聖經新譯本 (Simplified)

Swahili: New Testament

2 Peter

3

1必有人不信主再来的应许
1Wapenzi wangu, hii ni barua ya pili ninayowaandikia. Katika barua hizo mbili nimejaribu kufufua fikira safi akilini mwenu kwa kuwakumbusheni mambo haya.
2叫你们记起圣先知说过的话,和主救主借着使徒传给你们的诫命。
2Napenda mkumbuke maneno yaliyosemwa na manabii watakatifu, na ile amri ya Bwana na Mwokozi mliyopewa na mitume wenu.
3最重要的,你们应当知道:在末后的日子,必定有好讥笑的人出来,随着自己的私欲讥笑说:
3Awali ya yote jueni kwamba siku za mwisho watakuja watu ambao mienendo yao inatawaliwa na tamaa zao mbaya. Watawadhihaki ninyi
4“他要降临的应许在哪里呢?因为自从列祖睡了以来,万物依然存在,与起初创造的时候一样。”
4na kusema: "Aliahidi kwamba atakuja! Je, sasa yuko wapi? Mambo ni yaleyale tangu babu zetu walipokufa; hali ya vitu ni ileile kama ilivyokuwa mwanzo wa ulimwengu!"
5他们故意忘记这事:在太古的时候,因着 神的话,就有了天,和从水而出、借水而成的地。
5Watu hao, kwa makusudi, husahau kwamba zamani Mungu alinena, nazo mbingu na nchi zikaumbwa. Dunia iliumbwa kutoka katika maji na kwa maji;
6当时的世界,因被水淹没而消灭了。
6na kwa maji hayo, yaani yale maji ya gharika kuu, dunia ya wakati ule iliangamizwa.
7但现在的天地,还是因着同样的话可以存留,直到不敬虔的人受审判和遭灭亡的日子,用火焚烧。
7Lakini mbingu na nchi za sasa zahifadhiwa kwa neno la Mungu kwa ajili ya kuharibiwa kwa moto. Zimewekwa kwa ajili ya Siku ile ambapo watu wasiomcha Mungu watahukumiwa na kuangamizwa.
8主必再来亲爱的,这一件事你们不可忘记:在主看来,一日如千年,千年如一日。
8Lakini, wapenzi wangu, msisahau kitu kimoja! Mbele ya Bwana, hakuna tofauti kati ya siku moja na miaka elfu; kwake yote ni mamoja.
9主决不耽延他的应许,像有些人以为他是耽延的一样;其实他是宽容你们,不愿有一人灭亡,却愿人人都悔改。
9Bwana hakawii kutimiza yale aliyoahidi kama watu wengine wanavyofikiri kuwa atakawia. Yeye ana saburi kwa ajili yenu, maana hapendi hata mmoja wenu apotee, bali huwavuta wote wapate kutubu.
10但主的日子必要像贼一样来到。在那日,天必轰然一声地消失,所有元素都因烈火而融化;地和地上所有的,都要被烧毁。
10Siku ya Bwana itakuja kama mwizi. Siku hiyo, mbingu zitatoweka kwa kishindo kikuu; vitu vyake vya asili vitateketezwa kwa moto, nayo dunia itatoweka pamoja na kila kitu kilichomo ndani yake.
11这一切既然都要这样融化,你们应当怎样为人,过着圣洁和敬虔的生活,
11Maadamu kila kitu kitaharibiwa namna hiyo, je, ninyi mnapaswa kuwa watu wa namna gani? Mnapaswa kuishi kitakatifu na kumcha Mungu,
12等候并催促 神的日子降临呢?因为在那日,天要被火焚烧就融化了,所有元素都因烈火而融解!
12mkiingojea Siku ile ya Mungu na kuifanya ije upesi--Siku ambayo mbingu zitateketezwa kwa moto na kuharibiwa, na vitu vyake vya asili vitayeyushwa kwa joto.
13但是我们按照他所应许的,等候新天新地,有公义在那里居住。
13Lakini sisi, kufuatana na ahadi yake, twangojea mbingu mpya na dunia mpya ambayo imejaa uadilifu.
14要在主的恩典和知识上长进所以,亲爱的,你们既然等候这些事,就当殷勤努力,使你们没有污点,没有瑕疵,安然见主。
14Kwa hiyo wapenzi wangu, mkiwa mnangojea Siku ile, fanyeni bidii kuwa safi kabisa bila hatia mbele ya Mungu, na kuwa na amani naye.
15并且要以我们的主恒久忍耐为给人得救的机会,就如我们所亲爱的弟兄保罗,按照所赐给他的智慧,写给你们的一样;
15Mnapaswa kuuona uvumilivu wa Bwana kuwa ni nafasi anayowapeni mpate kuokolewa, kama Paulo ndugu yetu mpenzi alivyowaandikia akitumia hekima aliyopewa na Mungu.
16他在一切书信上,都讲论这些事。在这些书信中,有些难明白的地方,那不学无术和不稳定的人加以曲解,好像曲解别的经书一样,就自取灭亡。
16Hayo ndiyo asemayo katika barua zake zote anapozungumzia suala hilo. Yapo mambo kadhaa katika barua zake yaliyo magumu kuyaelewa, mambo ambayo watu wajinga, wasio na msimamo, huyapotosha kama wanavyopotosha sehemu nyingine za Maandiko Matakatifu. Hivyo wanasababisha maangamizi yao wenyewe.
17所以,亲爱的,你们既然预先知道了,就要谨慎,免得受恶人的错谬引导,就从自己坚固的地步上坠落。
17Lakini ninyi, wapenzi wangu, mmekwisha jua jambo hili. Basi, muwe na tahadhari msije mkapotoshwa na makosa ya waasi, mkaanguka kutoka katika msimamo wenu imara.
18你们却要在我们的主、救主耶稣基督的恩典和知识上长进。愿荣耀归给他,从现在直到永远。阿们。
18Lakini endeleeni kukua katika neema na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu uwe kwake, sasa na hata milele! Amina.