1天上的敬拜
1Baada ya hayo nilitazama nikaona mlango umefunguliwa mbinguni. Na ile sauti niliyoisikia pale awali ambayo ilikuwa kama sauti ya tarumbeta, ikasema, "Njoo hapa juu nami nitakuonyesha mambo yatakayotukia baadaye."
2立刻,我在灵里,就看见有一个宝座,设立在天上,有一位坐在宝座上。
2Mara nikachukuliwa na Roho. Kumbe, huko mbinguni kuna kiti cha enzi na juu yake ameketi mmoja.
3那位坐着的,看来好像碧玉和红宝石,又有彩虹围绕着宝座,看来好像绿宝石。
3Huyo aliyeketi juu yake alikuwa kama almasi na jiwe zuri jekundu. Upinde wa mvua ulikuwa unang'aa kama zumaridi na ulikizunguka kiti cha enzi pande zote.
4宝座的周围有二十四个座位,上面坐着二十四位长老,身穿白衣,头戴金冠。
4Kulikuwa na duara la viti ishirini na vinne kukizunguka kiti cha enzi, na juu ya viti hivyo wazee ishirini na wanne walikuwa wameketi wamevaa mavazi meupe na taji za dhahabu vichwani.
5有闪电、响声、雷轰从宝座中发出;又有七枝火炬在宝座前点着,这就是 神的七灵。
5Umeme, sauti na ngurumo, vilikuwa vinatoka kwenye hicho kiti cha enzi. Taa saba za moto zilikuwa zinawaka mbele ya hicho kiti cha enzi. Taa hizo ni roho saba za Mungu.
6宝座前有一个看来好像水晶的玻璃海。在宝座中间和宝座周围有四个活物,前后布满了眼睛。
6Mbele ya kiti cha enzi kulikuwa na kitu kama bahari ya kioo, angavu kama jiwe linga'aalo sana. Katika pande zote za hicho kiti cha enzi na kukizunguka, kilikuwa na viumbe hai vinne. Viumbe hivyo vilikuwa vimejaa macho mbele na nyuma.
7第一个活物像狮子,第二个活物像牛犊,第三个活物的脸面像人,第四个活物像飞鹰。
7Kiumbe cha kwanza kulikuwa kama simba, cha pili kama ng'ombe, cha tatu kilikuwa na sura kama mtu, na cha nne kilikuwa kama tai anayeruka.
8四个活物各有六个翅膀,里外布满了眼睛。他们昼夜不停地说:“圣哉!圣哉!圣哉!主、全能的 神,昔在、今在、以后永在的那一位。”
8Viumbe hivyo vinne vilikuwa na mabawa sita kila kimoja, na vilikuwa vimejaa macho, ndani na nje. Usiku na mchana, bila kupumzika huimba: "Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu ni Bwana, Mungu Mwenye Uwezo, aliyekuwako, aliyeko na anayekuja!"
9每逢四个活物把荣耀、尊贵、感谢献给那坐在宝座上,活到永永远远的那一位的时候,
9Kila mara viumbe vinne vilipoimba nyimbo za kumtukuza, kumheshimu na kumshukuru huyo aliyeketi juu ya kiti cha enzi, ambaye anaishi milele na milele,
10二十四位长老就俯伏在坐在宝座上那一位的面前,敬拜那活到永永远远的,又把他们的冠冕放在宝座前,说:
10wale wazee ishirini na wanne hujiangusha mbele ya huyo aliyeketi juu ya kiti cha enzi na kumwabudu huyo ambaye anaishi milele na milele; na huziweka taji zao mbele ya kiti cha enzi wakisema:
11“主、我们的 神,你是配得荣耀、尊贵、权能的,因为你创造了万有,万有都是因着你的旨意而存在,而被造的。”
11"Wewe ni Bwana na Mungu wetu, unastahili utukufu na heshima na nguvu; maana wewe uliumba vitu vyote, na kwa matakwa yako kila kitu kimepewa uhai na uzima."