1Baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohane nduguye, akaenda nao peke yao juu ya mlima mrefu.
1And after six days Jesus taketh with him Peter, and James, and John his brother, and bringeth them up into a high mountain apart:
2Huko, wakiwa wanamtazama, akageuka sura, uso wake ukang'aa kama jua na mavazi yake yakawa meupe kama nuru.
2and he was transfigured before them; and his face did shine as the sun, and his garments became white as the light.
3Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza naye.
3And behold, there appeared unto them Moses and Elijah talking with him.
4Hapo Petro akamwambia Yesu, "Bwana, ni vizuri sana kwamba tupo hapa! Ukipenda nitajenga vibanda vitatu: kimoja chako, kimoja cha Mose na kimoja cha Eliya."
4And Peter answered, and said unto Jesus, Lord, it is good for us to be here: if thou wilt, I will make here three tabernacles; one for thee, and one for Moses, and one for Elijah.
5Alipokuwa bado anasema hivyo, wingu jeupe likawafunika, na sauti ikasikika kutoka katika hilo wingu: "Huyu ni Mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye, msikilizeni."
5While he was yet speaking, behold, a bright cloud overshadowed them: and behold, a voice out of the cloud, saying, This is my beloved Son, in whom I am well pleased; hear ye him.
6Wanafunzi waliposikia hivyo wakaanguka kifudifudi, wakaogopa sana.
6And when the disciples heard it, they fell on their face, and were sore afraid.
7Yesu akawaendea, akawagusa, akasema, "Simameni, msiogope!"
7And Jesus came and touched them and said, Arise, and be not afraid.
8Walipoinua macho yao hawakumwona mtu, ila Yesu peke yake.
8And lifting up their eyes, they saw no one, save Jesus only.
9Basi, walipokuwa wanashuka mlimani, Yesu akawaonya: "Msimwambie mtu mambo mliyoyaona mpaka Mwana wa Mtu atakapofufuliwa kutoka wafu."
9And as they were coming down from the mountain, Jesus commanded them, saying, Tell the vision to no man, until the Son of man be risen from the dead.
10Kisha wanafunzi wakamwuliza, "Mbona walimu wa Sheria wanasema ati ni lazima kwanza Eliya aje?"
10And his disciples asked him, saying, Why then say the scribes that Elijah must first come?
11Yesu akawajibu, "Kweli, Eliya atakuja kutayarisha mambo yote.
11And he answered and said, Elijah indeed cometh, and shall restore all things:
12Lakini nawaambieni, Eliya amekwisha kuja nao hawakumtambua, bali walimtendea jinsi walivyotaka. Mwana wa Mtu atateswa vivyo hivyo mikononi mwao."
12but I say into you, that Elijah is come already, and they knew him not, but did unto him whatsoever they would. Even so shall the Son of man also suffer of them.
13Hapo hao wanafunzi wakafahamu kwamba alikuwa akiwaambia juu ya Yohane mbatizaji.
13Then understood the disciples that he spake unto them of John the Baptist.
14Walipojiunga tena na ule umati wa watu, mtu mmoja alimwendea Yesu, akampigia magoti,
14And when they were come to the multitude, there came to him a man, kneeling to him, saying,
15akasema, "Mheshimiwa, mwonee huruma mwanangu kwa kuwa ana kifafa, tena anateseka sana; mara nyingi yeye huanguka motoni na majini.
15Lord, have mercy on my son: for he is epileptic, and suffereth grievously; for oft-times he falleth into the fire, and off-times into the water.
16Nilimleta kwa wanafunzi wako lakini hawakuweza kumponya."
16And I brought him to thy disciples, and they could not cure him.
17Yesu akajibu, "Enyi kizazi kisicho na imani, kilichopotoka! Nitakaa nanyi mpaka lini? Nitawavumilia ninyi mpaka lini? Mleteni hapa huyo mtoto."
17And Jesus answered and said, O faithless and perverse generation, how long shall I be with you? how long shall I bear with you? bring him hither to me.
18Basi, Yesu akamkemea huyo pepo, naye akamtoka, na yule mtoto akapona wakati huohuo.
18And Jesus rebuked him; and the demon went out of him: and the boy was cured from that hour.
19Kisha wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha, wakamwuliza, "Kwa nini sisi hatukuweza kumtoa yule pepo?"
19Then came the disciples to Jesus apart, and said, Why could not we cast it out?
20Yesu akawajibu, "Kwa sababu ya imani yenu haba. Nawaambieni kweli, kama tu mkiwa na imani, hata iwe ndogo kama mbegu ya haradali, mtaweza kuuambia mlima huu: Toka hapa uende pale, nao utakwenda. Hakuna chochote ambacho hakingewezekana kwenu."
20And he saith unto them, Because of your little faith: for verily I say unto you, If ye have faith as a grain of mustard seed, ye shall say unto this mountain, Remove hence to yonder place; and it shall remove; and nothing shall be impossible unto you.
21"Pepo wa namna hii hawezi kuondolewa ila kwa sala na kufunga."
21[But this kind goeth not out save by prayer and fasting.]
22Walipokuwa pamoja huko Galilaya, Yesu aliwaambia, "Mwana wa Mtu atakabidhiwa kwa watu.
22And while they abode in Galilee, Jesus said unto them, The Son of man shall be delivered up into the hands of men;
23Watamuua, lakini siku ya tatu atafufuliwa." Wanafunzi wakahuzunika mno.
23and they shall kill him, and the third day he shall be raised up. And they were exceeding sorry.
24Walipofika Kafarnaumu watu wenye kukusanya fedha ya zaka ya Hekalu walimwendea Petro, wakamwuliza, "Je, mwalimu wenu hulipa fedha ya zaka?"
24And when they were come to Capernaum, they that received the half-shekel came to Peter, and said, Doth not your teacher pay the half-shekel?
25Petro akajibu, "Naam, hulipa." Basi, Petro alipoingia ndani ya nyumba, kabla hata hajasema neno, Yesu akamwuliza, "Simoni, wewe unaonaje? Wafalme wa dunia hukusanya ushuru au kodi kutoka kwa kina nani? Kutoka kwa wananchi ama kutoka kwa wageni?"
25He saith, Yea. And when he came into the house, Jesus spake first to him, saying, What thinkest thou, Simon? the kings of the earth, from whom do they receive toll or tribute? from their sons, or from strangers?
26Petro akajibu, "Kutoka kwa wageni." Yesu akamwambia, "Haya basi, wananchi hawahusiki.
26And when he said, From strangers, Jesus said unto him, Therefore the sons are free.
27Lakini kusudi tusiwakwaze, nenda ziwani ukatupe ndoana; chukua samaki wa kwanza atakayenaswa, fungua kinywa chake, na ndani utakuta fedha taslimu ya zaka. Ichukue ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako."
27But, lest we cause them to stumble, go thou to the sea, and cast a hook, and take up the fish that first cometh up; and when thou hast opened his mouth, thou shalt find a shekel: that take, and give unto them for me and thee.