1施舍不可张扬
1"Jihadharini msije mkafanya matendo yenu mema mbele ya watu kusudi mwonekane nao. La sivyo, Baba yenu aliye mbinguni hatawapeni tuzo.
2因此你施舍的时候,不可到处张扬,好像伪君子在会堂和街上所作的一样,以博取众人的称赞。我实在告诉你们,他们已经得了他们的赏赐。
2"Basi, unapomsaidia maskini, usijitangaze. Usifanye kama wanafiki wafanyavyo katika masunagogi na njiani ili watu wawasifu. Kweli nawaambieni, hao wamekwisha pata tuzo lao.
3你施舍的时候,不要让左手知道右手所作的,
3Lakini wewe unapomsaidia maskini, fanya hivyo kwamba hata rafiki yako asijue ufanyalo.
4好使你的施舍是在隐密中行的。你父在隐密中察看,必定报答你。
4Toa msaada wako kwa siri, na Baba yako aonaye yaliyofichika, atakutuza.
5如何祷告(路11:2-4)“你们祈祷的时候,不可像伪君子;他们喜欢在会堂和路口站着祈祷,好让人看见。我实在告诉你们,他们已经得了他们的赏赐。
5"Mnaposali, msifanye kama wanafiki. Wao hupenda kusimama na kusali katika masunagogi na katika pembe za njia ili watu wawaone. Kweli nawaambieni, hao wamekwisha pata tuzo lao.
6但你祈祷的时候,要进到密室里去,关上门,向在隐密中的父祈祷。你父在隐密中察看,必定报答你。
6Lakini wewe unaposali, ingia chumbani mwako, funga mlango, kisha umwombe Baba yako asiyeonekana. Naye Baba yako aonaye yaliyofichika, atakutuza.
7你们祈祷的时候,不可重复无意义的话,像教外人一样,他们以为话多了就蒙垂听。
7"Mnaposali, msipayuke maneno kama watu wasiomjua Mungu. Wao hudhani kwamba Mungu atawasikiliza ati kwa sababu ya maneno mengi.
8你们不可像他们,因为在你们祈求以先,你们的父已经知道你们的需要了。
8Msiwe kama wao. Baba yenu anajua mnayoyahitaji hata kabla ya kumwomba.
9所以你们要这样祈祷:‘我们在天上的父,愿你的名被尊为圣,
9Basi, hivi ndivyo mnavyopaswa kusali: Baba yetu uliye mbinguni: Jina lako litukuzwe.
10愿你的国降临,愿你的旨意成就在地上,如同在天上一样。
10Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
11我们每天所需的食物,求你今天赐给我们;
11Utupe leo chakula chetu tunachohitaji.
12赦免我们的罪,好像我们饶恕了得罪我们的人;
12Utusamehe makosa yetu, kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea.
13不要让我们陷入试探,救我们脱离那恶者。’(有些后期抄本在此有“因为国度、权柄、荣耀,全是你的,直到永远。阿们”一句)
13Usitutie katika majaribu, lakini utuokoe na yule Mwovu. is Baadhi ya makala za zamani zina; Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.
14如果你们饶恕别人的过犯,你们的天父也必饶恕你们。
14"Maana mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi pia.
15如果你们不饶恕别人,你们的父也必不饶恕你们的过犯。
15Lakini msipowasamehe watu makosa yao, naye Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
16禁食不让人知“你们禁食的时候,不可像伪君子那样愁眉苦脸,他们装成难看的样子,叫人看出他们在禁食。我实在告诉你们,他们已经得了他们的赏赐。
16"Mnapofunga, msiwe na huzuni kama wanafiki. Wao hukunja nyuso zao wapate kuonekana na watu kuwa wanafunga. Nawaambieni hakika, hao wamekwisha pata tuzo lao.
17可是你禁食的时候,要梳头洗脸,
17Wewe lakini unapofunga, paka kichwa chako mafuta, nawa uso wako,
18不要叫人看出你在禁食,只让在隐密中的父看见。你父在隐密中察看,必定报答你。
18ili mtu yeyote asijue kwamba unafunga, ila ujulikane tu kwa Baba yako asiyeonekana. Naye Baba yako aonaye yaliyofichika atakutuza.
19积财于天(路12:32-34)“不可为自己在地上积聚财宝,因为地上有虫蛀,有锈侵蚀,也有贼挖洞来偷。
19"Msijiwekee hazina hapa duniani ambako nondo na kutu huharibu, na wezi huingia na kuiba.
20要为自己积聚财宝在天上,那里没有虫蛀锈蚀,也没有贼挖洞来偷。
20Jiwekeeni hazina mbinguni ambako nondo na kutu hawawezi kuiharibu, wala wezi hawaingii wakaiba.
21你的财宝在哪里,你的心也在哪里。
21Maana pale ilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwa moyo wako.
22里面的光(路11:34-36)“眼睛就是身体的灯。如果你的眼睛健全,全身就都明亮;
22"Jicho ni taa ya mwili. Kama jicho lako ni zima, mwili wako wote utakuwa katika mwanga.
23如果你的眼睛有毛病,全身就都黑暗。如果你里面的光变成黑暗,这是多么的黑暗!
23Lakini ikiwa jicho lako ni bovu, mwili wako wote utakuwa katika giza. Basi, ikiwa mwanga ulioko ndani yako ni giza, basi, hilo ni giza la kutisha mno.
24不要为明天忧虑(路12:22-31)“一个人不能服事两个主人;他若不是恨这个爱那个,就是忠于这个轻视那个。你们不能服事 神,又服事金钱。
24"Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili. Maana atamchukia mmoja na kumpenda huyo wa pili; au ataambatana na mmoja na kumdharau huyo mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali pamoja.
25所以我告诉你们,不要为生命忧虑吃什么喝什么,也不要为身体忧虑穿什么。难道生命不比食物重要吗?身体不比衣服重要吗?
25"Ndiyo maana nawaambieni, msiwe na wasiwasi juu ya chakula na kinywaji mnavyohitaji ili kuishi, wala juu ya mavazi mnayohitaji kwa ajili ya miili yenu. Je, maisha ni chakula tu au zaidi? Na mwili, je, si zaidi ya mavazi?
26你们看天空的飞鸟:它们不撒种,不收割,也不收进仓里,你们的天父尚且养活它们;难道你们不比它们更宝贵吗?
26Waangalieni ndege wa mwituni: hawapandi, hawavuni, wala hawana ghala yoyoye. Hata hivyo, Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, ninyi si wa thamani kuliko hao?
27你们中间谁能用忧虑使自己的寿命延长一刻呢?
27Ni nani miongoni mwenu kwa kuwa na wasiwasi sana anaweza kuuongeza muda wa maisha yake?
28何必为衣服忧虑呢?试想田野的百合花怎样生长,它们不劳苦,也不纺织。
28"Na kuhusu mavazi, ya nini kuwa na wasiwasi? Tazameni maua ya porini jinsi yanavyostawi. Hayafanyi kazi wala hayasokoti.
29但我告诉你们,就是所罗门最威荣的时候所穿的,也比不上这花中的一朵。
29Lakini nawaambieni, hata Solomoni mwenyewe na fahari zake zote hakupata kuvikwa vizuri kama ua mojawapo.
30田野的草,今天还在,明天就投进炉里, 神尚且这样妆扮它们;小信的人哪,何况你们呢?
30Ikiwa basi Mungu hulivika hivyo jani la shambani ambalo leo liko na kesho latupwa motoni, je, hatafanya zaidi kwenu ninyi? Enyi watu wenye imani haba!
31所以不要忧虑,说:‘我们该吃什么?喝什么?穿什么?’
31"Basi, msiwe na wasiwasi: Tutakula nini, tutakunywa nini, tutavaa nini!
32这些都是教外人所寻求的,你们的天父原知道你们需要这一切。
32Maana hayo yote yanahangaikiwa na watu wasiomjua Mungu. Baba yenu wa mbinguni anajua kwamba mnahitaji vitu hivyo vyote.
33你们要先求他的国和他的义,这一切都必加给你们。
33Bali, zingatieni kwanza Ufalme wa Mungu na matakwa yake, na hayo mengine yote mtapewa kwa ziada.
34所以不要为明天忧虑,因为明天自有明天的忧虑,一天的难处一天当就够了。”
34Basi, msiwe na wasiwasi juu ya kesho; kesho inayo yake. Matatizo ya siku moja yanawatosheni kwa siku hiyo.