聖經新譯本 (Simplified)

Swahili: New Testament

Matthew

5

1论福(路6:20-23)
1Yesu alipoyaona makundi ya watu, alipanda mlimani, akaketi. Wanafunzi wake wakamwendea,
2他就开口教训他们:
2naye akaanza kuwafundisha:
3“心灵贫乏的人有福了,因为天国是他们的。
3"Heri walio maskini rohoni, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
4哀痛的人有福了,因为他们必得安慰。
4Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa.
5温柔的人有福了,因为他们必承受地土。
5Heri walio wapole, maana watairithi nchi.
6爱慕公义如饥如渴的人有福了,因为他们必得饱足。
6Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa.
7怜悯人的人有福了,因为他们必蒙怜悯。
7Heri walio na huruma, maana watahurumiwa.
8内心清洁的人有福了,因为他们必看见 神。
8Heri wenye moyo safi, maana watamwona Mungu.
9使人和平的人有福了,因为他们必称为 神的儿子。
9Heri wenye kuleta amani, maana wataitwa watoto wa Mungu.
10为义遭受迫害的人有福了,因为天国是他们的。
10Heri wanaoteswa kwa sababu ya kufanya atakavyo Mungu, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
11人若因我的缘故辱骂你们,迫害你们,并且捏造各样坏话毁谤你们,你们就有福了。
11"Heri yenu ninyi watu wakiwatukana, wakiwadhulumu na kuwasingizia kila aina ya uovu kwa ajili yangu.
12你们应该欢喜快乐,因为你们在天上的赏赐是大的;在你们以前的先知,他们也曾这样迫害。
12Furahini na kushangilia maana tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Hivyo ndivyo walivyowadhulumu manabii waliokuwako kabla yenu.
13门徒作盐作光(可9:50;路14:34-35)“你们是地上的盐;如果盐失了味,怎能使它再咸呢?结果毫无用处,唯有丢在外面任人践踏。
13"Ninyi ni chumvi ya dunia! Lakini chumvi ikipoteza ladha yake itakolezwa na nini? Haifai kitu tena, ila hutupwa nje na kukanyagwa na watu.
14你们是世上的光。建在山上的城是无法隐藏的;
14"Ninyi ni mwanga wa ulimwengu! Mji uliojengwa juu ya mlima hauwezi kufichika.
15人点了灯,不会放在量器底下,而是放在灯台上,就照亮一家人。
15Wala watu hawawashi taa na kuifunika kwa chungu, ila huiweka juu ya kinara ili iwaangazie wote waliomo nyumbani.
16照样,你们的光也应当照在人前,让他们看见你们的好行为,又颂赞你们在天上的父。
16Vivyo hivyo, ni lazima mwanga wenu uangaze mbele ya watu, ili wayaone matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni."
17论律法“你们不要以为我来是要废除律法和先知;我来不是要废除,而是要完成。
17"Msidhani ya kuwa nimekuja kutangua Sheria ya Mose na mafundisho ya manabii. Sikuja kutangua bali kukamilisha.
18我实在告诉你们,就算天地过去,律法的一点一画也不会废去,全部都要成就。
18Kweli nawaambieni, mpaka hapo mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata nukta moja au sehemu ndogo kabisa ya Sheria itakayoondolewa, mpaka yote yametimia.
19因此,无论谁废除诫命中最小的一条,又这样教导人,他在天国中必称为最小的;但若有人遵行这些诫命,并且教导人遵行,他在天国中必称为大。
19Basi, yeyote atakayevunja hata amri moja ndogo kuliko zote, na kuwafundisha wengine wafanye hivyo, huyo atakuwa mdogo kabisa katika Ufalme wa mbiguni. Lakini yule atakayezishika na kuwafundisha wengine, huyo atakuwa mkubwa katika Ufalme wa mbinguni.
20我告诉你们,你们的义若不胜过经学家和法利赛人的义,就必不能进天国。
20Ndiyo maana nawaambieni, wema wenu usipozidi ule wa Mafarisayo na walimu wa Sheria, hamtaingia kamwe katika Ufalme wa mbinguni.
21不可恨人(路12:58-59)“你们听过有这样吩咐古人的话:‘不可杀人,杀人的必被判罪。’
21"Mmekwisha sikia ya kuwa watu wa kale waliambiwa: Usiue! Atakayeua lazima ahukumiwe.
22可是我告诉你们,凡是向弟兄发怒的,必被判罪。人若说弟兄是‘拉加’,必被公议会审判;人若说弟兄是‘摩利’,必难逃地狱的火。
22Lakini mimi nawaambieni, yeyote anayemkasirikia ndugu yake, lazima ahukumiwe. Anayemdharau ndugu yake atapelekwa mahakamani. Anayemwita ndugu yake: Pumbavu atastahili kuingia katika moto wa Jehanamu.
23所以你在祭坛上献供物的时候,如果在那里想起你的弟兄对你不满,
23Basi, ukipeleka sadaka yako mbele ya madhabahu na hapo ukakumbuka kwamba ndugu yako ana ugomvi nawe,
24就当在坛前放下供物,先去与弟兄和好,然后才来献你的供物。
24iache sadaka yako mbele ya madhabahu, nenda kwanza ukapatane na ndugu yako, ndipo urudi ukatoe sadaka yako.
25趁着你和你的对头还在路上的时候,要赶快与他和解,免得他抓你去见法官,法官把你交给狱警,关在监里。
25"Patana na mshtaki wako upesi mkiwa bado njiani, kwenda mahakamani. La sivyo, mshtaki wako atakukabidhi kwa hakimu, naye hakimu atakukabidhi kwa askari, nawe utafungwa gerezani.
26我实在告诉你,除非你还清最后一分钱,否则决不能从那里出来。
26Kweli nakwambia, hutatoka humo mpaka umemaliza kulipa senti ya mwisho.
27不可动淫念“你们听过有这样的吩咐:‘不可奸淫。’
27"Mmesikia ya kuwa watu waliambiwa: Usizini!
28可是我告诉你们,凡是看见妇女就动淫念的,心里已经犯了奸淫。
28Lakini mimi nawaambieni, atakayemtazama mwanamke kwa kumtamani, amekwisha zini naye moyoni mwake.
29如果你的右眼使你犯罪,就把它挖出来丢掉;宁可失去身体的一部分,胜过全身被丢进地狱里。
29Basi, kama jicho lako la kulia linakukosesha, ling'oe ukalitupe mbali. Afadhali zaidi kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako, kuliko mwili wako wote kutupwa katika moto wa Jehanamu.
30如果你的右手使你犯罪,就把它砍下来丢掉;宁可失去身体的一部分,胜过全身进到地狱里去。
30Na kama mkono wako wa kulia unakukosesha, ukate ukautupe mbali. Afadhali zaidi kupoteza kiungo kimoja cha mwili, kuliko mwili wako wote uende katika moto wa Jehanamu.
31不可休妻(太19:9;可10:11-12;路16:18)“又有这样的吩咐:‘人若休妻,就应当给她休书。’
31"Ilikwisha semwa pia: Anayemwacha mke wake, yampasa ampe hati ya talaka.
32可是我告诉你们,凡休妻的,如果不是因她不贞,就是促使她犯奸淫;无论谁娶了被休的妇人,也就是犯奸淫了。
32Lakini mimi nawaambieni, anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, anamfanya azini; na mtu akimwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini.
33不可发誓“你们又听过有这样吩咐古人的话:‘不可背约,向主许的愿都要偿还。’
33"Tena mmesikia kuwa watu wa kale waliambiwa: Usivunje kiapo chako, bali ni lazima utimize kiapo chako kwa Bwana.
34可是我告诉你们,总不可发誓,不可指着天发誓,因为天是 神的宝座;
34Lakini mimi nawaambieni, msiape kamwe; wala kwa mbingu, maana ni kiti cha enzi cha Mungu;
35不可指着地发誓,因为地是 神的脚凳;不可指着耶路撒冷发誓,因为它是大君王的京城;
35wala kwa dunia, maana ni kiti chake cha kuwekea miguu; wala kwa Yerusalemu, maana ni mji wa Mfalme mkuu.
36也不可指着自己的头发誓,因为你不能使一根头发变白或变黑。
36Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kuufanya hata unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.
37你们的话,是就说‘是’,不是就说‘不是’;如果再多说,就是出于那恶者。
37Ukisema, Ndiyo, basi iwe Ndiyo; ukisema Siyo, basi iwe kweli Siyo. Chochote kinachozidi hayo hutoka kwa yule Mwovu.
38不可报复(路6:29-30)“你们听过有这样的吩咐:‘以眼还眼,以牙还牙。’
38"Mmesikia kwamba ilisemwa: Jicho kwa jicho, jino kwa jino.
39可是我告诉你们,不要与恶人对抗,有人打你的右脸,把另一边也转过来让他打;
39Lakini mimi nawaambieni, usimlipize kisasi mtu mbaya. Mtu akikupiga kofi shavu la kulia, mgeuzie pia shavu la pili.
40有人要告你,想拿你的衬衫,就连外套也让他拿去。
40Mtu akikupeleka mahakamani kutaka kukuchukulia shati lako, mwache achukue pia koti lako.
41有人要强迫你走一里路,就陪他走两里。
41Mtu akikulazimisha kubeba mzigo wake kilomita moja, ubebe kilomita mbili.
42有求你的,就给他;想借贷的,也不可拒绝。
42Akuombaye mpe, na mtu akitaka kukukopa kitu usimnyime.
43当爱仇敌(路6:27-28、32-36)“你们听过有这样的吩咐:‘当爱你的邻舍,恨你的仇敌。’
43"Mmesikia kwamba ilisemwa: Mpende jirani yako na kumchukia adui yako.
44可是我告诉你们,当爱你们的仇敌,为迫害你们的祈祷,
44Lakini mimi nawaambieni, wapendeni adui zenu na kuwaombea wale wanaowadhulumu ninyi
45好叫你们成为你们天父的儿子;因为他使太阳照恶人,也照好人;降雨给义人,也给不义的人。
45ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaangazia jua lake watu wabaya na wema, na kuwanyeshea mvua watu wanyofu na waovu.
46如果你们只爱那些爱你们的人,有什么赏赐呢?税吏不也是这样作吗?
46Je, mtapata tuzo gani kwa kuwapenda tu wale wanaowapenda ninyi? Hakuna! Kwa maana hata watoza ushuru hufanya hivyo!
47如果你们单问候你们的弟兄,有什么特别呢?教外人不也是这样作吗?
47Kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mmefanya kitu kisicho cha kawaida? Hata watu wasiomjua Mungu nao hufanya vivyo hivyo.
48所以你们要完全,正如你们的天父是完全的。”
48Basi, muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.