Swahili: New Testament

Estonian

John

9

1Yesu alipokuwa akipita alimwona mtu mmoja, kipofu tangu kuzaliwa.
1Edasi minnes nägi Jeesus ühte sündimisest saadik pimedat inimest.
2Basi, wanafunzi wakamwuliza, "Mwalimu! Ni nani aliyetenda dhambi: mtu huyu, ama wazazi wake, hata akazaliwa kipofu?"
2Ja ta jüngrid küsisid temalt: 'Rabi, kes on teinud pattu, kas tema ise või ta vanemad, et ta on sündinud pimedana?'
3Yesu akajibu, "Jambo hili halikutukia kwa sababu ya dhambi zake yeye, wala dhambi za wazazi wake; ila alizaliwa kipofu ili nguvu ya Mungu ionekane ikifanya kazi ndani yake.
3Jeesus vastas: 'Ei ole pattu teinud tema ise ega ta vanemad, vaid temas peavad saama avalikuks Jumala teod.
4Kukiwa bado mchana yatupasa kuendelea kufanya kazi za yule aliyenituma; maana usiku unakuja ambapo mtu hawezi kufanya kazi.
4Me peame tegema selle tegusid, kes minu on saatnud, niikaua kui on päev. Tuleb öö, mil ükski ei saa midagi teha.
5Wakati ningali ulimwenguni, mimi ni mwanga wa ulimwengu."
5Kuni mina olen maailmas, olen ma maailma valgus.'
6Baada ya kusema hayo, akatema mate chini, akafanyiza tope, akampaka yule kipofu machoni,
6Nende sõnade järel ta sülitas maha ja tegi süljest muda ning võidis mudaga tema silmi
7akamwambia, "Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu." (maana ya jina hili ni "aliyetumwa"). Basi, huyo kipofu akaenda, akanawa, kisha akarudi akiwa anaona.
7ja ütles talle: 'Mine pese end Siiloahi tiigis!' 'Siiloah' on tõlkes 'Läkitatu'. Siis pime läks ja pesi ning tuli tagasi nägijana.
8Basi, jirani zake na wale waliokuwa wanajua kwamba hapo awali alikuwa maskini mwombaji, wakasema, "Je, huyu siye yule maskini aliyekuwa akiketi na kuomba?"
8Siis ütlesid naabrid ja need, kes teda seni olid kerjusena näinud: 'Eks see ole sama mees, kes istus ja kerjas?'
9Baadhi yao wakasema, "Ndiye." Wengine wakasema, "La! Ila anafanana naye." Lakini huyo aliyekuwa kipofu akasema, "Ni mimi!"
9Ühed ütlesid: 'Jah, ta on seesama,' ja teised: 'Ei, ta on vaid tema sarnane.' Tema ise ütles: 'Mina olen seesama.'
10Basi, wakamwuliza, "Sasa, macho yako yalipataje kufumbuliwa?"
10Siis nad küsisid: 'Kuidas sinu silmad avanesid?'
11Naye akawajibu, "Yule mtu aitwaye Yesu alifanya tope, akanipaka machoni na kuniambia: Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu. Basi, mimi nikaenda, nikanawa, nikapata kuona."
11Tema vastas: 'Inimene, keda nimetatakse Jeesuseks, tegi muda ja võidis mu silmi ja ütles mulle: 'Mine Siiloahi tiigi äärde ja pese end!' Kui ma siis läksin ja pesin, saingi nägijaks.'
12Wakamwuliza, "Yeye yuko wapi?" Naye akawajibu, "Mimi sijui!"
12Ja nad küsisid temalt: 'Kus ta on?' Ta ütles: 'Ma ei tea.'
13Kisha wakampeleka huyo mtu aliyekuwa kipofu kwa Mafarisayo.
13Nad viisid tema, endise pimeda, variseride juurde,
14Siku hiyo Yesu alipofanya tope na kumfumbua macho mtu huyo, ilikuwa siku ya Sabato.
14sest see päev, mil Jeesus tegi muda ja avas ta silmad, oli hingamispäev.
15Basi, Mafarisayo wakamwuliza mtu huyo, "Umepataje kuona?" Naye akawaambia, "Alinipaka tope machoni, nami nikanawa na sasa naona."
15Ja variserid küsisid temalt nüüd omakorda, kuidas ta on saanud nägijaks. Aga tema ütles neile: 'Ta pani muda mu silmadele ja ma pesin end ning näen nüüd.'
16Baadhi ya Mafarisayo wakasema, "Mtu huyu hakutoka kwa Mungu, maana hashiki sheria ya Sabato." Lakini wengine wakasema, "Mtu mwenye dhambi awezaje kufanya ishara za namna hii?" Kukawa na mafarakano kati yao.
16Siis ütlesid mõned variseridest: 'See inimene ei ole Jumala juurest, sest ta ei pea hingamispäeva.' Teised ütlesid: 'Kuidas saab patune inimene teha niisuguseid tunnustähti?' Ja nende vahel oli lahkmeel.
17Wakamwuliza tena huyo mtu aliyekuwa kipofu, "Maadam yeye amekufungua macho, wasemaje juu yake?" Naye akawaambia, "Yeye ni nabii!"
17Nad ütlesid nüüd taas pimedale: 'Mida sina ise tema kohta ütled, et ta on avanud sinu silmad?' Aga tema ütles: 'Ta on prohvet.'
18Viongozi wa Wayahudi hawakusadiki kwamba mtu huyo alikuwa kipofu hapo awali na sasa anaona mpaka walipowaita wazazi wake.
18Siis ei tahtnud juudid uskuda, et ta oli olnud pime ja saanud nägijaks, kuni nad olid kutsunud nägijakssaanu vanemad
19Basi, wakawauliza hao wazazi, "Je, huyu ndiye mtoto wenu ambaye ninyi mwasema alizaliwa kipofu? Sasa amepataje kuona?"
19ning küsinud neilt: 'Kas see on teie poeg, kellest te ütlete, et ta sündis pimedana? Kuidas ta siis praegu näeb?'
20Wazazi wake wakajibu, "Tunajua kwamba huyu ni mtoto wetu, na kwamba alizaliwa kipofu.
20Seepeale kostsid ta vanemad: 'Me teame, et see on meie poeg ja et ta sündis pimedana,
21Lakini amepataje kuona, hatujui; na wala hatumjui yule aliyemfumbua macho. Mwulizeni yeye mwenyewe; yeye ni mtu mzima, anaweza kujitetea mwenyewe."
21aga kuidas ta nüüd näeb, seda me ei tea ega tea me ka seda, kes ta silmad avas. Küsige tema enda käest, ta on küllalt vana ja võib ise enda kohta rääkida.'
22Wazazi wake walisema hivyo kwa sababu waliwaogopa viongozi wa Wayahudi kwani viongozi hao walikuwa wamepatana ya kwamba mtu yeyote atakayekiri kwamba Yesu ni Kristo atafukuzwa nje ya sunagogi.
22Ta vanemad vastasid nõnda, sest nad kartsid juute, kuna juudid olid juba kokku leppinud, et kes iganes tema Messiaks tunnistab, heidetakse kogudusest välja.
23Ndiyo maana wazazi wake walisema: "Yeye ni mtu mzima, mwulizeni."
23Seepärast ta vanemad ütlesid: 'Ta on küllalt vana, küsige tema enda käest.'
24Basi, wakamwita tena aliyekuwa kipofu, wakamwambia, "Sema ukweli mbele ya Mungu! Sisi tunajua kwamba mtu huyu ni mwenye dhambi."
24Nad kutsusid nüüd teist korda inimese, kes oli olnud pime, ja ütlesid talle: 'Anna au Jumalale! Me teame, et see inimene on patune.'
25Yeye akajibu, "Kama ni mwenye dhambi mimi sijui. Lakini kitu kimoja najua: Nilikuwa kipofu, na sasa naona."
25Seepeale vastas too: 'Kas ta on patune või ei, seda mina ei tea. Tean ainult ühte: ma olin pime, praegu aga näen.'
26Basi, wakamwuliza, "Alikufanyia nini? Alikufumbuaje macho yako?"
26Nüüd nad küsisid temalt: 'Mis ta sulle tegi? Kuidas ta su silmad avas?'
27Huyo mtu akawajibu, "Nimekwisha waambieni, nanyi hamkusikiliza; kwa nini mwataka kusikia tena? Je, ninyi pia mnataka kuwa wafuasi wake?"
27Mees vastas neile: 'Ma ju ütlesin teile, ent teie ei võtnud kuulda. Miks te tahate seda veel kord kuulda? Kas ka teie tahate hakata tema jüngriteks?'
28Lakini wao wakamtukana wakisema, "Wewe ni mfuasi wake; sisi ni wafuasi wa Mose.
28Ja nad sõimasid teda ja ütlesid: 'Sina oled tema jünger, meie oleme aga Moosese jüngrid.
29Sisi tunajua kwamba Mungu alisema na Mose, lakini mtu huyu hatujui ametoka wapi!"
29Meie teame, et Jumal on rääkinud Moosesega, aga kust tema on, seda me ei tea.'
30Naye akawajibu, "Hili ni jambo la kushangaza! Ninyi hamjui ametoka wapi, lakini amenifumbua macho yangu!
30Mees kostis neile: 'See ongi imelik, et teie ei tea, kust ta on, ja ometi on ta avanud mu silmad.
31Tunajua kwamba Mungu hawasikilizi watu wenye dhambi, ila humsikiliza yeyote mwenye kumcha na kutimiza mapenzi yake.
31Me teame, et Jumal ei kuule patuseid, ent kui keegi on jumalakartlik ja teeb tema tahtmist, siis seda ta kuuleb.
32Tangu mwanzo wa ulimwengu haijasikika kwamba mtu ameyafumbua macho ya mtu aliyezaliwa kipofu.
32Veel ilmaski pole kuuldud, et keegi oleks avanud pimedalt sündinu silmad.
33Kama mtu huyu hakutoka kwa Mungu, hangeweza kufanya chochote!"
33Kui tema ei oleks Jumala juurest, ei suudaks ta teha midagi.'
34Wao wakamjibu, "Wewe ulizaliwa na kulelewa katika dhambi; unawezaje kutufundisha sisi?" Basi, wakamfukuzia mbali.
34Nad kostsid talle: 'Kas sina, kes sa oled sündinud lausa pattudes, tahad meid õpetada?' Ja nad heitsid ta kogudusest välja.
35Yesu alisikia kwamba walikuwa wamemfukuzia mbali, naye alipomkuta akamwuliza, "Je, wewe unamwamini Mwana wa Mtu?"
35Jeesus sai kuulda, et nad on ta kogudusest välja heitnud ja küsis teda kohates: 'Kas sa usud Inimese Pojasse?'
36Huyo mtu akajibu, "Mheshimiwa, niambie yeye ni nani, ili nipate kumwamini."
36Too kostis: 'Kes see on, isand? Ütle mulle seda, et ma saaksin temasse uskuda.'
37Yesu akamwambia, "Umekwisha mwona, naye ndiye anayesema nawe sasa."
37Jeesus ütles talle: 'Sa näed ju teda, see, kes sinuga räägib, ongi tema.'
38Basi, huyo mtu akasema, "Ninaamini Bwana!" Akamsujudia.
38Aga tema lausus: 'Ma usun, Issand!' ja kummardas teda.
39Yesu akasema, "Mimi nimekuja ulimwenguni kutoa hukumu, kusudi wasioona wapate kuona, na wale wanaoona wawe vipofu."
39Jeesus ütles: 'Mina olen tulnud maailma kohtumõistmiseks, et need, kes ei näe, hakkaksid nägema, ning nägijad jääksid pimedaks.'
40Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa pamoja naye walisikia maneno hayo, wakamwuliza, "Je, sisi pia ni vipofu?"
40Seda kuulsid mõned variseridest, kes olid tema juures, ja ütlesid talle: 'Kas meiegi oleme pimedad?'
41Yesu akawajibu, "Kama mngekuwa vipofu, hamngekuwa na hatia; lakini sasa ninyi mwasema: Sisi tunaona, na hiyo yaonyesha kwamba mna hatia bado.
41Jeesus ütles neile: 'Kui te oleksite pimedad, ei oleks teil pattu. Aga et te nüüd ütlete: 'Meie näeme', siis jääb teie patt teile.