1父母与儿女
1Enyi watoto, watiini wazazi wenu Kikristo maana hili ni jambo jema.
2“要孝敬父母,使你得福,在世长寿。”这是第一条带着应许的诫命。
2"Waheshimu Baba na mama yako," hii ndiyo amri ya kwanza ambayo imeongezewa ahadi, yaani,
3
3"Upate fanaka na miaka mingi duniani."
4你们作父亲的,不要激怒儿女,却要照着主的教训和劝戒,养育他们。
4Nanyi akina baba, msiwachukize watoto wenu ila waleeni katika nidhamu na mafundisho ya Kikristo.
5主人和仆人你们作仆人的,要存着敬畏、战兢和真诚的心,听从世上的主人,好像听从基督一样。
5Enyi watumwa, watiini mabwana zenu hapa duniani kwa hofu na tetemeko; fanyeni hivyo kwa unyofu wa moyo kana kwamba mnamtumikia Kristo.
6作事不要只作给人看,像那些讨人欢心的一样,却要像基督的仆人,从心里遵行 神的旨意,
6Fanyeni hivyo si tu wakati wanapowatazama ili mjipendekeze kwao, bali tumikieni kwa moyo kama atakavyo Mungu kwa sababu ninyi ni watumishi wa Kristo.
7甘心服务,像是服事主,不是服事人。
7Muwe radhi kutumikia kwa ajili ya Bwana na si kwa ajili ya watu.
8你们知道,无论是奴仆或自由的人,如果作了什么善事,都必从主那里得到赏赐。
8Kumbukeni kwamba kila mtu mwenye kutenda mema, awe mtumwa au mtu huru, atapokea tuzo lake kutoka kwa Bwana.
9你们作主人的,也要照样对待仆人,不要威吓他们;你们知道,他们和你们在天上同有一位主,他并不偏待人。
9Nanyi mnaotumikiwa, watendeeni vivyo hivyo watumwa wenu, na acheni kutumia vitisho. Kumbukeni kwamba ninyi pia kama vile wao, mnaye Bwana yuleyule mbinguni, kwake cheo cha mtu si kitu.
10穿戴 神所赐的军装最后,你们要靠主的大能大力,在他里面刚强。
10Hatimaye, nawatakeni muwe imara katika kuungana na Bwana na kwa msaada wa nguvu yake kuu.
11要穿戴 神所赐的全副军装,使你们能抵挡魔鬼的诡计。
11Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za Ibilisi.
12因为我们的争战,对抗的不是有血有肉的人,而是执政的、掌权的、管辖这黑暗世界的和天上的邪灵。
12Maana vita vyenu si vita kati yetu na binadamu, bali ni vita dhidi ya jeshi ovu la ulimwengu wa roho; tunapigana na watawala, wakuu na wenye nguvu wanaomiliki ulimwengu huu wa giza.
13所以要穿起 神所赐的全副军装,使你们在这邪恶的时代里可以抵挡得住,并且在作完了一切之后,还能站立得稳。
13Kwa sababu hiyo, vaeni silaha za Mungu ili siku ile itakapofika muweze kuyapinga mashambulio ya adui; na mkisha pigana mpaka mwisho, muwe bado thabiti.
14因此,你们要站稳,用真理当带子束腰,披上公义的胸甲,
14Basi, simameni imara! Ukweli uwe kama ukanda kiunoni mwenu, uadilifu uwe kama vazi la kujikinga kifuani,
15把和平的福音预备好了,当作鞋子,穿在脚上,
15na hamu ya kutangaza Habari Njema ya amani iwe kama viatu miguuni mwenu.
16拿起信心的盾牌,用来扑灭那恶者所有的火箭;
16Zaidi ya hayo yote, imani iwe daima kama ngao mikononi mwenu, iwawezeshe kuizima mishale ya moto ya yule Mwovu.
17并且要戴上救恩的头盔,拿起圣灵的宝剑,就是 神的道,
17Upokeeni wokovu kama kofia yenu ya chuma, na neno la Mungu kama upanga mnaopewa na Roho Mtakatifu.
18借着各样的祷告和祈求,随时在圣灵里祈祷,并且要在这事上恒久警醒,为众圣徒祈求。
18Salini daima, mkiomba msaada wa Mungu. Salini kila wakati kwa nguvu ya Roho. Kesheni bila kuchoka mkisali kwa ajili ya watu wote wa Mungu.
19也要为我祈求,使我传讲的时候,得着当说的话,可以坦然无惧地讲明福音的奥秘,
19Niombeeni nami pia ili niongeapo Mungu anijalie cha kusema, niweze kuwajulisha watu fumbo la Habari Njema kwa uthabiti.
20(我为这奥秘作了被捆锁的使者),也使我按着应当说的,放胆宣讲这福音的奥秘。
20Mimi ni balozi kwa ajili ya Habari Njema hiyo ingawa sasa niko kifungoni. Ombeni, basi, ili niweze kuwa hodari katika kuitangaza kama inipasavyo.
21祝福亲爱的推基古弟兄是主里忠心的仆人,他会把我的一切都告诉你们,使你们可以知道我的景况。
21Tukiko, ndugu yetu mpenzi na mtumishi mwaminifu wa Bwana, atawapeni habari zangu zote mpate kujua ninachofanya.
22为了这缘故,我就差他到你们那里去,好让你们明白我们的近况,并且叫他安慰你们的心。
22Namtuma kwenu awapeni habari zetu mpate kuwa na moyo.
23愿平安、慈爱、信心,从父 神和主耶稣基督临到众弟兄。
23Ninawatakieni ninyi ndugu amani, upendo na imani kutoka kwa Mungu Baba na kutoka kwa Bwana Yesu Kristo.
24愿一切以不朽的爱爱我们主耶稣基督的人,都蒙恩惠。
24Nawatakia neema ya Mungu wote wanaompenda Bwana wetu Yesu Kristo kwa mapendo yasiyo na mwisho.