World English Bible

Swahili: New Testament

Luke

22

1Now the feast of unleavened bread, which is called the Passover, drew near.
1Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa chachu, iitwayo Pasaka, ilikuwa inakaribia.
2The chief priests and the scribes sought how they might put him to death, for they feared the people.
2Makuhani wakuu na walimu wa Sheria wakawa wanatafuta njia ya kumwua Yesu, lakini waliwaogopa watu.
3Satan entered into Judas, who was surnamed Iscariot, who was numbered with the twelve.
3Basi, Shetani akamwingia Yuda aitwae Iskarioti, mmoja wa wale mitume kumi na wawili.
4He went away, and talked with the chief priests and captains about how he might deliver him to them.
4Yuda akaenda akajadiliana na makuhani wakuu na walinzi wa Hekalu kuhusu atakavyomsaliti Yesu kwao.
5They were glad, and agreed to give him money.
5Nao wakafurahi na kupatana naye kumlipa fedha.
6He consented, and sought an opportunity to deliver him to them in the absence of the multitude.
6Yuda akakubali, na akawa anatafuta nafasi nzuri ya kumkabidhi kwao bila umati wa watu kujua.
7The day of unleavened bread came, on which the Passover must be sacrificed.
7Basi, siku ya Mikate Isiyotiwa chachu ikafika. Hiyo ndiyo siku ambayo mwana kondoo wa Pasaka huchinjwa.
8He sent Peter and John, saying, “Go and prepare the Passover for us, that we may eat.”
8Hivyo Yesu akawatuma Petro na Yohane, akawaambia, "Nendeni mkatuandalie karamu ili tupate kula Pasaka."
9They said to him, “Where do you want us to prepare?”
9Nao wakamwuliza, "Unataka tuiandae wapi?"
10He said to them, “Behold, when you have entered into the city, a man carrying a pitcher of water will meet you. Follow him into the house which he enters.
10Akawaambia, "Sikilizeni! Mtakapokuwa mnakwenda mjini, mtakutana na mwanamume anayebeba mtungi wa maji. Mfuateni mpaka ndani ya nyumba atakayoingia.
11 Tell the master of the house, ‘The Teacher says to you, “Where is the guest room, where I may eat the Passover with my disciples?”’
11Mwambieni mwenye nyumba: Mwalimu anakuuliza, kiko wapi kile chumba ambamo nitakula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu?
12 He will show you a large, furnished upper room. Make preparations there.”
12Naye atawaonyesheni chumba kikubwa ghorofani ambacho kimepambwa. Andalieni humo."
13They went, found things as he had told them, and they prepared the Passover.
13Basi, wakaenda, wakakuta kila kitu sawa kama Yesu alivyokuwa amewaambia; wakaandaa karamu ya Pasaka.
14When the hour had come, he sat down with the twelve apostles.
14Saa ilipotimia, Yesu akakaa kula chakula pamoja na mitume wake.
15He said to them, “I have earnestly desired to eat this Passover with you before I suffer,
15Akawaambia, "Nimetamani sana kula Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu.
16 for I tell you, I will no longer by any means eat of it until it is fulfilled in the Kingdom of God.”
16Maana nawaambieni, sitaila tena hadi hapo itakapokamilika katika Ufalme wa Mungu."
17He received a cup, and when he had given thanks, he said, “Take this, and share it among yourselves,
17Kisha akatwaa kikombe, akashukuru akasema, "Pokeeni, mgawanye ninyi kwa ninyi.
18 for I tell you, I will not drink at all again from the fruit of the vine, until the Kingdom of God comes.”
18Kwa maana nawaambieni, sitakunywa tena divai ya zabibu mpaka Ufalme wa Mungu utakapokuja."
19He took bread, and when he had given thanks, he broke it, and gave to them, saying, “This is my body which is given for you. Do this in memory of me.”
19Halafu akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa akisema, "Huu ni mwili wangu, unaotolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa kunikumbuka."
20Likewise, he took the cup after supper, saying, “This cup is the new covenant in my blood, which is poured out for you.
20Akafanya vivyo hivyo na kikombe, baada ya chakula, akisema, "Kikombe hiki ni agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu inayomwagika kwa ajili yenu.
21 But behold, the hand of him who betrays me is with me on the table.
21"Lakini, tazameni! Yule atakayenisaliti yuko nami hapa mezani.
22 The Son of Man indeed goes, as it has been determined, but woe to that man through whom he is betrayed!”
22Kweli Mwana wa Mtu anakwenda kuuawa kama ilivyopangwa, lakini ole wake mtu anayemsaliti."
23They began to question among themselves, which of them it was who would do this thing.
23Hapo wakaanza kuulizana wao kwa wao ni nani kati yao atakayefanya jambo hilo.
24There arose also a contention among them, which of them was considered to be greatest.
24Kulitokea ubishi kati ya hao mitume kuhusu nani miongoni mwao anayefikiriwa kuwa mkuu zaidi kuliko wengine.
25He said to them, “The kings of the nations lord it over them, and those who have authority over them are called ‘benefactors.’
25Yesu akawaambia, "Wafalme wa mataifa huwatawala watu wao kwa mabavu, nao huitwa wafadhili wa watu.
26 But not so with you. But one who is the greater among you, let him become as the younger, and one who is governing, as one who serves.
26Lakini isiwe hivyo kati yenu; bali, yule aliye mkuu kati yenu ni lazima awe mdogo wa wote, na aliye kiongozi lazima awe kama mtumishi.
27 For who is greater, one who sits at the table, or one who serves? Isn’t it he who sits at the table? But I am in the midst of you as one who serves.
27Kwa maana, ni nani aliye mkuu: yule anayeketi mezani kula chakula, ama yule anayetumikia? Bila shaka ni yule anayeketi mezani kula chakula! Hata hivyo, mimi niko hapa kati yenu kama mtumishi.
28 But you are those who have continued with me in my trials.
28"Ninyi ndio mliobaki nami wakati wote wa majaribu yangu;
29 I confer on you a kingdom, even as my Father conferred on me,
29na, kama vile Baba yangu alivyonikabidhi Ufalme, vivyo hivyo nami nitawakabidhi ninyi Ufalme.
30 that you may eat and drink at my table in my Kingdom. You will sit on thrones, judging the twelve tribes of Israel.”
30Mtakula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu, na mtaketi katika viti vya enzi kuyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.
31The Lord said, “Simon, Simon, behold, Satan asked to have you, that he might sift you as wheat,
31"Simoni, Simoni! Sikiliza! Shetani alitaka kuwapepeta ninyi kama mtu anavyopepeta ngano.
32 but I prayed for you, that your faith wouldn’t fail. You, when once you have turned again, establish your brothers .”
32Lakini mimi nimekuombea ili imani yako isipungue. Nawe utakaponirudia, watie moyo ndugu zako."
33He said to him, “Lord, I am ready to go with you both to prison and to death!”
33Naye Petro akamjibu, "Bwana, mimi niko tayari kwenda pamoja nawe gerezani, na hata kufa."
34He said, “I tell you, Peter, the rooster will by no means crow today until you deny that you know me three times.”
34Yesu akamjibu, "Nakwambia wewe Petro, kabla jogoo hajawika leo utakuwa umenikana mara tatu."
35He said to them, “When I sent you out without purse, and wallet, and shoes, did you lack anything?” They said, “Nothing.”
35Kisha, Yesu akawauliza wanafunzi wake, "Wakati nilipowatuma bila mfuko wa fedha wala mkoba wala viatu, mlitindikiwa chochote?" Wakajibu, "La."
36Then he said to them, “But now, whoever has a purse, let him take it, and likewise a wallet. Whoever has none, let him sell his cloak, and buy a sword.
36Naye akawaambia, "Lakini sasa, yule aliye na mfuko wa fedha auchukue; na aliye na mkoba, hali kadhalika. Na yeyote asiye na upanga, auze koti lake anunue mmoja.
37 For I tell you that this which is written must still be fulfilled in me: ‘He was counted with transgressors.’ For that which concerns me has an end.”
37Maana nawaambieni, haya maneno ya Maandiko Matakatifu: Aliwekwa kundi moja na wahalifu, ni lazima yatimie. Naam, yale yanayonihusu yanafikia ukamilifu wake."
38They said, “Lord, behold, here are two swords.” He said to them, “That is enough.”
38Nao wakasema, "Bwana, tazama; hapa kuna panga mbili." Naye akasema, "Basi!"
39He came out, and went, as his custom was, to the Mount of Olives. His disciples also followed him.
39Yesu akatoka, na kama ilivyokuwa desturi yake, akaenda katika mlima wa Mizeituni; wanafunzi wake wakamfuata.
40When he was at the place, he said to them, “Pray that you don’t enter into temptation.”
40Alipofika huko akawaambia, "Salini, msije mkaingia katika kishawishi."
41He was withdrawn from them about a stone’s throw, and he knelt down and prayed,
41Kisha akawaacha, akaenda umbali wa mtu kuweza kutupa jiwe, akapiga magoti, akasali:
42saying, “Father, if you are willing, remove this cup from me. Nevertheless, not my will, but yours, be done.”
42"Baba, kama wapenda, ukiondoe kwangu kikombe hiki; hata hivyo, mapenzi yako yatimizwe, wala siyo yangu."
43An angel from heaven appeared to him, strengthening him.
43Hapo, malaika kutoka mbinguni, akamtokea ili kumtia moyo.
44Being in agony he prayed more earnestly. His sweat became like great drops of blood falling down on the ground.
44Akiwa katika uchungu mkubwa, alisali kwa bidii zaidi; na jasho likamtoka, kama matone ya damu, likatiririka mpaka chini.
45When he rose up from his prayer, he came to the disciples, and found them sleeping because of grief,
45Baada ya kusali, aliwarudia wanafunzi wake, akawakuta wamelala, kwani walikuwa na huzuni.
46and said to them, “Why do you sleep? Rise and pray that you may not enter into temptation.”
46Akawaambia, "Mbona mnalala? Amkeni msali, msije mkaingia katika kishawishi."
47While he was still speaking, behold, a multitude, and he who was called Judas, one of the twelve, was leading them. He came near to Jesus to kiss him.
47Alipokuwa bado anaongea, kundi la watu likaja likiongozwa na yule aliyeitwa Yuda, mmoja wa wale mitume kumi na wawili. Yuda akaenda kumsalimu Yesu kwa kumbusu.
48But Jesus said to him, “Judas, do you betray the Son of Man with a kiss?”
48Lakini Yesu akamwambia, "Yuda! Je, unamsaliti Mwana wa Mtu kwa kumbusu?"
49When those who were around him saw what was about to happen, they said to him, “Lord, shall we strike with the sword?”
49Wale wanafunzi wake walipoona hayo wakasema, "Bwana, tutumie panga zetu?"
50A certain one of them struck the servant of the high priest, and cut off his right ear.
50Na mmoja wao akampiga upanga mtumishi wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio lake la kulia.
51But Jesus answered, “Let me at least do this” —and he touched his ear, and healed him.
51Hapo, Yesu akasema, "Acha! Hii inatosha." Akaligusa sikio la mtu huyo akaliponya.
52Jesus said to the chief priests, captains of the temple, and elders, who had come against him, “Have you come out as against a robber, with swords and clubs?
52Kisha Yesu akawaambia makuhani wakuu, wakubwa wa walinzi wa Hekalu na wazee waliokuja kumkamata: "Je, mmekuja na mapanga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyang'anyi?
53 When I was with you in the temple daily, you didn’t stretch out your hands against me. But this is your hour, and the power of darkness.”
53Nilipokuwa pamoja nanyi kila siku Hekaluni hamkunitia nguvuni. Lakini, huu ndio wakati wenu hasa, ndio wakati wa utawala wa giza."
54They seized him, and led him away, and brought him into the high priest’s house. But Peter followed from a distance.
54Basi, wakamkamata, wakamchukua na kwenda naye nyumbani kwa Kuhani Mkuu. Petro akawa anamfuata nyuma kwa mbali.
55When they had kindled a fire in the middle of the courtyard, and had sat down together, Peter sat among them.
55Moto ulikuwa umewashwa katikati ya ua, nao wakawa wameketi pamoja Petro akiwa miongoni mwao.
56A certain servant girl saw him as he sat in the light, and looking intently at him, said, “This man also was with him.”
56Mjakazi mmoja alipomwona Petro ameketi karibu na moto, akamkodolea macho, akasema, "Mtu huyu alikuwa pia pamoja na Yesu."
57He denied Jesus, saying, “Woman, I don’t know him.”
57Lakini Petro akakana akisema, "Wee! simjui mimi."
58After a little while someone else saw him, and said, “You also are one of them!” But Peter answered, “Man, I am not!”
58Baadaye kidogo, mtu mwingine akamwona Petro, akasema, "Wewe ni mmoja wao." Lakini Petro akajibu "Bwana we; si mimi!"
59After about one hour passed, another confidently affirmed, saying, “Truly this man also was with him, for he is a Galilean!”
59Kama saa moja baadaye, mtu mwingine akasisitiza, "Hakika huyu alikuwa pamoja naye; ametoka Galilaya ati."
60But Peter said, “Man, I don’t know what you are talking about!” Immediately, while he was still speaking, a rooster crowed.
60Lakini Petro akasema, "Bwana wee; sijui hata unachosema!" Na papo hapo, akiwa bado anaongea, jogoo akawika.
61The Lord turned, and looked at Peter. Then Peter remembered the Lord’s word, how he said to him, “Before the rooster crows you will deny me three times.”
61Bwana akageuka na kumtazama Petro, naye Petro akakumbuka yale aliyokuwa ameambiwa na Bwana: "Leo kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu."
62He went out, and wept bitterly.
62Hapo akatoka nje, akalia sana.
63The men who held Jesus mocked him and beat him.
63Wale watu waliokuwa wanamchunga Yesu, walimpiga na kumdhihaki.
64Having blindfolded him, they struck him on the face and asked him, “Prophesy! Who is the one who struck you?”
64Walimfunga kitambaa usoni, wakawa wanamwuliza, "Ni nani aliyekupiga? Hebu bashiri tuone!"
65They spoke many other things against him, insulting him.
65Wakamtolea maneno mengi ya matusi.
66As soon as it was day, the assembly of the elders of the people was gathered together, both chief priests and scribes, and they led him away into their council, saying,
66Kulipokucha, kikao cha wazee wa watu kilifanyika, ambacho kilihudhuriwa na makuhani wakuu na walimu wa Sheria. Yesu akaletwa mbele ya Baraza hilo.
67“If you are the Christ, tell us.” But he said to them, “If I tell you, you won’t believe,
67Nao wakamwambia, "Twambie! Je, wewe ndiwe Kristo?" Lakini Yesu akawaambia, "Hata kama nikiwaambieni, hamtasadiki;
68 and if I ask, you will in no way answer me or let me go.
68na hata kama nikiwaulizeni swali, hamtanijibu.
69 From now on, the Son of Man will be seated at the right hand of the power of God.”
69Lakini tangu sasa, Mwana wa Mtu atakuwa ameketi upande wa kulia wa Mungu Mwenyezi."
70They all said, “Are you then the Son of God?” He said to them, “You say it, because I am.”
70Hapo wote wakasema, "Ndiyo kusema wewe ni Mwana wa Mungu?" Naye akasema, "Ninyi mnasema kwamba mimi ndiye."
71They said, “Why do we need any more witness? For we ourselves have heard from his own mouth!”
71Nao wakasema, "Je, tunahitaji ushahidi mwingine? Sisi wenyewe tumesikia akisema kwa mdomo wake mwenyewe."