聖經新譯本 (Simplified)

Swahili: New Testament

Revelation

8

1揭开第七个印
1Na Mwanakondoo alipouvunja mhuri wa saba, kukawa kimya mbinguni kwa muda wa nusu saa.
2我看见站在 神面前的七位天使,有七枝号筒赐给了他们。
2Kisha nikawaona wale malaika saba wanaosimama mbele ya Mungu wamepewa tarumbeta saba.
3另外有一位天使来了,拿着金香炉,站在祭坛前。有许多香赐给了他,好与所有圣徒的祈祷一同献在宝座前的金坛上。
3Malaika mwingine akafika, akiwa anachukua chetezo cha dhahabu, akasimama mbele ya madhabahu ya kufukizia ubani. Naye akapewa ubani mwingi autoe sadaka pamoja na sala za watu wote wa Mungu, juu ya madhabahu ya dhahabu iliyo mbele ya kiti cha enzi.
4那香的烟和众圣徒的祈祷,就从天使手中一同升到 神面前。
4Moshi wa ubani ukapanda juu, pamoja na sala za watu wa Mungu, kutoka mikononi mwake huyo malaika aliyekuwa mbele ya Mungu.
5天使拿着香炉,用坛上的火把它装满了,投在地上;于是就有雷轰、响声、闪电和地震。
5Kisha malaika akakichukua hicho chetezo, akakijaza moto wa madhabahuni akakitupa duniani. Kukawa na ngurumo, sauti, umeme na tetemeko la ardhi.
6吹六枝号拿着七枝号筒的七位天使,预备好了要吹号。
6Kisha wale malaika saba wenye tarumbeta saba wakajiweka tayari kupiga mbiu ya mgambo.
7第一位天使吹号,就有冰雹和混杂着血的火,投在地上。地的三分之一烧掉了,树的三分之一烧掉了,所有的青草也烧掉了。
7Malaika wa kwanza akapiga tarumbeta yake. Mchanganyiko wa mvua ya mawe na moto, pamoja na damu, ukamwagwa juu ya nchi. Theluthi moja ya nchi ikaungua, theluthi moja ya miti ikaungua, na majani yote mabichi yakaungua.
8第二位天使吹号,就有一座好像燃烧着的大山,投在海里。海的三分之一变成了血,
8Malaika wa pili akapiga tarumbeta yake. Na kitu kama mlima mkubwa unaowaka moto ukatupwa baharini. Theluthi moja ya bahari ikawa damu,
9海里受造的活物死了三分之一,船只也毁坏了三分之一。
9theluthi moja ya viumbe vya baharini vikafa na theluthi moja ya meli zikaharibiwa.
10第三位天使吹号,就有一颗燃烧着的大星,好像火把一样,从天上落下来,落在江河的三分之一上,和众水的泉源上。
10Kisha malaika wa tatu akapiga tarumbeta yake. Na nyota kubwa ikiwaka kama bonge la moto, ikaanguka kutoka mbinguni, na kutua juu ya theluthi moja ya mito na chemchemi za maji.
11这星名叫“苦堇”。众水的三分之一变为“苦堇”,因水变苦,就有许多人死了。
11(Nyota hiyo inaitwa "Uchungu.") Basi, theluthi moja ya maji yakawa machungu; watu wengi wakafa kutokana na maji hayo, kwa sababu yaligeuka kuwa machungu.
12第四位天使吹号,太阳的三分之一、月亮的三分之一、星辰的三分之一,就都受到击打,以致日月星的三分之一都变黑了,白天的三分之一没有光,夜晚也是这样。
12Kisha malaika wa nne akapiga tarumbeta yake. Ndipo theluthi moja ya jua, ya mwezi na ya nyota ikapata pigo; hata mwangaza ukapoteza theluthi moja ya mng'ao wake. Theluthi moja ya mchana ikakosa mwanga, hali kadhalika na theluthi moja ya usiku.
13我观看,就听见一只在高空飞翔的鹰,大声说:“有祸了!有祸了!住在地上的人有祸了!因为还有三位天使将要吹其余的号。”
13Kisha nikatazama, nikasikia tai akiruka juu kabisa angani anasema kwa sauti kubwa, "Ole, ole, ole kwa wanaoishi duniani wakati malaika watatu waliobaki watakapopiga tarumbeta zao!"