聖經新譯本 (Simplified)

Swahili: New Testament

1 Peter

1

1问安
1Mimi Petro, mtume wa Yesu Kristo nawaandikia ninyi wateule wa Mungu Baba, ambao mmetawanyika na mnaishi kama wakimbizi huko Ponto, Galatia, Kapadokia, Asia na Bithunia.
2就是照着父 神的预知蒙拣选,借着圣灵得成圣洁,因而顺服,并且被耶稣基督的血洒过的人。愿恩惠平安多多地加给你们。
2Mungu Baba aliwateua ninyi kufuatana na kusudi lake, na mmefanywa watakatifu na Roho, mpate kumtii Yesu Kristo na kusafishwa kwa damu yake. Nawatakieni neema na amani tele.
3信心经过考验比金子更宝贵我们主耶稣基督的父 神是应当称颂的。他照着自己的大怜悯,借着耶稣基督从死人中复活,重生了我们,使我们有永活的盼望,
3Asifiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo! Kwa huruma yake kuu alitufanya tuzaliwe upya kwa kumfufua Yesu kutoka wafu. Ametujalia tumaini lenye uzima,
4可以得着不能朽坏、不能玷污、不能衰残,为你们存留在天上的基业,
4na hivyo tunatazamia kupata baraka zile ambazo Mungu aliwawekea watu wake. Mungu amewawekeeni baraka hizo mbinguni ambako haziwezi kuoza au kuharibika au kufifia.
5就是你们这因信蒙 神能力保守的人,得着预备在末世要显现的救恩。
5Hizo zitakuwa zenu ninyi ambao kwa imani mnalindwa salama kwa nguvu ya Mungu kwa ajili ya wokovu ambao uko tayari kufunuliwa mwishoni mwa nyakati.
6因此,你们要喜乐。然而,你们现今在各种试炼中或许暂时会难过,
6Furahini kuhusu jambo hilo, ijapokuwa sasa, kwa kitambo kidogo, itawabidi kuhuzunika kwa sababu ya majaribio mbalimbali mnayoteseka.
7是要叫你们的信心经过试验,就比那被火炼过,仍会朽坏的金子更宝贵,可以在耶稣基督显现的时候,得着称赞、荣耀和尊贵。
7Shabaha yake ni kuthibitisha imani yenu. Hata dhahabu yenyewe ambayo huharibika, hujaribiwa kwa moto; hali kadhalika na imani yenu ambayo ni ya thamani zaidi kuliko dhahabu, ni lazima ijaribiwe ipate kuwa thabiti. Hapo mtapokea sifa na utukufu na heshima Siku ile Yesu Kristo atakapofunuliwa.
8你们虽然没有见过他,却爱他;现在虽然不能看见他,却信他。因此,你们就有无法形容、满有荣耀的大喜乐,
8Ninyi mnampenda ingawaje hamjamwona, na mnamwamini ingawa hamumwoni sasa. Hivyo, mnafurahi kwa furaha tukufu isiyoelezeka,
9得到你们信心的效果,就是灵魂得救。
9kwa sababu mnapokea wokovu wa roho zenu ambao ni lengo la imani yenu.
10论到这救恩,那预言你们要得恩典的众先知,都寻求考察过,
10Manabii walipeleleza kwa makini na kufanya uchunguzi juu ya wokovu huo, wakabashiri juu ya neema hiyo ambayo ninyi mngepewa.
11就是把他们心里基督的灵所预先见证,关于基督要受苦难后来得荣耀,是在什么时候和怎样的情况加以考察。
11Walijaribu kujua nyakati na mazingira ya tukio hilo, yaani wakati alioudokezea Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, akibashiri juu ya mateso yatakayompata Kristo na utukufu utakaofuata.
12他们蒙了启示,为这些事效力,并不是为自己,而是为你们。现在,借着传福音给你们的人,靠着从天上差来的圣灵,把这些事传给了你们;甚至天使也很想详细察看这些事。
12Mungu aliwafunulia kwamba wakati walipokuwa wanasema juu ya hayo mambo ambayo ninyi mmekwisha sikia sasa kutoka kwa wale wajumbe waliowatangazieni Habari Njema kwa nguvu ya Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni, hiyo kazi yao haikuwa kwa faida yao wenyewe, bali kwa ajili yenu. Hayo ndiyo mambo ambayo hata malaika wangependa kuyafahamu.
13你们要圣洁所以要准备好你们的心,警醒谨慎,专心盼望耶稣基督显现的时候所要带给你们的恩典。
13Kwa hiyo, basi, muwe tayari kabisa kwa nia, na kukesha. Wekeni tumaini lenu lote katika baraka ile mtakayopewa wakati Yesu Kristo atakapoonekana!
14你们既是顺服的儿女,就不要再效法从前无知的时候放纵私欲的生活。
14Kama watoto wa Mungu wenye utii, msikubali kamwe kufuata tena tamaa mbaya mlizokuwa nazo wakati mlipokuwa wajinga.
15那召你们的既是圣洁的,你们在一切所行的事上也要圣洁。
15Bali mnapaswa kuwa watakatifu katika mwenendo wenu wote, kama vile yule aliyewaiteni ni mtakatifu.
16因为圣经上记着说:“你们要圣洁,因为我是圣洁的。”
16Maandiko yasema: "Muwe watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu."
17你们既称那不偏待人、按各人行为审判的主为父,就当存敬畏的心,过你们寄居的日子;
17Mnapomtaja Mungu ninyi humwita Baba. Basi, jueni kwamba yeye humhukumu kila mmoja kadiri ya matendo yake, bila ubaguzi. Hivyo tumieni wakati wenu uliowabakia hapa ugenini katika kumcha Mungu.
18因为知道你们得赎,脱去你们祖先传下的妄行,不是凭着能坏的金银等物,
18Maana mnajua kwamba ninyi mlikombolewa katika mwenendo wenu usiofaa ambao mliupokea kutoka kwa wazee wenu, si kwa vitu vyenye kuharibika: kwa fedha na dhahabu;
19而是凭着基督的宝血,就像无瑕疵无玷污的羊羔的血。
19bali mlikombolewa kwa damu tukufu ya Kristo, ambaye alikuwa kama mwana kondoo asiye na dosari wala doa.
20基督是在创立世界以前,是 神所预知的,却在这末后的世代才为你们显现出来。
20Yeye alikuwa ameteuliwa na Mungu kabla ya ulimwengu kuumbwa, akafunuliwa siku hizi za mwisho kwa ajili yenu.
21借着他,你们信那使他从死人中复活、又给他荣耀的 神,叫你们的信心和盼望都在于 神。
21Kwa njia yake, ninyi mnamwamini Mungu aliyemfufua kutoka wafu na kumpa utukufu; na hivyo imani na matumaini yenu yako kwa Mungu.
22主的道永远长存你们既因顺从真理,洁净了自己的心灵,以致能真诚地爱弟兄,就应当从清洁的心里彼此切实相爱。
22Maadamu sasa, kwa kuutii ukweli, ninyi mmezitakasa roho zenu na kuwapenda wenzenu bila unafiki, basi, pendaneni kwa moyo wote.
23你们得了重生,并不是由于能坏的种子,却是由于不能朽坏的,就是借着 神永活长存的道。
23Maana kwa njia ya neno hai la Mungu, ninyi mmezaliwa upya, si kama watoto wa baba awezaye kufa, bali baba asiyekufa milele.
24因为“所有的人(“人”原文作“肉体”),尽都如草,他们的荣美,都像草上的花;草必枯干,花必凋谢,
24Kama Maandiko yasemavyo: "Kila binadamu ni kama nyasi, na utukufu wake wote ni kama maua ya porini. Nyasi hunyauka na maua huanguka.
25唯有主的道,永远长存。”所传给你们的福音就是这道。
25Lakini neno la Bwana hudumu milele." Neno hilo ni hiyo Habari Njema iliyohubiriwa kwenu.