1捐钱给圣徒的事
1Sasa, yahusu ule mchango kwa ajili ya watu wa Mungu: fanyeni kama nilivyoyaagiza makanisa ya Galatia.
2每逢七日的第一日,你们各人要按着自己的收入抽一些出来留着,免得我来的时候才现凑。
2Kila Jumapili kila mmoja wenu atenge kiasi cha fedha kadiri ya mapato yake, ili kusiwe na haja ya kufanya mchango wakati nitakapokuja.
3我来到之后,你们选中了什么人,我就派他们带着书信,把你们的捐款送到耶路撒冷去。
3Wakati nitakapokuja kwenu, nitawatuma wale mtakaowachagua miongoni mwenu wapeleke barua na zawadi zenu Yerusalemu.
4如果我也应该去,他们就可以和我一同去。
4Kama itafaa nami niende, basi, watakwenda pamoja nami.
5保罗的行程我现在正要路过马其顿。过了马其顿,我就会到你们那里去。
5Nitakuja kwenu, baada ya kupitia Makedonia--maana nataraji kupitia Makedonia.
6我也许会和你们同住一些时候,甚至和你们一同过冬;这样,我无论要到哪里去,你们都可以给我送行。
6Labda nitakaa kwenu kwa muda fulani, au huenda nitakaa pamoja nanyi wakati wote wa baridi, ili mpate kunisaidia niendelee na safari yangu kokote nitakakokwenda.
7我不愿意只是顺路见见你们,主若许可,我盼望和你们同住一个时期。
7Sipendi kupita kwenu harakaharaka na kuendelea na safari. Natumaini kukaa kwenu kwa kitambo fulani, Bwana akiniruhusu.
8不过我要在以弗所住到五旬节,
8Lakini nitabaki hapa Efeso mpaka siku ya Pentekoste.
9因为这里有又宽大又有果效的门为我开了,同时反对的人也很多。
9Mlango uko wazi kabisa kwa ajili ya kazi yangu muhimu hapa, ingawa wapinzani nao ni wengi.
10如果提摩太来了,你们务要使他在你们那里不会惧怕,因为他像我一样是作主的工作的。
10Timotheo akija, angalieni asiwe na hofu yoyote wakati yupo kati yenu, kwani anafanya kazi ya Bwana kama mimi.
11所以,谁也不要小看他。你们要送他平平安安地前行,使他到我这里来,因为我正在等着他和弟兄们一同来。
11Kwa hiyo mtu yeyote asimdharau, ila msaidieni aendelee na safari yake kwa amani ili aweze kurudi kwangu, maana mimi namngojea pamoja na ndugu zetu.
12至于亚波罗弟兄,我曾再三劝他要和弟兄们一同到你们那里去;但他不愿意现在就去,机会到了,他是会去的。
12Kuhusu ndugu Apolo, nimemsihi sana aje kwenu pamoja na ndugu wengine, lakini hapendelei kabisa kuja sasa ila atakuja mara itakapowezekana.
13劝勉和问安你们要警醒,要在信仰上站立得稳,要作大丈夫,要刚强。
13Kesheni, simameni imara katika imani, muwe hodari na wenye nguvu.
14你们所作的一切,都要凭爱心去作。
14Kila mfanyacho kifanyike kwa upendo.
15弟兄们,你们知道司提反一家人是亚该亚初结的果子,他们专心地服事圣徒。
15Ndugu, mnaifahamu jamaa ya Stefana; wao ni watu wa kwanza kabisa kuipokea imani ya Kikristo katika Akaya, na wamejitolea kuwatumikia watu wa Mungu. Ninawasihi ninyi ndugu zangu,
16我劝你们要顺服这样的人,和所有与他们一同工作一同劳苦的人。
16muufuate uongozi wa watu kama hao, na uongozi wa kila mtu afanyaye kazi na kutumikia pamoja nao.
17司提反、福徒拿都和亚该古都来了,所以我很快乐,因为他们补上了你们的不足,
17Nafurahi sana kwamba Stefana, Fortunato na Akaiko wamefika; wamelijaza pengo lililokuwako kwa kutokuwako kwenu.
18使我和你们的心都得着畅快。这样的人你们要敬重他们。
18Wameiburudisha roho yangu na yenu pia. Kwa hiyo inafaa kuwakumbuka watu wa namna hii.
19亚西亚的众教会都问候你们。亚居拉和百基拉,以及他们家里的教会在主里再三问候你们。
19Makanisa yote ya Asia yanawasalimuni. Akula na Priskila pamoja na watu wote wa Mungu walio nyumbani mwao wanawasalimuni sana katika Bwana.
20所有的弟兄都问候你们。你们要用圣洁的亲嘴彼此问安。
20Ndugu wote wanawasalimuni. Nanyi salimianeni kwa ishara ya mapendo ya Mungu.
21我保罗亲笔问候你们。
21Mimi Paulo nawasalimuni, nikiandika kwa mkono wangu mwenyewe.
22如果有人不爱主,他就该受咒诅。主啊,愿你来!
22Yeyote asiyempenda Bwana, na alaaniwe. MARANA THA--BWANA, njoo!
23愿主耶稣基督的恩惠与你们同在。
23Neema ya Bwana Yesu iwe nanyi.
24我的爱在基督耶稣里也与你们同在。(有古卷加“阿们”。)
24Mapendo yangu yawe kwenu katika kuungana na Kristo Yesu.