1在哥林多
1Baada ya hayo, Paulo aliondoka Athene, akaenda Korintho.
2遇见一个生在本都的犹太人,名叫亚居拉。因为革老丢下令所有的犹太人都要离开罗马,所以亚居拉最近同他的妻子百基拉从意大利来了,保罗就去找他们。
2Huko Korintho, alimkuta Myahudi mmoja aitwaye Akula, mzaliwa wa Ponto. Akula pamoja na mkewe aitwaye Priskila, walikuwa wamerudi kutoka Italia siku hizohizo kwa sababu Kaisari Klaudio alikuwa ameamuru Wayahudi wote waondoke Roma. Paulo alikwenda kuwaona,
3他们是以做帐棚为业的,因为是同业,保罗就与他们同住,一同工作。
3na kwa vile wao walikuwa mafundi wa kushona mahema kama alivyokuwa yeye, Paulo alikaa nao akafanya kazi.
4每逢安息日,保罗在会堂辩论,劝导犹太人和希腊人归主。
4Kila Sabato alifanya majadiliano katika sunagogi akijaribu kuwavuta Wayahudi na Wagiriki.
5西拉和提摩太从马其顿下来的时候,保罗就专心传扬主的道,向犹太人极力证明耶稣是基督。
5Baada ya Sila na Timotheo kuwasili kutoka Makedonia, Paulo alianza kutumia wakati wake wote kwa ajili ya kuhubiri, akawathibitishia Wayahudi kwamba Yesu ndiye Kristo.
6但是他们抗拒、亵渎,保罗就抖着衣服,对他们说:“你们的罪你们自己承担,这与我无关。从今以后,我要到外族人那里去了。”
6Walipompinga na kuanza kumtukana, aliyakung'uta mavazi yake mbele yao akisema, "Mkipotea ni shauri lenu wenyewe; mimi sina lawama yoyote juu ya jambo hilo. Na tangu sasa nitawaendea watu na mataifa mengine."
7他离开那里,到了提多.犹士都的家去。这人是敬拜 神的,他的家靠近会堂。
7Basi, akatoka hapo akaenda kukaa nyumbani kwa mtu mmoja mcha Mungu aitwaye Tito Yusto. Nyumba yake Tito ilikuwa karibu na lile sunagogi.
8会堂主管基利司布和他全家都信了主,许多哥林多人也听了道,信了主,而且受了洗。
8Lakini Krispo, mkuu wa sunagogi, alimwamini Bwana yeye pamoja na jamaa yake yote. Wakorintho wengi waliusikiliza ujumbe huo, wakaamini na kubatizwa.
9夜里,主借着异象对保罗说:“不要怕,只管讲,不要闭口!
9Siku moja usiku, Bwana alimwambia Paulo katika maono: "Usiogope, endelea kuhubiri tu bila kufa moyo,
10有我与你同在,必定没有人能害你,因为在这城里有许多属我的人。”
10maana mimi niko pamoja nawe. Hakuna mtu atakayejaribu kukudhuru maana hapa mjini pana watu wengi walio upande wangu."
11保罗在那里住了一年零六个月,把 神的道教导他们。
11Basi, Paulo alikaa huko akifundisha neno la Mungu kati yao kwa muda wa mwaka mmoja na nusu.
12当迦流作亚该亚省长的时候,犹太人一致起来攻击保罗,拉他到审判台前,
12Lakini wakati Galio alipokuwa mkuu wa mkoa wa Akaya, Wayahudi walimvamia Paulo kwa pamoja na kumpeleka mahakamani.
13说:“这个人劝人不照着律法去敬拜 神。”
13Wakasema, "Tunamshtaki mtu huyu kwa sababu ya kuwashawishi watu wamwabudu Mungu kwa namna inayopingana na Sheria."
14保罗刚要开口,迦流就对犹太人说:“犹太人啊,如果有犯法或邪恶的罪行,我当然要耐心听你们;
14Kabla tu Paulo hajaanza kusema, Galio aliwaambia Wayahudi, "Sikilizeni enyi Wayahudi! Kama kweli jambo hili lingekuwa juu ya uhalifu au uovu ningekuwa tayari kuwasikilizeni.
15但所争论的若是关于字句、名称和你们的律法,你们就应当自己处理。我不愿意审判这件事!”
15Lakini kama ni shauri la ubishi kuhusu maneno na majina ya Sheria yenu, amueni ninyi wenyewe. Mimi sitaki kuwa hakimu wa mambo haya!"
16于是就把他们从审判台前赶出去。
16Basi, akawafukuza kutoka mahakamani.
17众人揪住会堂主管苏提尼,在审判台前打他。这些事迦流一概不理。
17Nao wote wakamkamata Sosthene ambaye alikuwa kiongozi wa sunagogi, wakampiga palepale mbele ya mahakama. Lakini Galio hakujali kitendo hicho hata kidogo.
18结束第二次宣教旅程保罗住了许多日子,然后辞别弟兄们,坐船去叙利亚,同行的有百基拉和亚居拉。他因为许过愿,现在期满了,就在坚革里剃了头发。
18Paulo alikaa bado na wale ndugu huko Korintho kwa siku nyingi. Kisha aliwaaga, akapanda meli kwenda Siria pamoja na Priskila na Akula. Huko Kenkrea, alinyoa nywele zake kwa sababu ya nadhiri aliyokuwa ameweka.
19到了以弗所,保罗留他们在那里,自己却到会堂去,跟犹太人辩论。
19Walifika Efeso na hapo Paulo aliwaacha Priskila na Akula, akaenda katika sunagogi, akajadiliana na Wayahudi.
20众人请他多住些时候,他没有答应,
20Walimwomba akae nao muda mrefu zaidi, lakini hakupenda.
21却辞别他们说:“ 神若许可,我还要回到你们这里来。”于是从以弗所开船去了。
21Bali alipokuwa anaondoka, alisema, "Mungu akipenda nitakuja kwenu tena." Akaondoka Efeso kwa meli.
22保罗在该撒利亚登岸,上耶路撒冷问候教会,然后下安提阿去。
22Meli ilitia nanga Kaisarea, naye Paulo akaenda Yerusalemu kulisalimia lile kanisa, kisha akaenda Antiokia.
23第三次宣教旅程住了一些时候,他又动身,先后经过加拉太地区和弗吕家,坚固众门徒。
23Alikaa huko muda mfupi, halafu akaendelea na safari kwa kupitia sehemu za Galatia na Frugia akiwatia moyo wafuasi wote.
24亚波罗在以弗所传道有一个生在亚历山太的犹太人,名叫亚波罗,来到了以弗所。他很有口才,擅长讲解圣经。
24Myahudi mmoja aitwaye Apolo, mzaliwa wa Aleksandria, alifika Efeso. Alikuwa mtu mwenye ufasaha wa kuongea na mwenye ujuzi mkubwa wa Maandiko Matakatifu.
25这人在主的道上受过训练,心灵火热,很准确地讲论,并且教导人关于耶稣的事,但他只晓得约翰的洗礼。
25Alikuwa amefundishwa juu ya hiyo njia ya Bwana, na akiwa motomoto, aliongea juu ya habari za Yesu. Akafundisha kwa usahihi ingawa alikuwa amepata ubatizo wa Yohane tu.
26这人在会堂里放胆讲论起来;百基拉和亚居拉听了,就把他接来,把 神的道更准确地向他讲解。
26Priskila na Akula walipomsikia akiongea kwa uhodari ndani ya sunagogi, walimchukua kwao wakamfundisha hiyo Njia ya Mungu kwa usahihi zaidi.
27亚波罗有意要到亚该亚去,弟兄们就鼓励他,又写信请门徒接待他。他到了那里,对那些蒙恩信主的人帮助很多,
27Apolo alipoamua kwenda Akaya, wale ndugu walimtia moyo kwa kuwaandikia wafuasi kule Akaya wampokee. Alipofika huko, aliweza kwa msaada wa neema ya Mungu, kuwasaidia sana wale ndugu waliopata kuwa waumini;
28因为他当众有力地驳倒犹太人,引用圣经证明耶稣是基督。
28kwa maana aliendelea kwa uhodari kuwashinda Wayahudi hadharani akithibitisha kwa Maandiko Matakatifu kuwa Yesu ni Kristo.