1保罗阐明他的权柄与工作
1Mimi Paulo mwenyewe ambaye naonekana kuwa mpole nikiwa pamoja nanyi, lakini mkali wakati nikiwa mbali nanyi, nawasihini kwa huruma na wema wake Kristo.
2求你们使我在你们那里的时候,不要满有自信地放胆对你们,我认为要以这样的自信,勇敢地对付那些以为我们是照着世俗的标准(“世俗的标准”原文作“肉体”)行事的人。
2Nawaombeni msinisababishe kuwa mkali wakati nitakapokuja, maana nina hakika naweza kuwa mkali kwa wote wale wanaotudhania kwamba tunaishi kidunia.
3我们虽然在世上行事,却不是按照世俗的方式作战,
3Kweli tunaishi duniani, lakini hatupigani vita kidunia.
4因为我们作战所用的兵器,不是属于这世界的,而是在 神面前有能力的,可以攻陷坚固的堡垒,
4Maana, silaha tunazotumia katika vita vyetu si silaha za kidunia, ila ni nguvu za Mungu zenye kuharibu ngome zote. Tunaharibu hoja zote za uongo,
5攻破诡辩,和做来阻挡人认识 神的一切高墙,并且把一切心意夺回来,顺服基督。
5na kubomoa kila kizuizi cha majivuno kilichowekwa kuipinga elimu ya Mungu; tunaziteka fikira zote na kuzifanya zimtii Kristo.
6我们已经准备好了,等你们完全顺服的时候,就惩罚所有不顺从的人。
6Mkisha kuwa wakamilifu katika kutii, sisi tuko tayari kuadhibu kila namna ya kutotii.
7你们看事情,只看表面。如果有人自信是属于基督的,他就应该再想一想:他是属于基督的,同样,我们也是属于基督的。
7Ninyi hutazama mambo kwa nje tu. Je, yupo mtu yeyote anayedhani kwamba yeye ni wa Kristo? Sawa! Basi, afikirie vilevile kwamba sisi pia ni wa Kristo kama yeye alivyo wa Kristo.
8主把权柄赐给我们,是为了要造就你们,不是要破坏你们,就算我为这权柄夸口过分了一点,也不会觉得惭愧。
8Hata kama nimezidi katika kujivuna kwangu juu ya ule uwezo aliotupa--uwezo wa kuwajenga na sio wa kubomoa--hata hivyo sijutii hata kidogo.
9不要以为我写信是用来吓你们。
9Sipendi mfikiri kwamba nataka kuwatisha ninyi kwa barua zangu.
10因为有人说:“他的信又严厉又强硬,他本人却气貌不扬,言语粗俗。”
10Mtu anaweza kusema: "Barua za Paulo ni kali na zenye maneno mazito, lakini yeye mwenyewe anapokuwa pamoja nasi ni mtu dhaifu, na hata anapoongea maneno yake ni kama si kitu."
11说这话的人要想一想,我们不在你们那里的时候,信上怎样写,我们来到的时候也会怎样作。
11Mtu asemaye hivyo heri akumbuke kwamba hakuna tofauti ya yale tunayoandika katika barua wakati tuko mbali, na yale tutakayofanya wakati tutakapokuwa nanyi.
12我们不敢和那些自我推荐的人相提并论;他们拿自己来量自己,拿自己来比自己,实在不大聪明。
12Kwa vyovyote hatungethubutu kujiweka au kujilinganisha na wale watu wanaojisifia wenyewe. Watu wenye kujifanya wao kuwa kipimo cha kujipimia, na watu wanaojilinganisha wenyewe kwa wenyewe, ni wapumbavu.
13我们所夸的,并没有越过范围,而是在 神量给我们的界限之内;这界限一直延伸到你们那里。
13Lakini sisi hatutajivuna kupita kiasi; kujivuna huko kutabaki katika kile kipimo cha kazi aliyotukabidhi Mungu, kazi ambayo tunaifanya pia kwenu.
14如果我们没有到过你们那里,现在就自夸得过分了;但事实上,我们早就把基督的福音传到你们那里了。
14Na kwa vile ninyi mu katika mipaka hiyo, hatukuipita tulipokuja kwenu, tukiwaleteeni Habari Njema juu ya Kristo.
15我们并没有越过范围,拿别人的劳苦来夸口。我们盼望随着你们信心的增长,我们的界限就因你们而大大扩展,
15Basi, hatujivunii kazi waliyofanya wengine zaidi ya kipimo tulichopewa; ila tunatumaini kwamba imani yenu itazidi miongoni mwenu kufuatana na kipimo alichotuwekea Mungu.
16使我们可以把福音传到你们以外的地方。别人在他的界限以内所完成的工作,我们不会拿来夸口的。
16Hapo tutaweza kuihubiri Habari Njema katika nchi nyingine, mbali nanyi; na haitakuwa shauri la kujivunia kazi waliyofanya watu wengine mahali pengine.
17夸口的应当靠着主夸口,
17Lakini kama yasemavyo Maandiko: "Mwenye kuona fahari na aone fahari juu ya alichofanya Bwana."
18因为蒙悦纳的,不是自我推荐的人,而是主所推荐的人。
18Anayekubaliwa si yule anayejisifu mwenyewe, bali yule anayesifiwa na Bwana.