聖經新譯本 (Simplified)

Swahili: New Testament

Acts

5

1亚拿尼亚和撒非拉的鉴戒
1Mtu mmoja aitwaye Anania na mkewe Safira waliuza shamba lao vilevile.
2他私底下把钱留了一部分,妻子也知道这件事。他把其余的一部分带来,放在使徒的脚前。
2Lakini, mkewe akiwa anajua, Anania akajiwekea sehemu ya fedha alizopata na ile sehemu nyingine akawakabidhi mitume.
3彼得说:“亚拿尼亚,为什么撒但充满了你的心,使你欺骗圣灵,私底下把卖地的钱留了一部分呢?
3Basi, Petro akamwuliza, "Anania, mbona Shetani ameuingia moyo wako na kukufanya umdanganye Roho Mtakatifu kwa kujiwekea sehemu ya fedha ulizopata kutokana na lile shamba?
4田地还没有卖,不是你自己的吗?既然卖了,所得的钱不是由你作主吗?你为什么存心这样作呢?你这不是欺骗人,而是欺骗 神。”
4Kabla ya kuliuza lilikuwa mali yako, na baada ya kuliuza, bado hizo fedha zilikuwa zako uzitumie utakavyo. Kwa nini basi, uliamua moyoni mwako kufanya jambo la namna hii? Hukumdanganya mtu; umemdanganya Mungu!"
5亚拿尼亚一听见这话,就仆倒断了气。所有听见的人都十分害怕。
5Anania aliposikia hayo, akaanguka chini, akafa. Watu wote waliosikia habari ya tukio hilo waliogopa sana.
6有几个青年人来把他包好,抬出去埋了。
6Vijana wakafika wakaufunika mwili wake, wakamtoa nje, wakamzika.
7大约三小时之后,亚拿尼亚的妻子进来,还不知道发生了什么事。
7Baada ya muda wa saa tatu hivi, mke wake, bila kufahamu mambo yaliyotukia, akaingia mle ndani.
8彼得问她:“你告诉我,你们卖田地的钱,就是这么多吗?”她说:“是的,就是这么多。”
8Petro akamwambia, "Niambie! Je, kiasi hiki cha fedha ndicho mlichopata kwa kuuza lile shamba?" Yeye akamjibu, "Naam, ni kiasi hicho."
9彼得说:“你们为什么串同试探主的灵呢?你看,埋你丈夫的人的脚,已经到了门口,他们也要把你抬出去。”
9Naye Petro akamwambia, "Mbona mmekula njama kumjaribu Roho wa Bwana? Sikiliza! Wale watu waliokwenda kumzika mume wako, sasa wako mlangoni na watakuchukua wewe pia."
10她立刻就仆倒在彼得脚前,断了气。那些青年人进来,发现她死了,把她也抬出去,埋在她丈夫旁边。
10Mara Safira akaanguka mbele ya miguu ya Petro, akafa. Wale vijana walipoingia, walimkuta amekwisha kufa; hivyo wakamtoa nje, wakamzika karibu na mume wake.
11全体会众和所有听见这事的人,都很害怕。
11Kanisa lote pamoja na wote waliosikia habari ya tukio hilo, waliogopa sana.
12使徒行神迹奇事主借着使徒的手,在民间行了许多神迹奇事。他们都同心聚集在所罗门廊下,
12Mitume walifanya miujiza na maajabu mengi kati ya watu. Waumini walikuwa wakikutana pamoja katika ukumbi wa Solomoni.
13其余的人,没有一个敢接近他们,可是民众都很敬重他们。
13Mtu yeyote mwingine ambaye hakuwa mwamini hakuthubutu kujiunga nao. Hata hivyo, watu wengine wasiokuwa wa imani hiyo waliwasifu.
14信主的男男女女越来越多,
14Idadi ya watu waliomwamini Bwana, wanaume kwa wanawake, iliongezeka zaidi na zaidi.
15甚至有人把病人抬到街上,放在小床和褥子上,好让彼得经过时,他的身影可以落在一些人身上。
15Kwa sababu hiyo, watu walikuwa wakipeleka wagonjwa barabarani na kuwalaza juu ya vitanda na mikeka ili Petro akipita, walau kivuli chake kiwaguse baadhi yao.
16耶路撒冷周围城市的人,也带着病人和受污灵缠扰的,蜂拥而来,结果病人全都医好了。
16Watu wengi walifika kutoka katika miji ya kando kando ya Yerusalemu, wakiwaleta wagonjwa wao na wale waliokuwa na pepo wachafu, nao wote wakaponywa.
17使徒受迫害大祭司和他的同党撒都该人,满心忌恨,
17Kisha, Kuhani Mkuu na wenzake waliokuwa wa kikundi cha Masadukayo wa mahali hapo, wakawaonea mitume wivu.
18于是下手拿住使徒,把他们押在公共拘留所里。
18Basi, wakawatia nguvuni, wakawafunga ndani ya gereza kuu.
19夜间有一位天使,打开监门,把他们领出来,说:
19Lakini usiku malaika wa Bwana aliifungua milango ya gereza, akawatoa nje, akawaambia,
20“你们去,站在殿里,把一切有关这生命的话,都讲给众民听。”
20"Nendeni mkasimame Hekaluni na kuwaambia watu kila kitu kuhusu maisha haya mapya."
21使徒听完了,就在黎明的时候,进到殿里去施教。大祭司和他的同党来到了,就召齐了公议会,就是以色列人的众长老,派人到监牢去带使徒出来。
21Mitume walitii, wakaingia Hekaluni asubuhi na mapema, wakaanza kufundisha. Kuhani Mkuu na wenzake walipofika, waliita mkutano wa Baraza kuu, yaani halmashauri yote ya wazee wa Wayahudi halafu wakawatuma watu gerezani wawalete wale mitume.
22差役到了监里,找不到他们,回来报告说:
22Lakini hao watumishi walipofika huko hawakuwakuta mle gerezani. Hivyo walirudi, wakatoa taarifa mkutanoni,
23“我们发现监门紧闭,狱卒也守在门外;等到开了门,里面连一个人也找不到。”
23wakisema, "Tulikuta gereza limefungwa kila upande na walinzi wakilinda milango. Lakini tulipofungua hatukumkuta mtu yeyote ndani."
24圣殿的守卫和祭司长听了这些话,觉得很困惑,不知道这件事将来会怎样。
24Mkuu wa walinzi wa Hekalu na makuhani wakuu waliposikia habari hiyo wakawa na wasiwasi, wasijue yaliyowapata.
25忽然有人来报告说:“你们押在监里的那些人,正站在殿里教导众民呢!”
25Akafika mtu mmoja, akawaambia, "Wale watu mliowafunga gerezani, hivi sasa wamo Hekaluni, wanawafundisha watu."
26于是守卫和差役去带使徒来,不过没有用暴力,因为怕众民用石头打他们。
26Hapo mkuu wa walinzi wa Hekalu pamoja na watu wake walikwenda Hekaluni, akawaleta. Lakini hawakuwakamata kwa kutumia nguvu, maana waliogopa kwamba watu wangewapiga mawe.
27既然带来了,就叫他们站在公议会前。大祭司问他们:
27Basi, wakawapeleka, wakawasimamisha mbele ya Baraza. Kuhani Mkuu akawaambia,
28“我们严厉地吩咐过你们,不准再奉这名施教。看,你们却把你们的道理传遍了耶路撒冷,想要把流这人的血的责任推到我们身上。”
28"Tuliwakatazeni waziwazi kufundisha kwa jina la mtu huyu; sasa mmeyaeneza mafundisho yenu pote katika Yerusalemu na mnakusudia kutuwekea lawama ya kifo cha mtu huyo."
29彼得和众使徒回答:“服从 神过于服从人,是应当的。
29Hapo Petro, akiwa pamoja na wale mitume wengine, akajibu, "Lazima tumtii Mungu, na siyo binadamu.
30你们挂在木头上亲手杀害的耶稣,我们祖先的 神已经使他复活了。
30Mungu wa babu zetu alimfufua Yesu baada ya ninyi kumwua kwa kumtundika msalabani.
31 神把他高举在自己的右边,作元首作救主,把悔改的心赐给了以色列人,使他们罪得赦免。
31Huyu ndiye yule aliyekwezwa na Mungu mpaka upande wake wa kulia, akawa kiongozi na Mwokozi, ili awawezeshe watu wa Israeli watubu, wapate kusamehewa dhambi zao.
32我们为这些事作证, 神赐给顺从的人的圣灵也为这些事作证。”
32Sisi ni mashahidi wa tukio hilo, naye Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wale wanaomtii, anashuhudia pia tukio hilo."
33公议会的人听了,非常恼怒,就想要杀他们。
33Wajumbe wote wa lile Baraza waliposikia hayo, wakawaka hasira, hata wakaamua kuwaua.
34但有一个法利赛人,名叫迦玛列,是民众所尊敬的律法教师。他在公议会中站起来,吩咐人把使徒暂时带出去,
34Lakini Mfarisayo mmoja aitwaye Gamalieli ambaye alikuwa mwalimu wa Sheria na aliyeheshimika sana mbele ya watu wote, alisimama mbele ya lile Baraza, akataka wale mitume watolewe nje kwa muda mfupi.
35然后对大家说:“以色列人哪,你们应当小心处理这些人!
35Kisha akawaambia wale wajumbe wa Baraza, "Wananchi wa Israeli, tahadhari kabla ya kutekeleza hicho mnachotaka kuwatenda watu hawa!
36从前有个丢大,自命不凡,附从他的人约有四百。他一被杀,跟从他的人尽都星散,一败涂地。
36Zamani kidogo, kulitokea mtu mmoja jina lake Theuda, akajisema kuwa mtu wa maana na watu karibu mia nne wakajiunga naye. Lakini aliuawa, kisha wafuasi wake wote wakatawanyika na kikundi chake kikafa.
37这人之后,在户口登记的时候,又有一个加利利人犹大,拉拢人们来跟从他。后来他也丧命,跟从他的人也就烟消云散了。
37Tena, baadaye, wakati ule wa kuhesabiwa watu, alitokea Yuda wa Galilaya. Huyu naye, aliwavuta watu wakamfuata; lakini naye pia aliuawa, na wafuasi wake wakatawanyika.
38至于目前的事,我劝你们不要管这些人,由他们吧!因为这计划或这行动,如果是出于人意,终必失败;
38Na sasa pia mimi nawaambieni, msiwachukulie watu hawa hatua yoyote; waacheni! Kwa maana, ikiwa mpango huu au shughuli hii yao imeanzishwa na binadamu, itatoweka yenyewe.
39如果是出于 神,你们就不能破坏他们,恐怕你们是与 神作对了。”他们接受了他的劝告,
39Lakini kama imeanzishwa na Mungu, siyo tu kwamba hamtaweza kuwashinda, bali mtajikuta mnapigana na Mungu." Basi, wakakubaliana naye.
40就传使徒进来,鞭打一顿,禁止他们奉耶稣的名传讲,就把他们释放了。
40Hivyo wakawaita wale mitume, wakaamuru wachapwe viboko na kuwaonya wasifundishe tena kwa jina la Yesu; kisha wakawaacha waende zao.
41使徒欢欢喜喜从公议会里出来,因为他们算是配得为主的名受辱。
41Basi, mitume wakatoka nje ya ule mkutano wa halmashauri wakiwa wamejaa furaha, kwani walistahili kuaibishwa kwa ajili ya jina la Yesu.
42他们天天在殿里并在各人的家中,不断地施教,传讲耶稣是基督。
42Wakaendelea kila siku kufundisha na kuhubiri Habari Njema ya Kristo, Hekaluni na nyumbani mwa watu.