1Therefore I urge you, brothers, by the mercies of God, to present your bodies a living sacrifice, holy, acceptable to God, which is your spiritual service.
1Kwa hiyo, ndugu zangu, maadam Mungu ni mwenye huruma nyingi, nawasihi kwa moyo wote: jitoleeni nafsi zenu kwa Mungu kama tambiko iliyo hai, takatifu na yenye kupendeza. Hii ndiyo njia yenu halisi ya kumwabudu.
2Don’t be conformed to this world, but be transformed by the renewing of your mind, so that you may prove what is the good, well-pleasing, and perfect will of God.
2Msiige mitindo ya ulimwengu huu, bali Mungu afanye mabadiliko ndani yenu kwa kuzigeuza fikira zenu. Hapo ndipo mtakapoweza kuyajua mapenzi ya Mungu, kutambua jambo lililo jema, linalompendeza na kamilifu.
3For I say, through the grace that was given me, to every man who is among you, not to think of himself more highly than he ought to think; but to think reasonably, as God has apportioned to each person a measure of faith.
3Kutokana na neema aliyonijalia Mungu, nawaambieni ninyi nyote: msijione kuwa ni kitu zaidi kuliko mnavyopaswa kuwa. Fikira zenu na ziwe na kiasi kufuatana na kipimo cha imani Mungu aliyomgawia kila mmoja.
4For even as we have many members in one body, and all the members don’t have the same function,
4Mwili una viungo vingi, kila kimoja na kazi yake.
5so we, who are many, are one body in Christ, and individually members one of another.
5Hali kadhalika ingawa sisi ni wengi, tu mwili mmoja kwa kuungana na Kristo, na kila mmoja ni kiungo cha mwenzake.
6Having gifts differing according to the grace that was given to us, if prophecy, let us prophesy according to the proportion of our faith;
6Basi, tunavyo vipaji mbalimbali kufuatana na neema tuliyopewa. Mwenye kipaji cha unabii na akitumie kadiri ya imani yake.
7or service, let us give ourselves to service; or he who teaches, to his teaching;
7Mwenye kipaji cha utumishi na atumikie. mwenye kipaji cha kufundisha na afundishe.
8or he who exhorts, to his exhorting: he who gives, let him do it with liberality; he who rules, with diligence; he who shows mercy, with cheerfulness.
8Mwenye kipaji cha kuwafariji wengine na afanye hivyo. Mwenye kumgawia mwenzake alicho nacho na afanye hivyo kwa ukarimu. Msimamizi na asimamie kwa bidii; naye mwenye kutenda jambo la huruma na afanye hivyo kwa furaha.
9Let love be without hypocrisy. Abhor that which is evil. Cling to that which is good.
9Mapendo yenu na yawe bila unafiki wowote. Chukieni jambo lolote ovu, zingatieni jema.
10In love of the brothers be tenderly affectionate one to another; in honor preferring one another;
10Pendaneni kidugu; kila mmoja amfikirie mwenzake kwanza kwa heshima.
11not lagging in diligence; fervent in spirit; serving the Lord;
11Msilegee katika bidii, muwe wachangamfu rohoni katika kumtumikia Bwana.
12rejoicing in hope; enduring in troubles; continuing steadfastly in prayer;
12Tumaini lenu liwaweke daima wenye furaha; muwe na saburi katika shida na kusali daima.
13contributing to the needs of the saints; given to hospitality.
13Wasaidieni watu wa Mungu katika mahitaji yao; wapokeeni wageni kwa ukarimu.
14Bless those who persecute you; bless, and don’t curse.
14Watakieni baraka wote wanaowadhulumu ninyi; naam, watakieni baraka na wala msiwalaani.
15Rejoice with those who rejoice. Weep with those who weep.
15Furahini pamoja na wanaofurahi, lieni pamoja na wanaolia.
16Be of the same mind one toward another. Don’t set your mind on high things, but associate with the humble. Don’t be wise in your own conceits.
16Muwe na wema uleule kwa kila mtu. Msijitakie makuu, bali jishugulisheni na watu wadogo. Msijione kuwa wenye hekima sana.
17Repay no one evil for evil. Respect what is honorable in the sight of all men.
17Msilipe ovu kwa ovu. Zingatieni mambo mema mbele ya wote.
18If it is possible, as much as it is up to you, be at peace with all men.
18Kadiri inavyowezekana kwa upande wenu, muwe na amani na watu wote.
19Don’t seek revenge yourselves, beloved, but give place to God’s wrath. For it is written, “Vengeance belongs to me; I will repay, says the Lord.” Deuteronomy 32:35
19Wapenzi wangu, msilipize kisasi, bali mwachieni Mungu jambo hilo; maana Maandiko Matakatifu yasema: "Kulipiza kisasi ni shauri langu; mimi nitalipiza asema Bwana."
20Therefore “If your enemy is hungry, feed him. If he is thirsty, give him a drink; for in doing so, you will heap coals of fire on his head.” Proverbs 25:21-22
20Tena, Maandiko yasema: "Adui yako akiwa na njaa, mpe chakula; akiwa na kiu, mpe kinywaji. Maana kwa kufanya hivyo utamfanya apate aibu kali kama makaa ya moto juu ya kichwa chake."
21Don’t be overcome by evil, but overcome evil with good.
21Usikubali kushindwa na ubaya, bali ushinde ubaya kwa wema.