1印了十四万四千个以色列人
1Baada ya hayo nikawaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za dunia wakishika pepo nne za dunia ili upepo usivume hata kidogo: wala katika nchi, wala baharini, wala kwenye miti.
2我又看见另外一位天使,从日出之地上来,拿着永活 神的印,向那四位得了权柄可以伤害地和海的天使,大声呼喊,
2Kisha nikamwona malaika mwingine akipanda juu kutoka mashariki akiwa na mhuri wa Mungu aliye hai. Akapaaza sauti na kuwaambia hao malaika wanne waliokabidhiwa jukumu la kuiharibu nchi na bahari,
3说:“你们不要伤害地、海和树木,等我们在 神众仆人的额上先盖上了印。”
3"Msiharibu nchi, wala bahari, wala miti, mpaka tutakapokwisha wapiga mhuri watumishi wa Mungu wetu katika paji la uso."
4我听见被盖印的人的数目,以色列子孙各支派中被盖印的共有十四万四千人:
4Kisha nikasikia idadi ya hao waliopigwa mhuri: Watu mia moja arobaini na nne elfu wa makabila yote ya watu wa Israeli.
5犹大支派中被盖印的,一万二千人,流本支派中,一万二千人;迦得支派中,一万二千人;
5Kabila la Yuda walikuwa watu kumi na mbili elfu; kabila la Reubeni, kumi na mbili elfu, kabila la Gadi, kumi na mbili elfu;
6亚设支派中,一万二千人;拿弗他利支派中,一万二千人;玛拿西支派中,一万二千人;
6Kabila la Asheri, kumi na mbili elfu; kabila la Naftali, kumi na mbili elfu; kabila la Manase, kumi na mbili elfu;
7西缅支派中,一万二千人;利未支派中,一万二千人;以萨迦支派中,一万二千人;
7kabila la Simeoni, kumi na mbili elfu, kabila la Lawi, kumi na mbili elfu, kabila la Isakari, kumi na mbili elfu;
8西布伦支派中,一万二千人;约瑟支派中,一万二千人;便雅悯支派中,一万二千人。
8kabila la Zabuloni, kumi na mbili elfu; kabila la Yosefu, kumi na mbili elfu, na kabila la Benyamini, kumi na mbili elfu.
9各国各族的群众前来敬拜这些事以后,我观看,见有一大群人,没有人能数得过来,是从各邦国、各支派、各民族、各方言来的。他们都站在宝座和羊羔面前,身穿白袍,手里拿着棕树枝。
9Kisha nikatazama, nikaona umati mkubwa wa watu wasiohesabika: watu wa kila taifa, ukoo, jamaa na lugha. Nao walikuwa wamesimama mbele ya kiti cha enzi na mbele ya Mwanakondoo, wakiwa wamevaa mavazi meupe na kushika matawi ya mitende mikononi mwao.
10他们大声呼喊,说:“愿救恩归给那坐在宝座上我们的 神,也归给羊羔!”
10Wakapaaza sauti: "Ukombozi wetu watoka kwa Mungu wetu aketiye juu ya kiti cha enzi, na kutoka kwa Mwanakondoo!"
11所有的天使都站在宝座、众长老和四个活物的四周。他们在宝座前,面伏在地上敬拜 神,
11Malaika wote wakasimama kukizunguka kiti cha enzi, wazee na vile viumbe hai vinne. Wakaanguka kifudifudi mbele ya kiti cha enzi, wakamwabudu Mungu,
12说:“阿们!愿颂赞、荣耀、智慧、感谢、尊贵、权能、力量,都归给我们的 神,直到永永远远。阿们!”
12wakisema, "Amina! Sifa, utukufu, hekima, shukrani, heshima, uwezo na nguvu viwe kwa Mungu wetu, milele na milele! Amina!"
13长老中有一位问我:“这些身穿白袍的是谁?他们是从哪里来的呢?”
13Mmoja wa hao wazee akaniuliza, "Hawa waliovaa mavazi meupe ni watu gani? Na wametoka wapi?"
14我对他说:“我主啊,你是知道的。”他告诉我:“这些人是从大患难中出来的。他们用羊羔的血,把自己的衣袍洗洁白了。
14Nami nikamjibu, "Mheshimiwa, wewe wajua!" Naye akaniambia, "Hawa ni wale waliopita salama katika ule udhalimu mkuu. Waliyaosha mavazi yao katika damu ya Mwanakondoo, yakawa meupe kabisa.
15因此,他们可以在 神的宝座前,并且日夜在他的圣所里事奉他。那坐在宝座上的必展开帐幕覆庇他们。
15Ndiyo maana wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Humtumikia Mungu mchana na usiku katika Hekalu lake; naye aketiye juu ya kiti cha enzi atatandaza hema lake juu yao kuwalinda.
16他们必不再饿,也不再渴;太阳和一切炎热必不伤害他们。
16Hawataona tena njaa wala kiu; jua wala joto kali halitawachoma tena,
17因为在宝座中间的羊羔必牧养他们,领他们到生命水的泉源那里。 神也必抹去他们的一切眼泪。”
17kwa sababu Mwanakondoo aliye katikati ya kiti cha enzi atakuwa mchungaji wao, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji ya uzima. Naye Mungu atayafuta machozi yote machoni mwao."