Swahili: New Testament

American Standard Version

Mark

11

1Walipokuwa wanakaribia Yerusalemu walifika Bethfage na Bethania, karibu na mlima wa Mizeituni. Hapo aliwatuma wawili wa wanafunzi wake,
1And when they draw nigh unto Jerusalem, unto Bethphage and Bethany, at the mount of Olives, he sendeth two of his disciples,
2akawaambia, "Nendeni katika kijiji kilicho mbele yenu. Mtakapokuwa mnaingia humo, mtakuta mwana punda amefungwa ambaye bado hajatumiwa na mtu. Mfungueni mkamlete.
2and saith unto them, Go your way into the village that is over against you: and straightway as ye enter into it, ye shall find a colt tied, whereon no man ever yet sat; loose him, and bring him.
3Kama mtu akiwauliza, Mbona mnafanya hivyo? Mwambieni, Bwana anamhitaji na atamrudisha hapa mara."
3And if any one say unto you, Why do ye this? say ye, The Lord hath need of him; and straightway he will send him back hither.
4Basi, wakaenda, wakamkuta mwana punda barabarani amefungwa mlangoni. Walipokuwa wakimfungua,
4And they went away, and found a colt tied at the door without in the open street; and they loose him.
5baadhi ya watu waliokuwa wamesimama hapo wakawauliza "Kwa nini mnamfungua huyo mwana punda?"
5And certain of them that stood there said unto them, What do ye, loosing the colt?
6Wanafunzi wakajibu kama Yesu alivyokuwa amewaambia; nao wakawaacha waende zao.
6And they said unto them even as Jesus had said: and they let them go.
7Wakampelekea Yesu huyo mwana punda. Wakatandika mavazi yao juu ya huyo mwana punda, na Yesu akaketi juu yake.
7And they bring the colt unto Jesus, and cast on him their garments; and he sat upon him.
8Watu wengi wakatandaza mavazi yao barabarani; wengine wakatandaza matawi ya miti waliyoyakata mashambani.
8And many spread their garments upon the way; and others branches, which they had cut from the fields.
9Watu wote waliotangulia na wale waliofuata wakapaaza sauti zao wakisema, "Hosana! Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana!
9And they that went before, and they that followed, cried, Hosanna; Blessed [is] he that cometh in the name of the Lord:
10Ubarikiwe Ufalme ujao wa baba yetu Daudi. Hosana juu mbinguni!"
10Blessed [is] the kingdom that cometh, [the kingdom] of our father David: Hosanna in the highest.
11Yesu aliingia mjini Yerusalemu akaenda moja kwa moja mpaka Hekaluni, akatazama kila kitu kwa makini. Lakini kwa vile ilikwisha kuwa jioni, akaenda Bethania pamoja na wale kumi na wawili.
11And he entered into Jerusalem, into the temple; and when he had looked round about upon all things, it being now eventide, he went out unto Bethany with the twelve.
12Kesho yake, walipokuwa wanatoka Bethania, Yesu aliona njaa.
12And on the morrow, when they were come out from Bethany, he hungered.
13Basi, akaona kwa mbali mtini wenye majani mengi. Akauendea ili aone kama ulikuwa na tunda lolote. Alipoufikia, aliukuta bila tunda lolote ila majani matupu, kwa vile hayakuwa majira ya mtini kuzaa matunda.
13And seeing a fig tree afar off having leaves, he came, if haply he might find anything thereon: and when he came to it, he found nothing but leaves; for it was not the season of figs.
14Hapo akauambia mtini, "Tangu leo hata milele mtu yeyote asile matunda kwako." Nao wanafunzi wake walisikia maneno hayo.
14And he answered and said unto it, No man eat fruit from thee henceforward for ever. And his disciples heard it.
15Basi, wakafika Yerusalemu. Yesu akaingia Hekaluni, akaanza kuwafukuza nje watu waliokuwa wanauza na kununua vitu humo ndani. Akazipindua meza za wale waliokuwa wakibadilishana fedha na viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa.
15And they come to Jerusalem: and he entered into the temple, and began to cast out them that sold and them that bought in the temple, and overthrew the tables of the money-changers, and the seats of them that sold the doves;
16Hakumruhusu mtu yeyote kupitia Hekaluni akichukua kitu.
16and he would not suffer that any man should carry a vessel through the temple.
17Kisha akawafundisha, "Imeandikwa: Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa ajili ya mataifa yote! Lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi!"
17And he taught, and said unto them, Is it not written, My house shall be called a house of prayer for all the nations? but ye have made it a den of robbers.
18Makuhani wakuu na walimu wa Sheria waliposikia hayo, walianza kutafuta njia ya kumwangamiza. Lakini walimwogopa kwa sababu umati wa watu ulishangazwa na mafundisho yake.
18And the chief priests and the scribes heard it, and sought how they might destroy him: for they feared him, for all the multitude was astonished at his teaching.
19Ilipokuwa jioni, Yesu na wanafunzi wake waliondoka mjini.
19And every evening he went forth out of the city.
20Asubuhi na mapema, walipokuwa wanapita, waliuona ule mtini umenyauka wote, hata mizizi.
20And as they passed by in the morning, they saw the fig tree withered away from the roots.
21Petro aliukumbuka, akamwambia Yesu, "Mwalimu, tazama! Ule mtini ulioulaani, umenyauka!"
21And Peter calling to remembrance saith unto him, Rabbi, behold, the fig tree which thou cursedst is withered away.
22Yesu akawaambia, "Mwaminini Mungu.
22And Jesus answering saith unto them, Have faith in God.
23Nawaambieni kweli, mtu akiuambia mlima huu: Ng'oka ukajitose baharini bila kuona shaka moyoni mwake, ila akaamini kwamba mambo yote anayosema yanafanyika, atafanyiwa jambo hilo.
23Verily I say unto you, Whosoever shall say unto this mountain, Be thou taken up and cast into the sea; and shall not doubt in his heart, but shall believe that what he saith cometh to pass; he shall have it.
24Kwa hiyo nawaambieni, mnaposali na kuomba kitu, aminini kwamba mmekipokea, nanyi mtapewa.
24Therefore I say unto you, All things whatsoever ye pray and ask for, believe that ye receive them, and ye shall have them.
25Mnaposimama kusali, sameheni kila mtu aliyewakosea chochote, ili Baba yenu aliye mbinguni awasamehe ninyi makosa yenu.
25And whensoever ye stand praying, forgive, if ye have aught against any one; that your Father also who is in heaven may forgive you your trespasses.
26Lakini msipowasamehe wengine, hata Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu."
26[But if ye do not forgive, neither will your Father who is in heaven forgive your trespasses.]
27Basi, wakafika tena Yerusalemu. Yesu alipokuwa akitembea Hekaluni, makuhani wakuu, walimu wa Sheria na wazee walimwendea,
27And they come again to Jerusalem: and as he was walking in the temple, there come to him the chief priests, and the scribes, and the elders;
28wakamwuliza, "Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Nani aliyekupa mamlaka ya kufanya mambo haya?"
28and they said unto him, By what authority doest thou these things? or who gave thee this authority to do these things?
29Lakini Yesu akawaambia, "Nitawaulizeni swali moja; mkinijibu, na pia nitawaambieni ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya.
29And Jesus said unto them, I will ask of you one question, and answer me, and I will tell you by what authority I do these things.
30Je, mamlaka ya Yohane ya kubatiza yalitoka mbinguni ama kwa watu? Nijibuni."
30The baptism of John, was it from heaven, or from men? answer me.
31Wakaanza kujadiliana, "Tukisema, Yalitoka mbinguni, atatuuliza, Basi, mbona hamkumsadiki?
31And they reasoned with themselves, saying, If we shall say, From heaven; He will say, Why then did ye not believe him?
32Na tukisema, Yalitoka kwa watu..." (Waliogopa umati wa watu maana wote waliamini kwamba Yohane alikuwa kweli nabii.)
32But should we say, From men--they feared the people: for all verily held John to be a prophet.
33Basi, wakamjibu Yesu, "Sisi hatujui." Naye Yesu akawaambia, "Nami pia sitawaambieni ninafanya mambo haya kwa mamlaka gani."
33And they answered Jesus and say, We know not. And Jesus saith unto them, Neither tell I you by what authority I do these things.