Swahili: New Testament

American Standard Version

Matthew

20

1"Ufalme wa mbinguni unafanana na mtu mwenye shamba la mizabibu, ambaye alitoka asubuhi na mapema kuwaajiri wafanyakazi katika shamba lake.
1For the kingdom of heaven is like unto a man that was a householder, who went out early in the morning to hire laborers into his vineyard.
2Akapatana nao kuwalipa dinari moja kwa siku, kisha akawapeleka katika shamba lake la mizabibu.
2And when he had agreed with the laborers for a shilling a day, he sent them into his vineyard.
3Akatoka mnamo saa tatu asubuhi, akaona watu wengine wamesimama sokoni, hawana kazi.
3And he went out about the third hour, and saw others standing in the marketplace idle;
4Akawaambia, Nendeni nanyi mkafanye kazi katika shamba la mizabibu, nami nitawapeni haki yenu.
4and to them he said, Go ye also into the vineyard, and whatsoever is right I will give you. And they went their way.
5Basi, wakaenda. Huyo mwenye shamba akatoka tena mnamo saa sita na saa tisa, akafanya vivyo hivyo.
5Again he went out about the sixth and the ninth hour, and did likewise.
6Hata mnamo saa kumi na moja jioni, akatoka tena; akakuta watu wengine wamesimama pale sokoni. Basi, akawauliza, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?
6And about the eleventh [hour] he went out, and found others standing; and he saith unto them, Why stand ye here all the day idle?
7Wakamjibu: Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Yeye akawaambia, Nendeni nanyi mkafanye kazi katika shamba la mizabibu.
7They say unto him, Because no man hath hired us. He saith unto them, Go ye also into the vineyard.
8"Kulipokuchwa, huyo mwenye shamba alimwambia mtunza hazina wake, Waite wafanyakazi ukawalipe mshahara wao, ukianzia na wale walioajiriwa mwisho, na kumalizia na wale wa kwanza.
8And when even was come, the lord of the vineyard saith unto his steward, Call the laborers, and pay them their hire, beginning from the last unto the first.
9Basi, wakaja wale walioajiriwa mnamo saa kumi na moja, wakapokea kila mmoja dinari moja.
9And when they came that [were hired] about the eleventh hour, they received every man a shilling.
10Wale wa kwanza walipofika, walikuwa wanadhani watapewa zaidi; lakini hata wao wakapewa kila mmoja dinari moja.
10And when the first came, they supposed that they would receive more; and they likewise received every man a shilling.
11Wakazipokea fedha zao, wakaanza kumnung'unikia yule bwana.
11And when they received it, they murmured against the householder,
12Wakasema, Watu hawa walioajiriwa mwisho walifanya kazi kwa muda wa saa moja tu, mbona umetutendea sawa na wao hali sisi tumevumilia kazi ngumu kutwa na jua kali?
12saying, These last have spent [but] one hour, and thou hast made them equal unto us, who have borne the burden of the day and the scorching heat.
13"Hapo yule bwana akamjibu mmoja wao, Rafiki, sikukupunja kitu! Je, hukupatana nami mshahara wa denari moja?
13But he answered and said to one of them, Friend, I do thee no wrong: didst not thou agree with me for a shilling?
14Chukua haki yako, uende zako. Napenda kumpa huyu wa mwisho sawa na wewe.
14Take up that which is thine, and go thy way; it is my will to give unto this last, even as unto thee.
15Je, sina haki ya kufanya na mali yangu nipendavyo? Je, unaona kijicho kwa kuwa mimi ni mwema?"
15Is it not lawful for me to do what I will with mine own? or is thine eye evil, because I am good?
16Yesu akamaliza kwa kusema, "Hivyo, walio wa mwisho watakuwa wa kwanza na wa kwanza watakuwa wa mwisho."
16So the last shall be first, and the first last.
17Yesu alipokuwa anakwenda Yerusalemu, aliwachukua wale wanafunzi kumi na wawili faraghani, na njiani akawaambia,
17And as Jesus was going up to Jerusalem, he took the twelve disciples apart, and on the way he said unto them,
18"Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu, na huko Mwana wa Mtu atakabidhiwa kwa makuhani wakuu na walimu wa Sheria, nao watamhukumu auawe.
18Behold, we go up to Jerusalem; and the Son of man shall be delivered unto the chief priests and scribes; and they shall condemn him to death,
19Watamkabidhi kwa watu wa mataifa mengine ili adhihakiwe, apigwe viboko na kusulubiwa; lakini siku ya tatu atafufuliwa."
19and shall deliver him unto the Gentiles to mock, and to scourge, and to crucify: and the third day he shall be raised up.
20Hapo mama yao wana wa Zebedayo alimjia Yesu pamoja na wanawe, akapiga magoti mbele yake na kumwomba kitu.
20Then came to him the mother of the sons of Zebedee with her sons, worshipping [him], and asking a certain thing of him.
21Yesu akamwuliza, "Unataka nini?" Huyo mama akamwambia, "Ahidi kwamba katika Ufalme wako, hawa wanangu wawili watakaa mmoja upande wako wa kulia na mwingine upande wako wa kushoto."
21And he said unto her, What wouldest thou? She saith unto him, Command that these my two sons may sit, one on thy right hand, and one on thy left hand, in thy kingdom.
22Yesu akajibu, "Hamjui mnaomba nini. Je, mnaweza kunywa kikombe nitakachokunywa mimi?" Wakamjibu, "Tunaweza."
22But Jesus answered and said, Ye know not what ye ask. Are ye able to drink the cup that I am about to drink? They say unto him, We are able.
23Yesu akawaambia, "Kweli mtakunywa kikombe changu, lakini kuketi kulia au kushoto kwangu si kazi yangu kupanga; jambo hilo watapewa wale waliowekewa tayari na Baba yangu."
23He saith unto them, My cup indeed ye shall drink: but to sit on my right hand, and on [my] left hand, is not mine to give; but [it is for them] for whom it hath been prepared of my Father.
24Wale wanafunzi wengine kumi waliposikia hayo, wakawakasirikia hao ndugu wawili.
24And when the ten heard it, they were moved with indignation concerning the two brethren.
25Hivyo Yesu akawaita, akawaambia, "Mnajua kwamba watawala wa mataifa hutawala watu wao kwa mabavu na wakuu hao huwamiliki watu wao.
25But Jesus called them unto him, and said, Ye know that the rulers of the Gentiles lord it over them, and their great ones exercise authority over them.
26Lakini kwenu isiwe hivyo, ila yeyote anayetaka kuwa mkuu kati yenu sharti awe mtumishi wa wote;
26Not so shall it be among you: but whosoever would become great among you shall be your minister;
27na anayetaka kuwa wa kwanza kati yenu sharti awe mtumishi wenu.
27and whosoever would be first among you shall be your servant:
28Jinsi hiyohiyo, Mwana wa Mtu hakuja kutumikiwa, bali kutumikia na kutoa maisha yake kuwa fidia ya watu wengi."
28even as the Son of man came not to be ministered unto, but to minister, and to give his life a ransom for many.
29Yesu alipokuwa anaondoka mjini Yeriko, umati wa watu ulimfuata.
29And as they went out from Jericho, a great multitude followed him.
30Basi, kulikuwa na vipofu wawili wameketi kando ya njia, na waliposikia kwamba Yesu alikuwa anapitia hapo, walipaaza sauti: "Mheshimiwa, Mwana wa Daudi, utuhurumie!"
30And behold, two blind men sitting by the way side, when they heard that Jesus was passing by, cried out, saying, Lord, have mercy on us, thou son of David.
31Ule umati wa watu ukawakemea na kuwaambia wanyamaze. Lakini wao wakazidi kupaaza sauti: "Mheshimiwa, Mwana wa Daudi, utuhurumie!"
31And the multitude rebuked them, that they should hold their peace: but they cried out the more, saying, Lord, have mercy on us, thou son of David.
32Yesu akasimama, akawaita na kuwauliza, "Mnataka niwafanyie nini?"
32And Jesus stood still, and called them, and said, What will ye that I should do unto you?
33Wakamjibu, "Mheshimiwa, tunaomba macho yetu yafumbuliwe."
33They say unto him, Lord, that our eyes may be opened.
34Basi, Yesu akawaonea huruma, akawagusa macho yao, na papo hapo wakaweza kuona, wakamfuata.
34And Jesus, being moved with compassion, touched their eyes; and straightway they received their sight, and followed him.