana kwa ajili ya kuongezeana bidii ya kupendana na kutenda mema.
24and let us consider one another to provoke unto love and good works;
25Tusiache ile desturi ya kukutana pamoja, kama vile wengine wanavyofanya. Bali tunapaswa kusaidiana kwani, kama mwonavyo, Siku ile ya Bwana inakaribia.
25not forsaking our own assembling together, as the custom of some is, but exhorting [one another]; and so much the more, as ye see the day drawing nigh.
26Maana, tukiendelea kutenda dhambi makusudi baada ya kufahamu ukweli, hakuna dhabihu iwezayo kutolewa tena kwa ajili ya kuondoa dhambi.
26For if we sin wilfully after that we have received the knowledge of the truth, there remaineth no more a sacrifice for sins,
27Linalobaki ni kungojea tu kwa hofu hukumu ya Mungu na moto mkali utakaowaangamiza wote wanaompinga.
27but a certain fearful expectation of judgment, and a fierceness of fire which shall devour the adversaries.
28Mtu yeyote asiyeitii Sheria ya Mose, huuawa bila ya huruma kukiwa na ushahidi wa watu wawili au watatu.
28A man that hath set at nought Moses law dieth without compassion on [the word of] two or three witnesses:
29Je, mtu yule anayempuuza Mwana wa Mungu na kuidharau damu ya agano la Mungu iliyomtakasa, mtu anayemtukana Roho wa Mungu, anastahili kupata adhabu kali ya namna gani?
29of how much sorer punishment, think ye, shall he be judged worthy, who hath trodden under foot the Son of God, and hath counted the blood of the covenant wherewith he was sanctified an unholy thing, and hath done despite unto the Spirit of grace?
30Maana tunamfahamu yule aliyesema, "Mimi nitalipiza kisasi, mimi nitalipiza," na ambaye alisema pia, "Bwana atawahukumu watu wake."
30For we know him that said, Vengeance belongeth unto me, I will recompense. And again, The Lord shall judge his people.
31Kuanguka mikononi mwa Mungu aliye hai ni jambo la kutisha mno!
31It is a fearful thing to fall into the hands of the living God.
32Kumbukeni yaliyotokea siku zile za kwanza mlipoangaziwa mwanga wa Mungu. Ingawa siku zile mlipatwa na mateso mengi, ninyi mlistahimili.
32But call to remembrance the former days, in which, after ye were enlightened, ye endured a great conflict of sufferings;
33Mara nyingine mlitukanwa na kufedheheshwa hadharani; mara nyingine mlikuwa radhi kuungana na wale walioteswa namna hiyohiyo.
33partly, being made a gazingstock both by reproaches and afflictions; and partly, becoming partakers with them that were so used.
34Mlishiriki mateso ya wafungwa, na mliponyang'anywa mali yenu mlistahimili kwa furaha, maana mlijua kwamba mnayo mali bora zaidi na ya kudumu milele.
34For ye both had compassion on them that were in bonds, and took joyfully the spoiling of you possessions, knowing that ye have for yourselves a better possession and an abiding one.
35Basi, msipoteze uhodari wenu, maana utawapatieni tuzo kubwa.
35Cast not away therefore your boldness, which hath great recompense of reward.
36Mnahitaji kuwa na uvumilivu, ili mweze kufanya anayotaka Mungu na kupokea kile alichoahidi.
36For ye have need of patience, that, having done the will of God, ye may receive the promise.
37Maana kama yasemavyo Maandiko: "Bado kidogo tu, na yule anayekuja, atakuja, wala hatakawia.
37For yet a very little while, He that cometh shall come, and shall not tarry.
38Lakini mtu wangu aliye mwadilifu ataamini na kuishi; walakini akirudi nyuma, mimi sitapendezwa naye."
38But my righteous one shall live by faith: And if he shrink back, my soul hath no pleasure in him.
39Basi, sisi hatumo miongoni mwa wale wanaorudi nyuma na kupotea, ila sisi tunaamini na tunaokolewa.
39But we are not of them that shrink back unto perdition; but of them that have faith unto the saving of the soul.