1捆绑撒但一千年
1Kisha nikamwona malaika mmoja anashuka kutoka mbinguni akiwa na ufunguo wa kuzimu na mnyororo mkubwa mkononi mwake.
2他捉住了那龙,那古蛇,就是魔鬼,撒但,把它捆绑了一千年。
2Akalikamata lile joka--nyoka wa kale, yaani Ibilisi au Shetani--akalifunga kwa muda wa miaka elfu moja.
3天使把它拋在无底坑里,关起来,封上印,使它不能再迷惑列国,等到那一千年完了。以后,必须暂时释放它。
3Malaika akalitupa Kuzimu, akaufunga mlango wa kuingilia huko na kuutia mhuri ili lisiweze tena kuyapotosha mataifa mpaka hapo miaka elfu moja itakapotimia. Lakini baada ya miaka hiyo ni lazima lifunguliwe tena, lakini kwa muda mfupi tu.
4我又看见一些宝座,有人坐在上面,他们得了审判的权柄。我也看见那些因为替耶稣作见证,并且因为 神的道而被斩首的人的灵魂。他们没有拜过兽或兽像,也没有在额上或手上受过兽的记号。他们都复活了,与基督一同作王一千年。
4Kisha nikaona viti vya enzi na watu walioketi juu yake; watu hao walipewa mamlaka ya hukumu. Niliona pia roho za wale waliokuwa wamenyongwa kwa sababu ya kumtangaza Yesu na kwa sababu ya neno la Mungu. Hawa hawakumwabudu yule mnyama na sanamu yake, wala hawakupigwa alama yake juu ya paji za nyuso zao, au juu ya mikono yao. Walipata tena uhai, wakatawala pamoja na Kristo kwa muda wa miaka elfu moja.
5其余的死人还没有复活,等到那一千年完了。这是头一次的复活。
5(Wale wengine waliokufa hawakupata uhai mpaka miaka elfu moja itimie.) Huu ndio ufufuo wa kwanza.
6在头一次复活有分的人是有福的、圣洁的,第二次的死没有能力辖制他们。他们还要作 神和基督的祭司,与他一同作王一千年。
6Wameneemeka sana, tena heri yao wote wanaoshiriki ufufuo huu wa kwanza. Kifo cha pili hakitakuwa na nguvu juu yao; watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, na watatawala pamoja naye kwa miaka elfu moja.
7撒但的失败那一千年完了,撒但就要从监牢里被释放出来。
7Wakati miaka elfu mia moja itakapotimia, Shetani atafunguliwa kutoka gerezani mwake.
8他要出来迷惑地上四方的列国,就是高革和玛高革,使他们聚集争战。他们的人数好像海边的沙那么多。
8Basi, atatoka nje, ataanza kuyapotosha mataifa yote yaliyotawanyika kila mahali duniani, yaani Gogu na Magogu. Shetani atawakusanya pamoja kwa ajili ya vita; nao watakuwa wengi kama mchanga wa pwani.
9他们上来遍满了全地,围住了圣徒的营和那蒙爱的城,就有火从天上降下来,毁灭了他们。
9Walitawanyika katika nchi yote, wakaizunguka kambi ya watu wa Mungu na mji wa Mungu aupendao. Lakini moto ulishuka kutoka mbinguni, ukawaangamiza.
10那迷惑他们的魔鬼,被拋在硫磺的火湖里,就是兽和假先知所在的地方。他们必昼夜受痛苦,直到永永远远。
10Ibilisi, aliyekuwa anawapotosha, akatupwa ndani ya ziwa linalowaka moto wa kiberiti, walimo yule mnyama na yule nabii wa uongo, nao watateswa mchana na usiku, milele na milele.
11白色大宝座的审判我又看见一个白色的大宝座,和坐在上面的那位。天地都从他面前逃避,再也看不见了。
11Kisha nikaona kiti cha enzi kikubwa cheupe, na yule aketiye juu yake. Dunia na mbingu vikatoweka mbele ya macho yake, na havikuonekana tena.
12我又看见死了的人,无论大小,都站在宝座前。案卷都展开了,还有另一卷,就是生命册,也展开了。死了的人都凭着这些案卷所记载的,照着他们所行的受审判。
12Kisha nikawaona watu wakubwa na wadogo, wamesimama mbele ya kiti cha enzi, na vitabu vikafunguliwa. Halafu kitabu kingine, yaani kitabu cha uzima, kikafunguliwa pia. Wafu wakahukumiwa kadiri ya matendo yao, kama ilivyoandikwa ndani ya vitabu hivyo.
13于是海把其中的死人交出来,死亡和阴间也把其中的死人交出来,他们都照着各人所行的受审判。
13Bahari ikawatoa nje wafu waliokuwa ndani yake; kifo na kuzimu vikawatoa nje wafu waliokuwa ndani yao. Kila mmoja akahukumiwa kufuatana na matendo yake.
14死亡和阴间也被拋在火湖里。这火湖就是第二次的死。
14Kisha kifo na kuzimu vikatupwa ndani ya ziwa la moto. Ziwa hili la moto ndicho kifo cha pili.
15凡是名字没有记在生命册上的,他就被拋在火湖里。
15Mtu yeyote ambaye jina lake halikupatikana limeandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika ziwa la moto.