Swahili: New Testament

Croatian

Matthew

3

1Siku hizo Yohane Mbatizaji alitokea, akaanza kuhubiri katika jangwa la Yudea:
1U one dane pojavi se Ivan Krstitelj propovijedajući u Judejskoj pustinji:
2"Tubuni, maana Ufalme wa mbinguni umekaribia."
2"Obratite se jer približilo se kraljevstvo nebesko!"
3Huyu Yohane ndiye yule ambaye nabii Isaya alinena juu yake aliposema: "Sauti ya mtu imesikika jangwani: Mtayarishieni Bwana njia yake, nyoosheni vijia vyake."
3Ovo je uistinu onaj o kom proreče Izaija prorok: Glas viče u pustinji: Pripravite put Gospodinu, poravnite mu staze!
4Yohane alivaa vazi lililoshonwa kwa manyoya ya ngamia, na ukanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.
4Ivan je imao odjeću od devine dlake i kožnat pojas oko bokova; hranom mu bijahu skakavci i divlji med.
5Basi, watu kutoka Yerusalemu, kutoka mkoa wote wa Yudea na sehemu zote za kandokando ya mto Yordani, walimwendea,
5Grnuo k njemu Jeruzalem, sva Judeja i sva okolica jordanska.
6wakaziungama dhambi zao, naye akawabatiza katika mto Yordani.
6Primali su od njega krštenje u rijeci Jordanu ispovijedajući svoje grijehe.
7Lakini alipowaona Mafarisayo wengi na Masadukayo wanamjia ili awabatize, aliwaambia, "Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani aliyewadokezea kwamba mnaweza kuiepuka ghadhabu inayokuja?
7Kad ugleda mnoge farizeje i saduceje gdje mu dolaze na krštenje, reče im: "Leglo gujinje! Tko li vas je samo upozorio da bježite od skore srdžbe?
8Onyesheni basi kwa matendo, kwamba mmetubu kweli.
8Donosite dakle plod dostojan obraćenja.
9Msidhani kwamba mtaweza kujitetea kwa kusema, Baba yetu ni Abrahamu! Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyafanya mawe haya yawe watoto wa Abrahamu.
9I ne usudite se govoriti u sebi: 'Imamo oca Abrahama!' Jer, kažem vam, Bog iz ovoga kamenja može podići djecu Abrahamovu.
10Basi, shoka liko tayari kuikata mizizi ya miti; hivyo, kila mti usiozaa matunda mazuri, utakatwa na kutupwa motoni.
10Već je sjekira položena na korijen stablima. Svako dakle stablo koje ne donosi dobroga roda, siječe se i u oganj baca."
11Mimi ninawabatizeni kwa maji kuonyesha kwamba mmetubu. Lakini yule anayekuja baada yangu ana uwezo kuliko mimi. Mimi sistahili hata kubeba viatu vyake. Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
11"Ja vas, istina, krstim vodom na obraćenje, ali onaj koji za mnom dolazi jači je od mene. Ja nisam dostojan obuće mu nositi. On će vas krstiti Duhom Svetim i ognjem.
12Yeye anashika mkononi chombo cha kupuria nafaka, ili aipure nafaka yake; akusanye ngano ghalani, na makapi ayachome kwa moto usiozimika."
12U ruci mu vijača, pročistit će svoje gumno i skupiti žito u svoju žitnicu, a pljevu spaliti ognjem neugasivim."
13Wakati huo Yesu alitoka Galilaya akafika katika mto Yordani, akamwendea Yohane ili abatizwe naye.
13Tada dođe Isus iz Galileje na Jordan Ivanu da ga on krsti.
14Lakini Yohane alijaribu kumzuia akisema, "Je, wewe unakuja kwangu? Mimi hasa ndiye ninayehitaji kubatizwa nawe."
14Ivan ga odvraćaše: "Ti mene treba da krstiš, a ti da k meni dolaziš?"
15Lakini Yesu akamjibu, "Acha tu iwe hivyo kwa sasa, maana kwa namna hii inafaa tuyatekeleze yale yote Mungu anayotaka." Hapo Yohane akakubali.
15Ali mu Isus odgovori: "Pusti sada! Ta dolikuje nam da tako ispunimo svu pravednost!" Tada mu popusti.
16Mara tu Yesu alipokwisha batizwa, alitoka majini; na ghafla mbingu zikafunguka, akaona Roho wa Mungu akishuka kama njiwa na kutua juu yake.
16Odmah nakon krštenja izađe Isus iz vode. I gle! Otvoriše se nebesa i ugleda Duha Božjega gdje silazi kao golub i spušta se na nj.
17Sauti kutoka mbinguni ikasema, "Huyu ndiye Mwanangu mpendwa, nimependezwa naye."
17I eto glasa s neba: "Ovo je Sin moj, Ljubljeni! U njemu mi sva milina!"