1耶稣比摩西更尊贵
1Ndugu zangu watu wa Mungu ambao mmeitwa na Mungu, fikirini juu ya Yesu ambaye Mungu alimtuma awe Kuhani Mkuu wa imani tunayoiungama.
2他忠于那位委派他的,好像摩西在 神的全家尽忠一样。
2Yeye alikuwa mwaminifu kwa Mungu aliyemteua kufanya kazi yake kama vile Mose alivyokuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu.
3他比摩西配得更大的荣耀,好像建造房屋的人比房屋配得更大的尊贵一样。
3Mjenzi wa nyumba hupata heshima zaidi kuliko hiyo nyumba yenyewe. Hali kadhalika naye Yesu anastahili heshima kubwa zaidi kuliko Mose.
4因为每一间房屋都是人建造的,只有万物是 神建造的。
4Kila nyumba hujengwa na mjenzi fulani--na Mungu ndiye mjenzi wa vitu vyote.
5摩西不过是个仆人,在 神的全家尽忠,为以后要传讲的事作证;
5Mose alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Bwana kama mtumishi, na alinena juu ya mambo ambayo Mungu atayasema hapo baadaye.
6但是基督却是儿子,管理自己的家。如果我们把坦然无惧的心和可夸的盼望持守到底,我们就是他的家了。
6Lakini Kristo ni mwaminifu kama Mwana mwenye mamlaka juu ya nyumba ya Mungu. Sisi ni nyumba yake kama tukizingatia uhodari wetu na uthabiti wetu katika kile tunachotumainia.
7以色列人因不信得不到安息所以,就像圣灵所说的:“如果你们今天听从他的声音,
7Kwa hiyo, basi, kama asemavyo Roho Mtakatifu: "Kama mkisikia sauti ya Mungu leo,
8就不要硬着心,好像在旷野惹他发怒、试探他的日子一样;
8msiifanye mioyo yenu kuwa migumu kama wazee wenu walivyokuwa wakati walipomwasi Mungu; kama walivyokuwa siku ile kule jangwani,
9在那里,你们的祖先以试验来试探我,观看我的作为有四十年之久。
9Huko wazee wenu walinijaribu na kunichunguza, asema Bwana, ingawa walikuwa wameyaona matendo yangu kwa miaka arobaini.
10所以,我向那个世代的人发怒,说:‘他们心里常常迷误,不认识我的道路。’
10Kwa sababu hiyo niliwakasirikia watu hao nikasema, Fikira za watu hawa zimepotoka, hawajapata kamwe kuzijua njia zangu.
11我就在烈怒中起誓,说:‘他们绝不可进入我的安息。’”
11Basi, nilikasirika, nikaapa: Hawataingia huko ambako ningewapa pumziko."
12弟兄们,你们要小心,免得你们中间有人存着邪恶、不信的心,以致离弃了永活的 神;
12Basi ndugu, jihadharini asije akawako yeyote miongoni mwenu aliye na moyo mbaya hivyo na asiyeamini hata kujitenga na Mungu aliye hai.
13趁着还有叫作“今天”的时候,总要天天互相劝勉,免得你们中间有人受了罪恶的诱惑,心里就刚硬了。
13Maadamu hiyo "Leo" inayosemwa katika Maandiko bado inatuhusu sisi, mnapaswa kusaidiana daima, ili mtu yeyote miongoni mwenu asidanganywe na dhambi na kuwa mkaidi.
14如果我们把起初的信念坚持到底,就是有分于基督的人了。
14Maana sisi tunashirikiana na Kristo ikiwa tutazingatia kwa uthabiti tumaini tulilokuwa nalo mwanzoni.
15经上说:“如果你们今天听从他的声音,就不要硬着心,像惹他发怒的时候一样。”
15Maandiko yasema hivi: "Kama mkisikia sauti ya Mungu leo, msiifanye mioyo yenu kuwa migumu kama wazee wenu walivyokuwa wakati walipomwasi Mungu."
16那时,听了他的话而惹他发怒的是谁呢?不就是摩西从埃及领出来的那些人吗?
16Ni akina nani basi, waliosikia sauti ya Mungu wakamwasi? Ni wale wote walioongozwa na Mose kutoka Misri.
17四十年之久, 神向谁发怒呢?不就是向那些犯了罪陈尸旷野的人吗?
17Mungu aliwakasirikia akina nani kwa miaka arobaini? Aliwakasirikia wale waliotenda dhambi, maiti zao zikatapakaa kule jangwani.
18他又向谁起誓说,他们绝对不可以进入他的安息呢?不就是向那些不顺从的人吗?
18Mungu alipoapa: "Hawataingia huko ambako ningewapa pumziko," alikuwa anawasema akina nani? Alikuwa anasema juu ya hao walioasi.
19这样看来,他们不能进入安息,是因为不信的缘故。
19Basi, twaona kwamba hawakuingia huko kwa sababu hawakuamini.