1迦拿的婚筵
1Siku ya tatu kulikuwa na arusi mjini Kana, mkoani Galilaya. Mama yake Yesu alikuwapo,
2耶稣和门徒也被邀请参加婚筵。
2naye Yesu alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake.
3酒用尽了,耶稣的母亲对他说:“他们没有酒了。”
3Divai ilipokwisha, mama yake akamwambia, "Hawana divai!"
4耶稣说:“母亲(“母亲”原文作“妇人”),我跟你有什么关系呢?我的时候还没有到。”
4Yesu akamjibu, "Mama, usiniambie la kufanya. Saa yangu bado."
5他母亲告诉仆人说:“他吩咐你们什么,就作什么。”
5Hapo mama yake akawaambia watumishi, "Lolote atakalowaambieni, fanyeni."
6在那里有六口石缸,每口可盛两三桶水,是为犹太人行洁净礼用的。
6Hapo palikuwa na mitungi sita ya mawe, ambayo kila mmoja uliweza kuchukua kiasi cha madebe mawili au matatu. Ilikuwa imewekwa hapo kufuatana na desturi ya Kiyahudi ya kutawadha.
7耶稣吩咐仆人:“把缸都倒满水!”他们就倒满了,直到缸口。
7Yesu akawaambia, "Ijazeni mitungi hiyo maji." Nao wakaijaza mpaka juu.
8耶稣又吩咐他们:“现在舀出来,送给筵席的总管!”他们就送去了。
8Kisha akawaambia, "Sasa choteni mkampelekee mkuu wa karamu."
9总管尝了那水变的酒,不知道是从哪里来的,只有舀水的仆人知道。总管就叫新郎来,
9Mkuu wa karamu alipoonja hayo maji, kumbe yalikuwa yamegeuka kuwa divai. Yeye hakujua ilikotoka, (lakini wale watumishi waliochota maji walijua). Mkuu wa karamu akamwita bwana arusi,
10对他说:“人人都是先摆上好酒,等到亲友喝够了,才摆上次等的,你倒把好酒留到现在。”
10akamwambia, "Kila mtu huandaa divai nzuri kwanza hata wakisha tosheka huandaa ile hafifu. Lakini wewe umeiweka divai nzuri mpaka sasa!"
11这是耶稣所行的第一件神迹,是在加利利的迦拿行的。他显出了自己的荣耀,他的门徒就信了他。
11Yesu alifanya ishara hii ya kwanza huko Kana, Galilaya, akaonyesha utukufu wake; nao wanafunzi wake wakamwamini.
12这事以后,耶稣和母亲、弟弟、门徒,都下到迦百农去,在那里住了没有几天。
12Baada ya hayo, Yesu alishuka pamoja na mama yake, ndugu zake na wanafunzi wake, wakaenda Kafarnaumu ambako walikaa kwa siku chache.
13洁净圣殿(太21:12-13;可11:15-17;路19:45-46)犹太人的逾越节近了,耶稣就上耶路撒冷去。
13Sikukuu ya Wayahudi ya Pasaka ilikuwa imekaribia; hivyo Yesu akaenda Yerusalemu.
14他在圣殿的外院里看见有卖牛羊鸽子的,和坐在那里兑换银钱的,
14Hekaluni aliwakuta watu wakiuza ng'ombe, kondoo na njiwa, na wavunja fedha walikuwa wamekaa kwenye meza zao.
15就用绳索做了一条鞭子,把众人连牛带羊都从外院赶出去,倒掉兑换银钱的人的钱,推翻他们的桌子;
15Akatengeneza mjeledi wa kamba, akawafukuza wote nje ya Hekalu pamoja na kondoo na ng'ombe wao, akazimwaga sarafu za wenye kuvunja fedha na kupindua meza zao.
16又对卖鸽子的说:“把这些东西搬出去,不要把我父的殿当作巿场。”
16Akawaambia wale waliokuwa wanauza njiwa, "Ondoeni vitu hivi hapa. Msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa soko!"
17他的门徒就想起经上记着:“我为你的殿心中迫切,如同火烧。”
17Wanafunzi wake wakakumbuka kwamba Maandiko yasema: "Upendo wangu kwa nyumba yako waniua."
18犹太人就问他:“你可以显什么神迹给我们看,证明你有权作这些事呢?”
18Baadhi ya Wayahudi wakamwuliza Yesu, "Utafanya muujiza gani kuonyesha kwamba unayo haki kufanya mambo haya?"
19耶稣回答:“你们拆毁这殿,我三天之内要把它建造起来。”
19Yesu akawaambia, "Vunjeni Hekalu hili, nami nitalijenga kwa siku tatu."
20犹太人说:“这殿建了四十六年,你三天之内就能把它建造起来吗?”
20Hapo Wayahudi wakasema, "Hekalu hili lilijengwa kwa muda wa miaka arobaini na sita. Je, wewe utalijenga kwa siku tatu?"
21但耶稣所说的殿,就是他的身体。
21Lakini Yesu alikuwa anaongea juu ya Hekalu ambalo ni mwili wake.
22所以当耶稣从死人中复活以后,门徒想起了他说过这话,就信了圣经和耶稣所说的话。
22Basi, alipofufuliwa kutoka wafu, wanafunzi wake walikumbuka kwamba alikuwa amesema hayo, wakaamini Maandiko Matakatifu na yale maneno aliyokuwa akisema Yesu.
23耶稣知道人的内心耶稣在耶路撒冷过逾越节的时候,许多人看见他所行的神迹,就信了他的名。
23Yesu alipokuwa Yerusalemu kwa sikukuu ya Pasaka, watu wengi walimwamini walipoona ishara alizozifanya.
24耶稣却不信任他们,因为他知道所有的人,
24Lakini Yesu hakuwa na imani nao kwa sababu aliwajua wote.
25也不需要谁指证人是怎样的,因为他知道人心里存的是什么。
25Hakuhitaji kuambiwa chochote juu ya watu, maana aliyajua barabara mambo yote yaliyomo mioyoni mwao.