Swahili: New Testament

Syriac: NT

Colossians

2

1Napenda mjue jinsi ninavyofanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu, kwa ajili ya watu wa Laodikea na kwa ajili ya wote ambao hawajapata kuniona kwa macho.
1ܨܒܐ ܐܢܐ ܕܝܢ ܕܬܕܥܘܢ ܐܝܢܐ ܐܓܘܢܐ ܐܝܬ ܠܝ ܚܠܦܝܟܘܢ ܘܚܠܦ ܗܢܘܢ ܕܒܠܕܝܩܝܐ ܘܚܠܦ ܫܪܟܐ ܐܝܠܝܢ ܕܦܪܨܘܦܝ ܠܐ ܚܙܘ ܒܒܤܪ ܀
2Nafanya hivi kusudi mioyo yao ifarijiwe na kuvutwa pamoja katika upendo, ili wajazwe uthabiti mwingi uletwao na elimu ya kweli. Hapo wataijua siri ya Mungu ambayo ni Kristo mwenyewe.
2ܕܢܬܒܝܐܘܢ ܠܒܘܬܗܘܢ ܘܢܬܩܪܒܘܢ ܒܚܘܒܐ ܠܟܠܗ ܥܘܬܪܐ ܕܦܝܤܐ ܘܠܤܘܟܠܐ ܕܝܕܥܬܗ ܕܐܪܙܐ ܕܐܠܗܐ ܐܒܐ ܘܕܡܫܝܚܐ ܀
3Ndani yake zimefichika hazina zote za hekima na elimu.
3ܗܘ ܕܒܗ ܟܤܝܢ ܟܠܗܝܢ ܤܝܡܬܐ ܕܚܟܡܬܐ ܘܕܝܕܥܬܐ ܀
4Basi, nawaambieni, msikubali kudanganywa na mtu yeyote kwa maneno ya uongo hata kama ni ya kuvutia sana.
4ܗܕܐ ܕܝܢ ܐܡܪ ܐܢܐ ܕܠܐ ܐܢܫ ܢܗܘܐ ܡܛܥܐ ܠܟܘܢ ܒܦܝܤܐ ܕܡܠܐ ܀
5Maana, ingawa mimi niko mbali nanyi kwa mwili, lakini niko pamoja nanyi kwa roho, na ninafurahi kuona uthabiti kamili mnaosimama nao pamoja katika imani yenu kwa Kristo.
5ܐܦܢ ܒܒܤܪ ܓܝܪ ܦܪܝܩ ܐܢܐ ܡܢܟܘܢ ܐܠܐ ܒܪܘܚ ܥܡܟܘܢ ܐܢܐ ܘܚܕܐ ܐܢܐ ܕܚܙܐ ܐܢܐ ܡܛܟܤܘܬܟܘܢ ܘܫܪܝܪܘܬܐ ܕܗܝܡܢܘܬܟܘܢ ܕܒܡܫܝܚܐ ܀
6Maadamu ninyi mmemkubali Kristo Yesu kuwa Bwana, basi, ishini katika muungano naye.
6ܐܝܟܢܐ ܗܟܝܠ ܕܩܒܠܬܘܢ ܠܝܫܘܥ ܡܫܝܚܐ ܡܪܢ ܒܗ ܗܠܟܘ ܀
7Mnapaswa kuwa na mizizi ndani yake, kujijenga juu yake na kuwa imara katika imani yenu kama mlivyofundishwa. Muwe na shukrani tele.
7ܟܕ ܡܫܪܪܝܢ ܥܩܪܝܟܘܢ ܘܡܬܒܢܝܢ ܐܢܬܘܢ ܒܗ ܘܡܬܩܝܡܝܢ ܐܢܬܘܢ ܒܗܝܡܢܘܬܐ ܗܝ ܕܝܠܦܬܘܢ ܕܒܗ ܬܬܝܬܪܘܢ ܒܬܘܕܝܬܐ ܀
8Angalieni basi, mtu asiwapotoshe kwa udanganyifu mtupu wa hekima ya kibinadamu, ambayo chanzo chake ni mafundisho ya mapokeo ya watu na ya pepo watawala, na wala si Kristo mwenyewe!
8ܐܙܕܗܪܘ ܕܠܡܐ ܐܢܫ ܢܚܠܨܟܘܢ ܒܦܝܠܤܦܘܬܐ ܘܒܛܥܝܘܬܐ ܤܪܝܩܬܐ ܐܝܟ ܝܘܠܦܢܐ ܕܒܢܝܢܫܐ ܘܐܝܟ ܐܤܛܘܟܤܘܗܝ ܕܥܠܡܐ ܘܠܐ ܐܝܟ ܡܫܝܚܐ ܀
9Maana, ndani yake Kristo katika ubinadamu wake, umo ukamilifu wote wa Mungu,
9ܕܒܗ ܥܡܪ ܟܠܗ ܡܘܠܝܐ ܕܐܠܗܘܬܐ ܓܘܫܡܢܐܝܬ ܀
10nanyi mmepewa uzima kamili katika kuungana naye. Yeye yuko juu ya pepo watawala wote na wakuu wote.
10ܘܒܗ ܐܦ ܐܢܬܘܢ ܡܫܬܡܠܝܬܘܢ ܕܗܘ ܐܝܬܘܗܝ ܪܫܐ ܕܟܠܗܝܢ ܐܪܟܘܤ ܘܫܘܠܛܢܐ ܀
11Katika kuungana na Kristo ninyi mlitahiriwa, lakini si kwa tohara ifanywayo na watu, bali inayofanywa na Kristo mwenyewe, na ambayo inahusikana na kukombolewa kutoka katika utu wa dhambi.
11ܘܒܗ ܐܬܓܙܪܬܘܢ ܓܙܘܪܬܐ ܕܠܐ ܒܐܝܕܝܢ ܒܫܠܚ ܒܤܪܐ ܕܚܛܗܐ ܒܓܙܘܪܬܗ ܕܡܫܝܚܐ ܀
12Maana, mlipobatizwa mlizikwa pamoja na Kristo, na katika ubatizo, mlifufuliwa pia pamoja naye kwa imani yenu katika nguvu ya Mungu ambaye alimfufua Kristo kutoka wafu.
12ܘܐܬܩܒܪܬܘܢ ܥܡܗ ܒܡܥܡܘܕܝܬܐ ܘܒܗ ܩܡܬܘܢ ܥܡܗ ܕܗܝܡܢܬܘܢ ܒܚܝܠܐ ܕܐܠܗܐ ܕܐܩܝܡܗ ܡܢ ܒܝܬ ܡܝܬܐ ܀
13Wakati mmoja nanyi mlikuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kwa sababu ninyi mlikuwa watu wa mataifa mengine. Lakini Mungu amewapa ninyi uzima pamoja na Kristo. Mungu ametusamehe dhambi zetu zote;
13ܘܠܟܘܢ ܕܡܝܬܝܢ ܗܘܝܬܘܢ ܒܚܛܗܝܟܘܢ ܘܒܥܘܪܠܘܬ ܒܤܪܟܘܢ ܐܚܝܟܘܢ ܥܡܗ ܘܫܒܩ ܠܢ ܟܠܗܘܢ ܚܛܗܝܢ ܀
14alifutilia mbali ile hati ya deni iliyokuwa inatukabili na masharti yake, na kuifuta kabisa kwa kuipigilia msalabani.
14ܘܥܛܐ ܒܦܘܩܕܢܘܗܝ ܫܛܪ ܚܘܒܝܢ ܗܘ ܕܐܝܬܘܗܝ ܗܘܐ ܤܩܘܒܠܢ ܘܫܩܠܗ ܡܢ ܡܨܥܬܐ ܘܩܒܥܗ ܒܙܩܝܦܗ ܀
15Juu ya msalaba Kristo aliwapokonya nguvu zao hao pepo watawala na wakuu; aliwafanya kuwa kitu cha fedheha hadharani kwa kuwaburuta kama mateka katika msafara wa ushindi wake.
15ܘܒܫܠܚ ܦܓܪܗ ܦܪܤܝ ܠܐܪܟܘܤ ܘܠܫܠܝܛܢܐ ܘܐܒܗܬ ܐܢܘܢ ܓܠܝܐܝܬ ܒܩܢܘܡܗ ܀
16Kwa hiyo, basi, msikubali kupewa masharti na mtu yeyote kuhusu vyakula au vinywaji, siku za sherehe, sikukuu ya Mwezi mpya au Sabato.
16ܠܐ ܗܟܝܠ ܐܢܫ ܢܕܘܕܟܘܢ ܒܡܐܟܠܐ ܘܒܡܫܬܝܐ ܐܘ ܒܦܘܠܓܐ ܕܥܐܕܐ ܘܕܪܝܫ ܝܪܚܐ ܘܕܫܒܐ ܀
17Mambo ya aina hiyo ni kivuli tu cha yale yatakayokuja; ukweli wenyewe ndiye Kristo.
17ܗܠܝܢ ܕܐܝܬܝܗܝܢ ܛܠܢܝܬܐ ܕܐܝܠܝܢ ܕܥܬܝܕܢ ܦܓܪܐ ܕܝܢ ܡܫܝܚܐ ܗܘ ܀
18Msikubali kuhukumiwa na mtu yeyote anayejitakia kuwa wa maana kwa sababu ya maono ya pekee na ambaye anasisitiza juu ya unyenyekevu wa uongo na ibada kwa malaika. Mtu wa namna hiyo amepumbazika kwa fikira danganifu za kidunia
18ܘܠܡܐ ܐܢܫ ܢܨܒܐ ܒܡܟܝܟܘܬ ܪܥܝܢܐ ܠܡܚܝܒܘܬܟܘܢ ܕܬܫܬܥܒܕܘܢ ܠܦܘܠܚܢܐ ܕܡܠܐܟܐ ܒܕܤܥܐ ܥܠ ܡܕܡ ܕܠܐ ܚܙܐ ܘܤܪܝܩܐܝܬ ܡܬܚܬܪ ܒܪܥܝܢܐ ܕܒܤܪܗ ܀
19na amejitenga na Kristo aliye kichwa cha huo mwili. Chini ya uongozi wa Kristo, mwili wote unalishwa na kuunganishwa pamoja kwa viungo na mishipa yake, nao hukua kama atakavyo Mungu.
19ܘܠܐ ܐܚܕ ܪܫܐ ܕܡܢܗ ܟܠܗ ܦܓܪܐ ܡܬܪܟܒ ܘܡܬܩܝܡ ܒܫܪܝܢܐ ܘܒܗܕܡܐ ܘܪܒܐ ܬܪܒܝܬܐ ܕܐܠܗܐ ܀
20Ninyi mmekufa pamoja na Kristo na kukombolewa kutoka nguvu za pepo watawala wa ulimwengu. Kwa nini, basi, kuishi tena kama vile mngekuwa wa ulimwengu huu? Ya nini kuwekewa masharti:
20ܐܢ ܓܝܪ ܡܝܬܬܘܢ ܥܡ ܡܫܝܚܐ ܡܢ ܐܤܛܘܟܤܘܗܝ ܕܥܠܡܐ ܠܡܢܐ ܐܝܟ ܗܘ ܕܚܝܝܢ ܐܢܬܘܢ ܒܥܠܡܐ ܡܬܕܝܢܝܢ ܐܢܬܘܢ ܀
21"Msishike hiki," "Msionje kile," "Msiguse kile!"
21ܠܐ ܠܡ ܬܩܪܘܒ ܘܠܐ ܬܛܥܡ ܘܠܐ ܬܩܦ ܀
22Mambo hayo yote yanahusika na vitu vyenye kuharibika mara tu vinapotumiwa; hayo ni maagizo na mafundisho ya kibinadamu tu.
22ܕܐܝܬܝܗܝܢ ܗܠܝܢ ܚܫܚܬܐ ܕܡܬܚܒܠܐ ܘܦܘܩܕܐ ܐܢܝܢ ܘܝܘܠܦܢܐ ܕܒܢܝܢܫܐ ܀
23Kweli, masharti hayo yaonekana kuwa ya hekima katika namna ya ibada ya kujitakia wenyewe, unyenyekevu wa uongo na kuutendea mwili kwa ukali; lakini kwa kweli, haifai chochote kuzuia tamaa za mwili.
23ܘܡܬܚܙܝܢ ܕܐܝܬ ܒܗܝܢ ܡܠܬܐ ܕܚܟܡܬܐ ܒܦܪܨܘܦ ܡܟܝܟܘܬܐ ܘܕܚܠܬ ܐܠܗܐ ܘܕܠܐ ܚܝܤܝܢ ܥܠ ܦܓܪܐ ܠܘ ܒܡܕܡ ܕܡܝܩܪ ܐܠܐ ܒܐܝܠܝܢ ܕܚܫܚܬܐ ܐܢܝܢ ܕܒܤܪܐ ܀