聖經新譯本 (Simplified)

Swahili: New Testament

Mark

13

1预言圣殿被毁(太24:1-2;路21:5-6)
1Yesu alipokuwa anatoka Hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake alimwambia, "Mwalimu, tazama jinsi mawe haya na majengo haya yalivyo ya ajabu!"
2耶稣对他说:“你看见这些伟大的建筑吗?将来必没有一块石头留在另一块石头上面,每一块都要拆下来。”
2Yesu akamwambia, "Je, unayaona majengo haya makubwa? Hakuna hata jiwe moja litakalosalia juu ya lingine; kila kitu kitabomolewa."
3这世代终结的预兆(太24:3-14;路21:7-19)耶稣在橄榄山上,面对圣殿坐着,彼得、雅各、约翰和安得烈私下问他:
3Yesu alipokuwa ameketi juu ya mlima wa Mizeituni akielekea Hekalu, Petro, Yakobo, Yohane na Andrea wakamwuliza kwa faragha,
4“请告诉我们,什么时候会有这些事呢?这一切事将要成就的时候有什么预兆呢?”
4"Twambie mambo haya yatatukia lini? Ni ishara gani itakayoonyesha kwamba mambo haya karibu yatimizwe?"
5耶稣就告诉他们说:“你们要小心,不要被人迷惑。
5Yesu akaanza kuwaambia, "Jihadharini msije mkadanganywa na mtu.
6有许多人要来,假冒我的名说‘我就是基督’,并且要迷惑许多的人。
6Maana wengi watakuja wakilitumia jina langu, wakisema, Mimi ndiye! nao watawapotosha watu wengi.
7你们听见战争和战争的风声,也不要惊慌,这是免不了的,不过,结局还没有到。
7Mtakaposikia juu ya vita na fununu za vita, msifadhaike. Mambo hayo lazima yatokee, lakini mwisho wenyewe ungali bado.
8一个民族要起来攻打另一个民族,一个国家要起来攻打另一个国家,到处要有地震,有饥荒,这些不过是痛苦的开始。
8Taifa moja litapigana na taifa lingine; utawala mmoja utapigana na utawala mwingine; kila mahali kutakuwa na mitetemeko ya ardhi na njaa. Mambo haya ni kama tu maumivu ya kwanza ya kujifungua mtoto.
9但你们要小心!因为人要把你们交给公议会,你们要在会堂里被鞭打,又要为我的缘故站在总督和君王面前,向他们作见证。
9"Lakini ninyi jihadharini. Maana watu watawapelekeni mahakamani, na kuwapigeni katika masunagogi. Mtapelekwa mbele ya watawala na wafalme kwa sababu yangu ili mpate kunishuhudia kwao.
10然而福音必须先传给万民。
10Lakini lazima kwanza Habari Njema ihubiriwe kwa mataifa yote.
11人把你们捉去送官的时候,用不着预先思虑要说什么,到那时候赐给你们什么话,你们就说什么,因为说话的不是你们,而是圣灵。
11Nao watakapowatieni nguvuni na kuwapeleka mahakamani, msiwe na wasiwasi juu ya yale mtakayosema; saa ile itakapofika, semeni chochote mtakachopewa, maana si ninyi mtakaosema, bali Roho Mtakatifu.
12弟兄要出卖弟兄,父亲要出卖儿子,甚至把他们置于死地;儿女要悖逆父母,害死他们。
12Ndugu atamsaliti ndugu yake auawe; baba atamsaliti mwanae; watoto watawashambulia wazazi wao na kuwaua.
13你们为我的名,要被众人恨恶,然而坚忍到底的必然得救。
13Watu wote watawachukieni ninyi kwa sababu ya jina langu. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokolewa.
14大灾难的日子(太24:15-28;路21:20-24)“当你们看见‘那造成荒凉的可憎者’,站在不该站的地方(读者必须领悟),那时,住在犹太的应当逃到山上;
14"Mtakapoona Chukizo Haribifu limesimama mahali ambapo si pake, (msomaji na atambue maana yake!) Hapo watu walioko Yudea wakimbilie milimani.
15在房顶的不要下来,也不要进到屋子里拿什么东西;
15Mtu aliye juu ya paa la nyumba asishuke kuingia nyumbani mwake kuchukua kitu.
16在田里的也不要回去取衣服。
16Aliye shambani asirudi nyuma kuchukua vazi lake.
17当那些日子,怀孕的和乳养孩子的有祸了!
17Ole wao waja wazito na wanaonyonyesha siku hizo!
18你们应当祈求,不要让这些事在冬天发生。
18Ombeni ili mambo hayo yasitukie nyakati za baridi.
19因为那些日子必有灾难,这是从 神创世的开始到现在未曾有过的,以后也必不会再有。
19Maana wakati huo kutakuwa na dhiki ambayo haijatokea tangu Mungu alipoumba ulimwengu mpaka leo, wala haitatokea tena.
20如果不是主减少那些日子,没有一个人可以存活;但是为了自己的选民,他必使那些日子减少。
20Kama Bwana asingepunguza siku hizo, hakuna binadamu ambaye angeokolewa. Lakini kwa ajili ya wateule wake, Bwana amezipunguza siku hizo.
21那时,如果有人对你们说:‘看哪,基督在这里!看哪,他在那里!’你们不要信。
21"Basi mtu akiwaambieni, Tazama, Kristo yupo hapa! au Yupo pale! msimsadiki.
22因为必有假基督和假先知出现,行神迹和奇事,如果可以的话,连选民也要迷惑了。
22Maana watatokea kina Kristo wa uongo na manabii wa uongo, watafanya ishara na maajabu, ili kuwapotosha wateule wa Mungu, kama ikiwezekana.
23所以你们应当小心!我已经事先把一切都告诉你们了。
23Lakini ninyi jihadharini. Mimi nimewaambieni mambo yote kabla hayajatokea.
24人子必驾云降临(太24:29-35;路21:25-33)“当那些日子,在那灾难以后,太阳就变黑了,月亮也不发光,
24"Basi, siku hizo baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza na mwezi hautaangaza.
25众星从天坠落,天上的万象震动。
25Nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za mbingu zitatikiswa.
26那时,他们要看见人子,满有能力和荣耀,驾着云降临;
26Hapo watamwona Mwana wa Mtu akija katika mawingu kwa nguvu nyingi na utukufu.
27他要差派天使,把他的选民从四方,从地极直到天边,都招聚来。
27Kisha atawatuma malaika wake; atawakusanya wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho wa dunia mpaka mwisho wa mbingu.
28“你们应该从无花果树学个功课:树枝发出嫩芽长出叶子的时候,你们就知道夏天近了。
28"Kwa mtini jifunzeni mfano huu: Mara tu matawi yake yanapoanza kuwa laini na kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia.
29同样,你们什么时候看见这些事发生,就知道他已经近在门口了。
29Hali kadhalika nanyi mtakapoona mambo hayo yakitendeka, jueni kwamba Mwana wa Mtu yuko karibu sana.
30我实在告诉你们,这一切都必会发生,然后这世代才会过去。
30Nawaambieni kweli, kizazi hiki hakitapita kabla ya mambo hayo yote kutukia.
31天地都要过去,但我的话决不会废去。
31Mbingu na dunia zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
32警醒准备(太24:36-51;路21:34-36)“至于那日子和时间,没有人知道,连天上的天使和子也不知道,只有父知道。
32"Lakini hakuna mtu ajuaye siku au saa hiyo itakuja lini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana; Baba peke yake ndiye ajuaye.
33你们要小心,要警醒,因为你们不知道那日期什么时候来到。
33Muwe waangalifu na kesheni, maana hamjui wakati huo utafika lini.
34这就像一个人出外远行,把责任(“责任”原文作“权柄”)一一地交给他的仆人,又吩咐看门的要警醒。
34Itakuwa kama mtu anayeondoka nyumbani kwenda safari akiwaachia watumishi wake madaraka, kila mmoja na kazi yake; akamwambia mlinzi wa mlango awe macho.
35所以你们要警醒,因为你们不知道家主什么时候来到,也许在黄昏,也许在半夜,也许在鸡叫时,也许在清晨。
35Kesheni, basi, kwa maana hamjui mwenye nyumba atarudi lini; huenda ikawa jioni, usiku wa manane, alfajiri au asubuhi.
36恐怕他忽然来到,发现你们正在睡觉。
36Kesheni ili akija ghafla asije akawakuta mmelala.
37我对你们所说的话,也是对众人说的,‘你们要警醒’。”
37Ninayowaambieni ninyi, nawaambia wote: Kesheni!"