聖經新譯本 (Simplified)

Swahili: New Testament

3 John

1

1问安我这作长老的写信给亲爱的该犹,就是我在真理中所爱的。
1Mimi mzee nakuandikia wewe Gayo, rafiki yangu, ninayekupenda kweli.
2亲爱的,我祝你凡事亨通,身体健壮,正如你的灵魂安泰一样。
2Mpenzi wangu, nakutakia mafanikio mema ya kila aina; nakutakia afya njema ya mwili kama ulivyo nayo rohoni.
3有些弟兄来到,证实你心中存有真理,就是你按真理行事,我就非常欣慰。
3Nimefurahi sana ndugu kadhaa walipofika hapa, wakaiambia juu ya uaminifu wako kuhusu ukweli; naam, wewe unaishi daima katika ukweli.
4我听见我的儿女按真理行事,我的喜乐没有比这更大的了。
4Hakuna kitu kinachonifurahisha zaidi kuliko kusikia kwamba watoto wangu wanaishi katika ukweli.
5称赞该犹接待弟兄亲爱的,你向弟兄所行的,特别是向外地来的弟兄所行的,都是出于忠心。
5Mpenzi wangu, wewe ni mwaminifu kila mara unapowahudumia ndugu, hata kama ni wageni.
6他们在教会面前证实了你的爱;你照着 神所喜悦的,资助他们的旅程,这样是好的。
6Ndugu hao wamelieleza kanisa hapa habari za upendo wako. Tafadhali uwasaidie waendelee na safari yao kwa namna itakayompendeza Mungu,
7因为他们为主的名出外,并没有从教外人接受什么。
7Maana wanaanza safari yao katika utumishi wa Kristo bila kupokea msaada wowote kutoka kwa watu wasioamini.
8所以我们应当接待这样的人,好让我们为了真理成为同工。
8Basi, sisi tunapaswa kuwasaidia watu hawa, ili nasi tupate kushiriki katika kazi yao kwa ajili ya ukweli.
9不要效法恶,应该效法善我曾经略略写信给你那里的教会,但他们中间那好作领袖的丢特腓不接待我们。
9Niliandika barua fupi kwa hilo kanisa; lakini Diotrefe, ambaye hupenda kuwa kiongozi wao, hataki kabisa kunisikiliza.
10因此,我来的时候,必要提起他所作的事,就是他用恶言中伤我们;这还不够,他不但不接待弟兄,还要阻止那些想要接待的人,甚至把他们赶出教会。
10Basi, nitakapokuja nitayafichua mambo yote anayofanya, maneno mabaya anayotutolea na uongo anaosema juu yetu. Isitoshe, yeye hukataa kuwakaribisha hao ndugu walio safarini, na hata huwazuia watu wengine wanaotaka kuwakaribisha, na hujaribu kuwafukuzia nje ya kanisa.
11亲爱的,不要效法恶,应该效法善。行善的属于 神,作恶的没有见过 神。
11Mpenzi wangu, usifuate mfano mbaya, bali mfano mwema. Kila atendaye mema ni wa Mungu; lakini anayetenda mabaya hajapata kumwona Mungu.
12低米丢行善,有众人为他作证,真理本身也为他作证。我们也为他作证,你知道我们的见证是真的。
12Kila mtu anamsifu Demetrio; naam, ukweli wenyewe unamsifu. Nasi pia tunatoa ushahidi wetu juu yake, nawe wajua kwamba tunachosema ni kweli.
13问候的话我还有许多话要写给你,可是我不愿借用笔墨。
13Ninayo bado mengi ya kukwambia, lakini sipendi kuyaandika kwa kalamu na wino.
14我盼望很快就见到你,当面谈谈。 [ (III John 1:15) 愿你平安。这里的朋友都问候你。请你一一提名问候你那里的朋友。 ]
14Natumaini kukuona karibuni na hapo tutazungumza ana kwa ana. (G1-15) Nakutakia amani. Rafiki zako wanakusalimu. Wasalimu rafiki zetu wote kila mmoja binafsi.