1Kumbuka kwamba, katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati za taabu.
1But know this, that in the last days, grievous times will come.
2watu watakuwa na ubinafsi, wenye tamaa ya fedha, wenye majivuno, wenye kujiona, wenye kumtukana Mungu, wasiowatii wazazi wao, wasio na shukrani na waovu;
2For men will be lovers of self, lovers of money, boastful, arrogant, blasphemers, disobedient to parents, unthankful, unholy,
3watatokea watu wasio na upendo moyoni, wasio na huruma, wachongezi, walafi na wakali; watachukia chochote kilicho chema;
3without natural affection, unforgiving, slanderers, without self-control, fierce, no lovers of good,
4watakuwa wahaini, wakaidi na waliojaa kiburi; watapenda anasa kuliko kumpenda Mungu.
4traitors, headstrong, conceited, lovers of pleasure rather than lovers of God;
5Kwa nje wataonekana kama watu wenye kumcha Mungu, lakini wataikana nguvu yake. Jiepushe kabisa na watu wa namna hiyo.
5holding a form of godliness, but having denied its power. Turn away from these, also.
6Baadhi yao huenda katika nyumba za watu na huwateka wanawake dhaifu waliolemewa mizigo ya dhambi na ambao wanaongozwa na tamaa za kila aina;
6For some of these are people who creep into houses, and take captive gullible women loaded down with sins, led away by various lusts,
7wanawake ambao wanajaribu daima kujifunza lakini hawawezi kuufikia ujuzi wa huo ukweli.
7always learning, and never able to come to the knowledge of the truth.
8Watu hao huupinga ukweli kama vile Yane na Yambre walivyompinga Mose.
8Even as Jannes and Jambres opposed Moses, so do these also oppose the truth; men corrupted in mind, who concerning the faith, are rejected.
9Lakini hawataweza kuendelea zaidi kwa maana upumbavu wao utaonekana wazi kwa wote. Ndivyo ilivyokuwa kwa akina Yane na Yambre.
9But they will proceed no further. For their folly will be evident to all men, as theirs also came to be.
10Wewe lakini, umeyafuata mafundisho yangu, mwenendo wangu, makusudi yangu katika maisha, imani yangu, uvumilivu wangu, upendo wangu, subira yangu,
10But you did follow my teaching, conduct, purpose, faith, patience, love, steadfastness,
11udhalimu na mateso yangu. Unayajua mambo yaliyonipata huko Antiokia, Ikonio na Lustra. Nilivumilia udhalimu mkubwa mno! Lakini Bwana aliniokoa katika mambo hayo yote.
11persecutions, and sufferings: those things that happened to me at Antioch, Iconium, and Lystra. I endured those persecutions. Out of them all the Lord delivered me.
12Kila mtu anayetaka kuishi maisha ya kumcha Mungu katika kuungana na Kristo Yesu lazima adhulumiwe.
12Yes, and all who desire to live godly in Christ Jesus will suffer persecution.
13Watu waovu na wadanyanyifu watazidi kuwa waovu zaidi na zaidi kwa kuwadanganya wengine na kudanganyika wao wenyewe.
13But evil men and impostors will grow worse and worse, deceiving and being deceived.
14Lakini wewe dumu katika ukweli ule uliofundishwa, ukaukubali kabisa. Unawajua wale waliokuwa walimu wako.
14But you remain in the things which you have learned and have been assured of, knowing from whom you have learned them.
15Unakumbuka kwamba tangu utoto wako umeyajua Maandiko Matakatifu ambayo yaweza kukupatia hekima iletayo wokovu kwa njia ya imani kwa Kristo Yesu.
15From infancy, you have known the holy Scriptures which are able to make you wise for salvation through faith, which is in Christ Jesus.
16Maandiko yote Matakatifu yameandikwa kwa uongozi wa Mungu, na yanafaa katika kufundishia ukweli, kuonya, kusahihisha makosa, na kuwaongoza watu waishi maisha adili,
16Every Scripture is God-breathed and or, Every writing inspired by God is profitable for teaching, for reproof, for correction, and for instruction in righteousness,
17ili mtu anayemtumikia Mungu awe mkamilifu, na tayari kabisa kufanya kila tendo jema.
17that the man of God may be complete, thoroughly equipped for every good work.