聖經新譯本 (Simplified)

Swahili: New Testament

Revelation

5

1得胜的羊羔配展开书卷
1Kisha katika mkono wa kulia wa huyo aliyeketi juu ya kiti cha enzi, nikaona kitabu; nacho kilikuwa kimeandikwa ndani na nje na kufungwa na mihuri saba.
2我又看见一位大力的天使,大声宣告说:“谁配展开那书卷,拆开它的封印呢?”
2Tena nikamwona malaika mwenye nguvu akitangaza kwa sauti kubwa: "Nani anayestahili kuvunja hiyo mihuri na kukifungua kitabu hicho?"
3在天上、地上、地底下,没有一个能够展开书卷观看的。
3Lakini hakupatikana mtu yeyote mbinguni, wala duniani, wala chini Kuzimu, aliyeweza kukifungua hicho kitabu au kukitazama ndani.
4因为没有人配展开观看书卷,我就大哭。
4Basi, mimi nikalia sana kwa sababu hakupatikana mtu aliyestahili kukifungua, au kukitazama ndani.
5长老中有一位对我说:“不要哭!看哪,那从犹大支派出来的狮子,大卫的根,他已经得胜了,他能够展开那书卷,拆开它的七印。”
5Kisha mmoja wa wale wazee akaniambia, "Usilie! Tazama! Simba wa kabila la Yuda, mjukuu maarufu wa Daudi, ameshinda. Yeye anaweza kuivunja mihuri yake saba na kukifungua hicho kitabu."
6我又看见在宝座和四个活物中间,并且在众长老中间,有羊羔站着,像是被杀过的。他有七角七眼,就是 神的七灵,奉差遣到全地去的。
6Kisha nikaona pale katikati ya kiti cha enzi Mwana kondoo amesimama, akizungukwa kila upande na vile viumbe hai vinne, na wale wazee. Huyo Mwanakondoo alionekana kana kwamba amechinjwa. Alikuwa na pembe saba na macho saba ambayo ni roho saba za Mungu zilizokuwa zimepelekwa kila mahali duniani.
7羊羔走过去,从坐在宝座上那位的右手中取了书卷。
7Mwanakondoo akaenda, akakitwaa hicho kitabu kutoka mkono wa kulia wa yule aliyeketi juu ya kiti cha enzi.
8他拿了书卷之后,四个活物和二十四位长老就俯伏在羊羔面前,各拿着琴和盛满了香的金炉,这香就是众圣徒的祈祷。
8Mara tu alipokwisha twaa hicho kitabu, vile viumbe hai vinne pamoja na wale wazee ishirini na wanne walianguka kifudifudi mbele ya Mwanakondoo. Kila mmoja, alikuwa na kinubi na bakuli za dhahabu zilizojaa ubani, ambao ni sala za watu wa Mungu.
9他们唱着新歌,说:“你配取书卷,配拆开封印,因为你曾被杀,曾用你的血,从各支派、各方言、各民族、各邦国,把人买了来归给 神,
9Basi, wakaimba wimbo huu mpya: "Wewe unastahili kukitwaa hicho kitabu na kuivunja mihuri yake. Kwa sababu wewe umechinjwa, na kwa damu yako umemnunulia Mungu watu kutoka katika kila kabila, lugha, jamaa na taifa.
10使他们成为我们 神的国度和祭司,他们要在地上执掌王权。”
10Wewe umewafanya wawe ufalme wa makuhani wamtumikie Mungu wetu nao watatawala duniani."
11我又观看,听见了千千万万天使的声音,他们都在宝座、活物和长老的四周,
11Kisha nikatazama, nikasikia sauti ya malaika wengi sana, idadi isiyohesabika, maelfu na maelfu. Walikuwa wamekaa kuzunguka kiti cha enzi, vile viumbe hai vinne na wale wazee;
12大声说:“被杀的羊羔是配得权能、丰富、智慧、力量、尊贵、荣耀、颂赞的!”
12wakasema kwa sauti kuu: "Mwanakondoo aliyechinjwa anastahili kupokea uwezo, utajiri, hekima, nguvu, utukufu na sifa."
13我又听见在天上、地上、地底下和海里的一切被造之物,以及天地间的万有,都说:“愿颂赞、尊贵、荣耀、能力,都归给坐在宝座上的那一位和羊羔,直到永永远远!”
13Nikasikia viumbe vyote mbinguni, duniani, chini kuzimuni na baharini--viumbe vyote ulimwenguni--vikisema: "Kwake yeye aketiye katika kiti cha enzi, na kwa Mwanakondoo, iwe sifa na heshima na utukufu na enzi milele na milele."
14四个活物就说:“阿们!”众长老也俯伏敬拜。
14Na vile viumbe vinne hai vikasema, "Amina!" Na wale wazee wakaanguka kifudifudi, wakaabudu.