1不可判断(路6:37-38、41-42)
1"Msiwahukumu wengine, msije nanyi mkahukumiwa na Mungu;
2你们怎样判断人,也必怎样被判断;你们用什么标准衡量人,也必照样被衡量。
2kwa maana jinsi mnavyowahukumu wengine, ndivyo nanyi mtakavyohukumiwa; na kipimo kilekile mnachotumia kwa wengine ndicho Mungu atakachotumia kwenu.
3为什么看见你弟兄眼中的木屑,却不理会自己眼中的梁木呢?
3Kwa nini wakiona kibanzi kilicho jichoni mwa ndugu yako, na papo hapo huioni boriti iliyoko jichoni mwako?
4你自己眼中有梁木,怎能对弟兄说:‘让我除掉你眼中的木屑’呢?
4Au, wawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi jichoni mwako, wakati wewe mwenyewe unayo boriti jichoni mwako?
5伪君子啊!先除掉你眼中的梁木,才可以看得清楚,去除掉弟兄眼中的木屑。
5Mnafiki wewe! Ondoa kwanza boriti iliyoko jichoni mwako na hapo ndipo utaona waziwazi kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilichoko jichoni mwa ndugu yako.
6不要把圣物给狗,也不要把你们的珍珠丢在猪前,免得它们用脚把珍珠践踏,又转过来猛噬你们。
6"Msiwape mbwa vitu vitakatifu wasije wakageuka na kuwararua ninyi; wala msiwatupie nguruwe lulu zenu wasije wakazikanyaga.
7祈求就必得着(路11:9-13,13:24)“你们祈求,就给你们;寻找,就寻见;叩门,就给你们开门。
7"Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata; bisheni, nanyi mtafunguliwa.
8因为凡祈求的就得着,寻找的就寻见,叩门的就给他开门。
8Maana, aombaye hupewa, atafutaye hupata, na abishaye hufunguliwa.
9你们中间哪一个人,儿子向他要饼,反给他石头;
9Je, kuna yeyote miongoni mwenu ambaye mtoto wake akimwomba mkate, atampa jiwe?
10要鱼,反给他蛇呢?
10Au je, akimwomba samaki, atampa nyoka?
11你们虽然邪恶,尚且知道把好东西给儿女,何况你们在天上的父,难道不更把好东西赐给求他的人吗?
11Kama basi ninyi, ingawa ni waovu, mwajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, hakika Baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi: atawapa mema wale wanaomwomba.
12你们愿意人怎样待你们,你们也要怎样待人,这是律法和先知的总纲。
12"Watendeeni wengine yale mnayotaka wao wawatendee ninyi. Hii ndiyo maana ya Sheria ya Mose na mafundisho ya manabii.
13“你们当进窄门,因为引到灭亡的门是宽的,路是大的,进去的人也多;
13"Ingieni kwa kupitia mlango mwembamba. Kwa maana njia inayoongoza kwenye maangamizi ni pana, na mlango wa kuingilia humo ni mpana; waendao njia hiyo ni wengi.
14但引到生命的门是窄的,路是小的,找着的人也少。
14Lakini njia inayoongoza kwenye uzima ni nyembamba, na mlango wa kuingilia humo ni mwembamba; ni watu wachache tu wanaoweza kuigundua njia hiyo.
15坏树不能结好果子(路6:43-44)“提防假先知!他们披着羊皮到你们当中,里面却是残暴的狼。
15"Jihadharini na manabii wa uongo. Wao huja kwenu wakionekana kama kondoo kwa nje, lakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali.
16凭着他们的果子就可以认出他们来:荆棘里怎能摘到葡萄?蒺藜里怎能摘到无花果呢?
16Mtawatambua kwa matendo yao. Je, watu huchuma zabibu katika miti ya miiba, au tini katika mbigili? La!
17照样,好树结好果子,坏树结坏果子;
17Basi, mti mwema huzaa matunda mema, na mti mbaya huzaa matunda mabaya.
18好树不能结坏果子,坏树也不能结好果子。
18Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mema.
19凡是不结好果子的树,就被砍下来,丢在火中。
19Kila mti usiozaa matunda mema utakatwa na kutupwa motoni.
20因此你们凭着他们的果子就可以认出他们来。
20Kwa hiyo, mtawatambua kwa matendo yao.
21“不是每一个对我说:‘主啊,主啊!’的人,都能进入天国,唯有遵行我天父旨意的人,才能进去。
21"Si kila aniambiaye, Bwana, Bwana, ataingia katika Ufalme wa mbinguni; ila ni yule tu anayetimiza mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
22到那日,必有许多人对我说:‘主啊,主啊!难道我们没有奉你的名讲道,奉你的名赶鬼,奉你的名行过许多神迹吗?’
22Wengi wataniambia Siku ile ya hukumu: Bwana, Bwana! kwa jina lako tulitangaza ujumbe wako, na kwa jina lako tuliwatoa pepo na kufanya miujiza mingi.
23但我必向他们声明:‘我从来不认识你们;你们这些作恶的人,离开我去吧!’
23Hapo nitawaambia: Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni mbele yangu, enyi watenda maovu.
24听道要行道(路6:47-49)“所以,凡听见我这些话又遵行的,就像聪明的人,把自己的房子盖在磐石上。
24"Kwa sababu hiyo, kila mtu anayeyasikia maneno yangu na kuyazingatia, anafanana na mtu mwenye busara, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba.
25雨淋、水冲、风吹,摇撼那房子,房子却不倒塌,因为建基在磐石上。
25Mvua ikanyesha, mito ikafurika, pepo kali zikavuma na kuipiga nyumba hiyo. Lakini haikuanguka kwa sababu ilikuwa imejengwa juu ya mwamba.
26凡听见我这些话却不遵行的,就像愚蠢的人,把自己的房子盖在沙土上。
26"Lakini yeyote anayesikia maneno yangu haya bila kuyazingatia, anafanana na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga.
27雨淋、水冲、风吹,摇撼那房子,房子就倒塌了,并且倒塌得很厉害。”
27Mvua ikanyesha, mito ikafurika, pepo kali zikavuma na kuipiga nyumba hiyo, nayo ikaanguka; tena kwa kishindo kikubwa."
28耶稣讲完了这些话,群众都惊奇他的教训。
28Yesu alipomaliza kusema maneno hayo, umati wa watu ukashangazwa na mafundisho yake.
29因为耶稣教导他们,像一个有权柄的人,不像他们的经学家。
29Hakuwa kama walimu wao wa Sheria, bali alifundisha kwa mamlaka.