World English Bible

Swahili: New Testament

Hebrews

13

1Let brotherly love continue.
1Endeleeni kupendana kidugu.
2Don’t forget to show hospitality to strangers, for in doing so, some have entertained angels without knowing it.
2Msisahau kuwakaribisha wageni; maana kwa kufanya hivyo watu wengine walipata kuwakaribisha malaika bila kujua.
3Remember those who are in bonds, as bound with them; and those who are ill-treated, since you are also in the body.
3Wakumbukeni wale waliofungwa kana kwamba mmefungwa pamoja nao. Wakumbukeni wale wanaoteseka kana kwamba nanyi mnateseka kama wao.
4Let marriage be held in honor among all, and let the bed be undefiled: but God will judge the sexually immoral and adulterers.
4Ndoa inapaswa kuheshimiwa na watu wote, na haki zake zitekelezwe kwa uaminifu. Mungu atawahukumu waasherati na wazinzi.
5Be free from the love of money, content with such things as you have, for he has said, “I will in no way leave you, neither will I in any way forsake you.”
5Msiwe watu wa kupenda fedha; toshekeni na vile vitu mlivyo navyo. Mungu mwenyewe amesema: "Sitakuacha kamwe, wala sitakutupa."
6So that with good courage we say, “The Lord is my helper. I will not fear. What can man do to me?”
6Ndiyo maana tunathubutu kusema: "Bwana ndiye msaada wangu, sitaogopa. Binadamu atanifanya nini?"
7Remember your leaders, men who spoke to you the word of God, and considering the results of their conduct, imitate their faith.
7wakumbukeni viongozi wenu waliowatangazieni ujumbe wa Mungu. Fikirieni juu ya mwenendo wao, mkaige imani yao.
8Jesus Christ is the same yesterday, today, and forever.
8Yesu Kristo ni yuleyule, jana, leo na milele.
9Don’t be carried away by various and strange teachings, for it is good that the heart be established by grace, not by food, through which those who were so occupied were not benefited.
9Msipeperushwe huku na huku kwa mafundisho tofauti ya kigeni. Neema ya Mungu ndiyo inayoimarisha roho zetu na wala si masharti juu ya chakula; masharti hayo hayakumsaidia kamwe mtu yeyote aliyeyafuata.
10We have an altar from which those who serve the holy tabernacle have no right to eat.
10Sisi tunayo madhabahu ambayo wale wanaotumikia bado katika hema la Wayahudi, hawana haki ya kula vitu vyake.
11For the bodies of those animals, whose blood is brought into the holy place by the high priest as an offering for sin, are burned outside of the camp.
11Kuhani Mkuu wa Kiyahudi huleta damu ya wanyama katika Mahali Patakatifu na kuitoa dhabihu kwa ajili ya dhambi; lakini nyama za hao wanyama huteketezwa nje ya kambi.
12Therefore Jesus also, that he might sanctify the people through his own blood, suffered outside of the gate.
12Ndiyo maana Yesu pia, kusudi apate kuwatakasa watu kwa damu yake mwenyewe, aliteswa na kufa nje ya mji.
13Let us therefore go out to him outside of the camp, bearing his reproach.
13Basi, tumwendee huko nje ya kambi tukajitwike laana yake.
14For we don’t have here an enduring city, but we seek that which is to come.
14Maana hapa duniani hatuna mji wa kudumu; lakini tunautafuta ule unaokuja.
15Through him, then, let us offer up a sacrifice of praise to God continually, that is, the fruit of lips which proclaim allegiance to his name.
15Basi, kwa njia ya Yesu, tumtolee Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani sifa zinazotolewa na midomo inayoliungama jina lake.
16But don’t forget to be doing good and sharing, for with such sacrifices God is well pleased.
16Msisahau kutenda mema na kusaidiana, maana hizi ndizo dhabihu zinazompendeza Mungu.
17Obey your leaders and submit to them, for they watch on behalf of your souls, as those who will give account, that they may do this with joy, and not with groaning, for that would be unprofitable for you.
17Watiini viongozi wenu na kushika amri zao; wao huchunga roho zenu usiku na mchana, na watatoa ripoti ya utumishi wao mbele ya Mungu. Kama mkiwatii watafanya kazi zao kwa furaha, la sivyo, watazifanya kwa huzuni, na hiyo haitakuwa na faida kwenu.
18Pray for us, for we are persuaded that we have a good conscience, desiring to live honorably in all things.
18Tuombeeni na sisi. Tuna hakika kwamba tunayo dhamiri safi, maana twataka kufanya lililo sawa daima.
19I strongly urge you to do this, that I may be restored to you sooner.
19Nawasihi sana mniombee ili Mungu anirudishe kwenu upesi iwezekanavyo.
20Now may the God of peace, who brought again from the dead the great shepherd of the sheep with the blood of an eternal covenant, our Lord Jesus,
20Mungu amemfufua Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ni Mchungaji Mkuu wa kondoo kwa sababu ya kumwaga damu yake iliyothibitisha agano la milele.
21make you complete in every good work to do his will, working in you that which is well pleasing in his sight, through Jesus Christ, to whom be the glory forever and ever. Amen.
21Mungu wa amani awakamilishe katika kila tendo jema ili mtekeleze mapenzi yake; yeye na afanye ndani yetu kwa njia ya Kristo yale yanayompendeza mwenyewe. Utukufu uwe kwake, milele na milele! Amina.
22But I exhort you, brothers, endure the word of exhortation, for I have written to you in few words.
22Basi, ndugu, nawasihi mpokee kwa utulivu ujumbe huu wa kuwatieni moyo. Hii ni barua fupi tu ambayo nimewaandikieni.
23Know that our brother Timothy has been freed, with whom, if he comes shortly, I will see you.
23Napenda kuwajulisheni kwamba ndugu yetu Timotheo amekwisha funguliwa gerezani. Kama akifika hapa mapema, nitakuja naye nitakapokuja kwenu.
24Greet all of your leaders and all the saints. The Italians greet you.
24Wasalimieni viongozi wenu wote pamoja na watu wa Mungu! Ndugu wa Italia wanawasalimuni.
25Grace be with you all. Amen.
25Tunawatakieni nyote neema ya Mungu.